Majina ajira za Ualimu 2014 haya hapa

Majina ajira za Ualimu 2014 haya hapa

Status
Not open for further replies.
Jaslaws, kumbuka kuwa Ualimu ndio fani mama, wacha watu waendelee kuipenda, pamoja na kuwa ni kazi isiyokuwa na malipo/maslahi mazuri ila ina exposure, kupitia ualimu wengi wao hufikia malengo yao ya kielimu, ndio maana wengi wa maprofesa ni walimu

heri nisukume mkokoten kuliko kuwa mwalimu Tanzania...... Hii serikali haina maana kabisa. Kama mawazir wenyew mizigo wamefoji vyeti hawajui chochote watakuwa na fikra za kujali kaz mama kama ya ualimu...... Naona aibu kuitwa mtanzania
 
jaman weken moja yabadilishen hata kwenye word maana hzo link hazfunguki
 
watu8, ukiondoa walimu hawa 12688, ambao majina yao tayari yamekwisha toka na wao kupangiwa Halmashauri za kwenda kufanya kazi, walimu wanaobaki ni wa shule za msingi (17,928) jumlisha walimu wenye diploma (5,416) = 23,344/= ndio ambao bado hawajafahamu hatima ya ajira zao, nadhani ndio hawa wanahaha kufahamu wamepangwa wapi. Kwa ufupi mwaka huu Wizara ya TAMISEMI + Wizara ya Elimu wataajiri walimu 36,021/= tu. Hivyo basi kwa wastani wahitimu kwa kila mwaka huenda sambamba na idadi ya wanaoajiriwa mwaka husika/unaofuata.Yaani serikali kila mwaka huchukua records za wahitimu woote katika vyuo vyoote vya elimu na karibia woote huajiriwa.
Hivi kwa wastani kwa mwaka mmoja wa masomo huwa kunakuwa na wahitimu wangapi wa ualimu kwa ngazi zote?

Maana haya matokeo ya upangiwaji ajira za ualimu yamekuwa yakingojewa kwa hamu sana...
 
Ngahekapahi, Kwa utaratibu wa TAMISEMI/MOE walimu wa Certificate na Diploma kwa pamoja waliwekwa kwenye first batch, na walimu wa ngazi ya shahada(Degree) wamewekwa kwenye second batch.
What I see ni Kwamba hiyo ni second batch. First batch ipo wapi?

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Gogadi, naendelea kuwasiliana na source ya hayo majina ya Diploma na Certificate ili tuweze kuyaweka jukwaani ila changamoto mdau (source) yupo mbali sana na server yenye majina hayo si unajua leo weekend mzee, ila kasema muda wowote anaweza kwenda kwa ofisi atanirushia na ww utafaidi kuyaona kupitia hii thread
Brother James...tuwekee na ya stashahada pia hongera sana kwa kuleta taatifa nzuri na nyeti kama hizo...umechukua points zangu zote kiongozi
 
Uboya, soma taarifa hiyo hapo chini:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14
Jumla ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) ifikapo tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika shule za Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo
5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada). Orodha rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa itatangazwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) ifikapo tarehe 15 Machi, 2014. Walimu wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri walikopangiwa ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja. Inasisitizwa kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi zifanyiwe kazi na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili 2014 na hivyo kuepukaulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza ajira. Mwalimu yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za msingi zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo.
Ikumbukwe kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa mahitaji ya walimu. Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba na nauli ambazo zitalipwa kwa kila Mwalimu atakayeripoti kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri walikopangwa walimu hao. Hivyo, kila mwalimu
anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri alikopangwa. Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kufanya kazi walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho baada ya mwalimu kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.
Ni vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya. Walimu ambao tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao na kuendelea na kazi.
IMETOLEWA NA
JUMANNE A. SAGINI

KATIBU MKUU

OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI

mbona haioneshi tarehe ya ku report kituoni?
 
