Majigambo ya Humphrey Polepole na V8 ndiyo yaliyochagiza ununuzi wa magari ya kifahari kwa Ma-DED na Taasisi nyingine

Majigambo ya Humphrey Polepole na V8 ndiyo yaliyochagiza ununuzi wa magari ya kifahari kwa Ma-DED na Taasisi nyingine

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana JF.

Ukiangalia kwa umakini unaweza kuona maDED kama wameonewa vile kwa sababu chama chenyewe kupitia katibu mwenezi mstaafu ndiye kinala wa uchochezi kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kuna kiclip moja HP alitamba sana kuwa viongozi wengi hata wa hali yA chini wanatumia magari makali sana kiasi cha kutofikiwa na mtu yeyote.

Kiukweli magari ya viongozi wa CCM mengi ni VXR yaani yanafikia gharama ya million490 sasa ukiangalia hawa watu wanaopigania kupunguza matumizi kiuzalendo hapa wanakwama wapi kutoonyesha wanavyokula maraha na magari ya bei mbaya huku hospital zikikosa dawa.

Au pesa ya chama aina matumizi mengine mpaka wanunue maV8 . Napata ukakasi kwamba hii clip ya HP ilitoka bahati mbaya au ndivyo walivyo wangata na kupuliza.

Kama aliteleza basi atuombe samahani na Ma-DED waombewe samahani haya magari yote yapigwe mnada tununue ya million 108 kutoka China wanayotumia mapolisi kwani nayo mazuri.
 
Ngoja niulize swali la kizushi kama vile mwanafunzi wa Form One, "Je hivi unatakiwa usome kombi (combi) gani, ili mtu uweze kuteuliwa na kuwa DED wa wilaya na ku-enjoy hayo magari Ma-VXR ? "
 
CCM inaingiza zaidi ya sh bilioni 55 kwa mwaka na ina uwezo hata wa kununua ndege bwashee!
Wivu wa nn sasa kwa Ma DED?? Na hao ndiyo waliohakikisha ccm inapata ushindi kwa gharama yeyote ile. Inawezekana walitumia nguvu kupita kiasi kwa ushirika wa Vyombo vya Dola.
 
Wivu wa nn sasa kwa Ma DED?? Na hao ndiyo waliohakikisha ccm inapata ushindi kwa gharama yeyote ile. Inawezekana walitumia walitumia nguvu kupita kiasi kwa ushirika wa Vyombo vya Dola.
Hakuna wivu wowote bwashee ni kanuni xa serikali tu!
 
Wana JF.

Ukiangalia kwa umakini unaweza kuona maDED kama wameonewa vile kwa sababu chama chenyewe kupitia katibu mwenezi mstaafu ndiye kinala wa uchochezi kwa matumizi mabaya ya fedha za umma. Kuna kiclip moja HP alitamba sana kuwa viongozi wengi hata wa hali yA chini wanatumia magari makali sana kiasi cha kutofikiwa na mtu yeyote. Kiukweli magari ya viongozi wa CCM mengi ni VXR yaani yanafikia gharama ya million490 sasa ukiangalia hawa watu wanaopigania kupunguza matumizi kiuzalendo hapa wanakwama wapi kutoonyesha wanavyokula maraha na magari ya bei mbaya huku hospital zikikosa dawa. Au pesa ya chama aina matumizi mengine mpaka wanunue maV8 . Napata ukakasi kwamba hii clip ya HP ilitoka bahati mbaya au ndivyo walivyo wangata na kupuliza. Kama aliteleza basi atuombe samahani na Maded waombewe samahani haya magari yote yapigwe mnada tununue ya million 108 kutoka China wanayotumia mapolisi kwani nayo mazuri.
Shira iko hivi,kuna ule ukoo wanasema baba mwizi,mama mwizi na mtoto mwizi.
 
CCM inaingiza zaidi ya sh bilioni 55 kwa mwaka na ina uwezo hata wa kununua ndege bwashee!
Wewe mjamaa sijui mlevi!! Pole Pole alisema wanayo Mahela mengi kufanya lolote, MaDED kupitia madiwani wakayachungulia wakajisevia sasa wanalaumiwa kwa nini wakati wamemuiga Polepole HP. Nao acha wajipongeze kwa kufanikisha ushindi wa kushindilia
 
Back
Top Bottom