GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,337
Katika hali ya kusikitisha waafrika bado tunaonekana kuendelea kuamini imani mbovu mbovu.baada ya kubainika kuwa ile team ya majimaji jana ilikuja uwanjani ikiamini kuwa mashambulizi ya team ya simba langoni mwao yatageuka kuwa maji.
Kocha wa majimaji ambaye alikuja na tambo za kuwa yeye simba hawampi shida ni team tu kama team nyingine huku akiwa amewajaza ujinga wachezaji wake kama alivyofanya kinjekitile mwaka 1905-07 katika vita vya majimaji.
Wachezaji walikuja na ari kubwa wakiamini kabisa kuwa mashambulizi ya simba katika miili yao yatageuka maji hivyo wakaingia msituni katika pori la taifa linalojulikana zaidi kama okwi stadium kuwa kwa kutumia fimbo wangeweza kumuua mnyama simba. Waliingi katik pori hilo huku wakimtafuta mnyama na kuimba maji maji.hata walipoanza kushambuliwa na mmoja mmoja kuraruriwa walikuwa wakipiga kelele "maji maji'
Hali ilipowazidia walibadilisha mlio na kijikuta wakiita " mma mma" na hatimaye kujikuta wameraruriwa na mnyama huyo aliyekuwa na njaa. Mwishowe vijana na wazee waliamua kulikimbia pori hilo na kurudi vijijini kwao kwa majonzi makubwa.
Hili ni funzo kwa tamaduni zetu kuwa tunapaswa kujiandaa kiukwel kwel kupambana na si kutumia imani mbovu mbovu.