Majibu ya rufaa yangu baada ya kufukuzwa kazi serikalini

Majibu ya rufaa yangu baada ya kufukuzwa kazi serikalini

Poleni na majukumu ndugu zangu Wanafamilia ya Jamiiforum!

Nimerudi Tena kuleta mrejesho na kuomba kuendelea kuongezewa uwezo kwani naamini kuwa humu mpo baba zangu, mama zangu na wengine wengi.
NINAWAHESHIMU na KUWATHAMINI SANA kwa umuhimu wenu.

Mapema mwaka huu Baada ya kutengenezewa tuhuma na kunisababishia nifukuzwe kazi Nilileta taarifa iliyokuwa na kichwa "MKUU WA SHULE NA MZAZI WA MWANAFUNZI WALINITENGENEZEA ZENGWE MPAKA NIKAFUKUZWA KAZI"

Kwa kipindi kile nilikuwa nimekata rufaa ngazi ya TSC Makao makuu na nilikuwa ninasubiri ushughulikiwaji wa rufaa yangu iliyochukua muda mrefu kutokana na tume kusubiri uteuzi baada ya kumaliza muda wake.

NDUGU ZANGU WANAJAMII FORUM; Kwa ukurasa huu ninatumia fursa hii kuwataarifu matokeo ya rufaa yangu baada ya kupitiwa na kutolewa maamuzi.

Rufaa ilipitiwa na nilipewa taarifa iliyonitaka nirejeshwe kazini na tuhuma ianzishwe upya kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu.

Nilipewa majibu ya rufaa yangu japo kwa kuchelewa kidogo kutokana na changamoto za kimawasiliano.

Ndugu WANAJAMII FORUM; kwa sasa nilikwisharipoti kazini katika kituo changu Cha zamani na ninaendelea na Majukumu yangu ya kazi.

Katika ukurasa huu ninaomba sana ndugu zangu mniongezee uwezo kwenye mambo kadhaa muhimu sana;

1. Tuhuma imeanzishwa upya, kosa ninalotuhumiwa nalo ni "KUWA NA TABIA YA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWANAFUNZI YANAYOASHIRIA KUTAKA KUFANYA NAYE NGONO KINYUME NA KANUNI"
** T.S.C Wilaya wameanzisha kesi upya kwa kosa lile lile nililokuwa nimetuhumiwa na kuhukumiwa mwaka Jana.
**Nilipewa notisi na hati ya mashitaka iliyotaka nitoe utetezi ndani ya siku kumi na nne na Nilifanikiwa kuandika na kuwasilisha utetezi ndani ya muda niliopangiwa na kwa sasa ninasubiri mrejesho wao.
Ombi langu katika hili ni ushauri wa namna yoyote ile kutoka kwenu.

2. Barua yangu ya kurejeshwa kazini ilikuwa na nakala iliyotaka Mkurugenzi anirejeshe kwenye payroll ya malipo ya serikali, lakini ni miezi miwili sasa sijarudishwa kwenye payroll. Je nifuate taratibu zipi ili nirudishwe kwenye payroll?

3. Wafanyakazi wezangu katika kituo changu Cha kazi kwa sehemu kubwa ni wale wale waliotumika kutoa ushahidi wa uongo nikafukuzwa kazi, baada ya kurudi nawaona hawako sawa hasa kwa upande wa kunipa ushirikiano na misaada ya kikazi. Je nifanye Nini niendane nao?

NDUGU WANAJAMII FORUM ninawategemea sana katika kuniweka sawa kiakili na kimwili.

Ninatanguliza Shukran zangu za dhati, MUNGU AENDELEE KUWA NANYI NA KUWABARIKI🙏🙏​
USHAURI wangu tafuta wakili rafiki akupe USHAURI wa kisheria.

Huduma za kumuona wakili huwa ni 10,000- 20,000/ kumuona na kukupa USHAURI. Consultation fees

Hapa utapata USHAURI ambao utakuwa wa. Kihisia na siyo wa kisheria.

Suala lako linahusu vifungu vya kisheria.

Mfano, Hiyo hukumu wanasema "

ikaanzishwe upya kwa Kuzingatia taratibu"

Hapo Kuna shida👆

Inaamana mashitaka ya mwanzo yalikiuka hizo taratibu,
Na kama yalikiuka hizo taratibu walitakiwa kujifuta kesi na siyo kutoa agizo wakailete upya.

Wao wahusika (Mkuu wa shule alipaswa ) kama wasingeridhika na hukumu walipaswa wakate RUFAA.

Sasa kwa hukumu hiyo ya kuwataka wakarekebishe ili kesi uendelee maana yake hii ya kwanza umeshinda kwa kigezo cha kuwa hawakufuata Sheria.

Sasa wakienda KUIREKEBISHA hiyo dosari wakaileta upya Kuna mawili

Ushahidi ukiwa upo wa kutosha uutashindwa kesi.

Au ushahidi ukiwa hafifu utashinda kesi.
 
Je kwa Mtumishi aliyeshinda kesi tume ya Utumishi arudishwe kazini, Mwajiri hajaridhika kakata rufaa Ofisi ya Rais, je huchukua muda gani majibu kutoka? Na je Maamuzi ya Tume ya Utumishi yanaweza tenguliwa?
 
Sijawahi hata kumtongoza mtoto ninayetuhumiwa naye. Hata mara ya kwanza walitumia ushahidi wa kulazimisha Tena kwa nguvu mpaka za polisi
Usirudie Tena kutaka watoto wa shule hata kuwakonyeza! Utakuwa kulikuwa una utani na huyo mtoto.
 
Back
Top Bottom