Majibu ya watu walionitafuta kuhusu komenti ya biashara Kariakoo

passion_amo1

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2023
Posts
1,828
Reaction score
3,922
Wakuu habari za uzima?

Kuna uzi mmoja jamaa alianzisha kama sikosei ni Goodluck7 akiuliza biashara ya mtaji wa milioni 2.

Nilitoka komenti yangu kuhusu kuja Kariakoo kufanya biashara kwa pesa hiyo.

Nilipokea Pm nyingi sana lakini sikujibu hata moja sababu PM yangu haifunguki na nilishalalamika sana hakuna msaada niliopata.

Nilijibu baadhi ya watu na kuwawekea mawasiliano, kwa sasa sipo Dar es Salaam nasimamia biashara yangu mpya ya urembo wa magari.

ILA niseme tu JF wengi watu hawapo serious.

Nilitoa maelezo jinsi ya kupata meza, huwezi kupata meza bila kupitia kwa madalali waliopo Kariakoo wanafahamu hilo. Meza zinaanzia laki moja mpaka laki tatu kwa mwezi zinategemea na ni eneo gani unahitaji uweke biashara yako.

Nilitoa namba ya dalali na unafika kuhakikisha Eneo ambalo unahitaji, ila sana sana nimeendelea kupokea meseji tu.

Kama kweli unataka kufanya biashara acha kuuliza kwenye mitandao fika eneo kutana na madalali uongee nao.

Cha mwisho ni kuwa makini utapeli upo.

Nawatakia asubuhi njema.
 
asant kiongozi umetufungua akili kwa kias fulan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…