Elections 2010 Majimbo 21 yatakayochukuliwa na CHADEMA kabla ya oct 31

Haya si ndio mambo ambayo Kaimu Mkurugenzi wa Daily News, Nd. Mkumbwa aliandika kuhusu matokeo ya urais akashutumiwa na kila mpenda demokrasia nchini? Hatujafika tarehe 31 October tayari Fanfa anatangaza matokeo ya uchaguzi majimboni. Let us be realistic.
 
Mbona mbeya mjini hujaliweka?
Mpesya anapumulia mashine kule
Kweli mkuu hili jimbo kalisahau hali ya CCM kule Mbeya ni ya kukatisha tamaa maana Chadema wanakunywa mpaka uji wa mgonjwa
 
Red alert:
Huyu ni Engineer toka Bank Kuu ya Tanzania,Anapita bila kupingwa,watu wa Siha wamemchoka Aggrey Mwanri vibaya mno.Anapumulia icu.
 
Umesahau Said Arfi (Chadema) wa Mpanga kati ambae hata meneja wa kampeni wa ccm amejikuta akimpigia debe (source Tanzania Daima la leo), lakini pia Sumbawanga mjini Aeshi wa CCM anapumulia mashine kwa Norbet Yamsebo wa Chadema anaeungwa mkono hata na mzee wa mji Mzindakaya.
 
Wee kweli ni fanfa, yaani umeacha majimbo kibao kwa mfano anakotoka makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. S. Arfi au humfahamu??? Sumbawanga mjini, Mbozi, Mbeya mjini, Kawe, na orodha inaendelea....
jimbo la chalinze,bagamoyo,muheza,handeni, monduli,bagamoyo,lushoto,mwanga, same mashariki&magharibi,chamwino,dodoma mjini,simanjiro,rungwe mashariki&magharibi,kyela aaaaaaahhh jamani mbona yapo mengi mmeshindwa kuyataja?
na hii ni kwa mujibu wa utafiti makini wa SYNOVATE..

CHADEMA HOYYYY........EEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 

Majimbo yote ya Chadema weka tick kuanzia leo, labda kwa yale ambayo hawana wagombea kabisa!
 

Tathimini yako mkuu iko sahihi kabisa na wala hujapinda ukweli. Ndio maana nilisema nguvu zaidi inahitajika kwa CHADEMA kuhakikisha Hukumu ya wapiga kura INAKAZIWA maana wameshaamua.
 
Wanaoshabikia ccm ama ni wajinga sana au maskini sana na ni rahisi kuwa- manipulate. Mtu mjinga hawezi kuhusisha siasa za chama na maisha yake kuwa magumu. Mtu maskini sana aweza kuuza kura yake kwa t-shirt, kofia , shs 5000/=. wengine wanaoshabikia ccm ni beneficiaries wa system. wameneemeka kwa mfumo wa kifisadi na hawako tayari kuupoteza mfumo huo kwani watakula wapi Dr Slaa akichukua nchi.
 

Swala la kuiba kura ni kitu kingine na hali halisi ya kisiasa ni kitu kingine. Ndio maana tunasema kura zilindwe kwa gharama yoyote katika majimbo yaliyotajwa na yanayoendelea kutolewa tathimini. Lakini pia kuhamasisha watu wapige kura. Ahsante kwa angalizo lako
 
Wakuu msisahau Mpanda Kati na vijijini wagombea wa Chadema wanafunika ile mbaya. Pia nasikia Sumbawanga mjini wale wa Tshirt za kijani wameshikwa pabaya.
 
Ahsante sana kwa kumtakia mema mtoto wa watu, najua unaonge kinyume!

Fuatilia siasa za kule Kigoma kaskazini utagundua nafasi yake. Kuna mambo kadhaa yamemuharibia ikiwemo kuwa nje ya jimbo kwa muda mrefu, kuonyesha nia ya kugombea majimbo mengiine na nguvu ya wagombea wa vyama vingine vya upinzani.

Sina shaka na kiti cha Hai kwa Mbowe lakini tarime yule jamaa aliyehama kutoka Chadema atakuwa na athari mbaya.

Huyo Mtema akikaa na upinzani wa kwenye Keyboard (JF) ubunge atausikia redioni.

Unakumbuka Lyatonga alivyoshinda ubunge Temeke, ilikuwa hakuna kulala wala longo longo kwenye vyombo vya habari. Ni nyumba kwa nyumba, kijiwe kwa kijiwe kila siku. Ni kwa staili hiyo ndio unaweza kuishinda CCM.

Nautakia kila la heri upinzani lakini inabidi watu wafahamishwe uhalisia ulivyo huko majimboni na kama hilo wengine hampendi kulisikia, tuvumiliane.
 
Hamuwafahamu CCM kwenye ballot box. Muulize Dr Mvungi aliyegombea Urais kwa tiketi ya NCCR mwaka ule. Hakuiona hata kura aloojipigia yeye mwenyewe pale Chuo.
WildCard Mkuu umenena CCM ni Mafia wa wizi wa kura!
 


We jamaa wa ajabu sana mimi huwa sikuelewi yani upo kama CHAJA YA KOBE au SIGARA KALI.

Kasome tena hiyo hoja hapo juu, huyu muungwana nia yake ilikuwa ni kufahamu majimbo mangapi chadema wana uwezekano wa kuyachukua na yeye akasema hayo 31 na akataka na wengine waseme wanayo yajua.

NA MWISHO AKAOMBA UONGOZI WA CHADEMA HUWEKE MKAKATI WA KULINDA NA KUAKIKISHA HAYA MAJIMBO AU MAYAI YANA TOTOA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…