Ngahekapahi, Kwa utaratibu wa TAMISEMI/MOE walimu wa Certificate na Diploma kwa pamoja waliwekwa kwenye first batch, na walimu wa ngazi ya shahada(Degree) wamewekwa kwenye second batch.

Nashukuru mkuu kwa maelezo hayo maana mimekuwa nikitazama majina ya baadhi ya ndugu zangu sikuona na wana degree so nikadhani may be wanaweza kuwa Kwenye first batch.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Wapendwa hayo majina yanaonekanaje nimehangaika sana plz your help
 
Ngahekapahi, usikate tamaa kama hukuyaona majina yao kwani maranyingi kwa miaka iliyopita tumeshuhudia majina ya watu yakikosewa hivyo basi kwa bahati mbaya yawezekana majina unayoyatafuta yakawa yamewekwa kwenye first batch kimakosa kwani ni mara nyingi tu kimetokea kitu kama hicho, hembu tusubiri first batch itoke kwa ajili ya kujiridhisha zaidi
Nashukuru mkuu kwa maelezo hayo maana mimekuwa nikitazama majina ya baadhi ya ndugu zangu sikuona na wana degree so nikadhani may be wanaweza kuwa Kwenye first batch.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Ngahekapahi, usikate tamaa kama hukuyaona majina yao kwani maranyingi kwa miaka iliyopita tumeshuhudia majina ya watu yakikosewa hivyo basi kwa bahati mbaya yawezekana majina unayoyatafuta yakawa yamewekwa kwenye first batch kimakosa kwani ni mara nyingi tu kimetokea kitu kama hicho, hembu tusubiri first batch itoke kwa ajili ya kujiridhisha zaidi

Shukrani mkuu.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
watu8, ukiondoa walimu hawa 12688, ambao majina yao tayari yamekwisha toka na wao kupangiwa Halmashauri za kwenda kufanya kazi, walimu wanaobaki ni wa shule za msingi (17,928) jumlisha walimu wenye diploma (5,416) = 23,344/= ndio ambao bado hawajafahamu hatima ya ajira zao, nadhani ndio hawa wanahaha kufahamu wamepangwa wapi. Kwa ufupi mwaka huu Wizara ya TAMISEMI + Wizara ya Elimu wataajiri walimu 36,021/= tu. Hivyo basi kwa wastani wahitimu kwa kila mwaka huenda sambamba na idadi ya wanaoajiriwa mwaka husika/unaofuata.Yaani serikali kila mwaka huchukua records za wahitimu woote katika vyuo vyoote vya elimu na karibia woote huajiriwa.

Mkuu Brother James

Kwanza haya majina yapo 12,666,sio 12,688 kama unavyosema..

Nimejaribu kupitia majina haya naona jina langu halimo...! sasa naomba unisaidie kupata ile orodha ya wakufunzi,nina

wasiwasi naweza kuwemo kule,kwa sababu nimesoma BED..!

Shukrani !
 
Last edited by a moderator:
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OWM - TAMISEMI)

AJIRA MPYA YA WALIMU WA PYA KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013/14.

A: OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI I NATANGAZA ORODHA YA WANACHUO WAHITIMU WA MAFUNZO YA UALIMU KAMA IFUATAVYO:-

i. Wa limuwa Cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 17,928

ii. Walimu wa Stashahada kwa ajili ya shule za sekondari 5,416

iii. Walimu wa Shahada kwa ajili ya shule za sekondari 12,677

Walimu hawa wamepangwa katika Halmashauri na shule za mazoezi za vyuo vyaualimu Tanzania Bara
.
B:Kila Mwalimu ( Ajirampya) atatakiwakuzingatiayafuatayo:-
1.Kuripoti tarehe 01/04/2014 kwenye ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwaajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi.

2.Mwalimu atatakiwa kuwa na vyeti vyake halisi vyachuonaSekondari

3.Walimu ambao ni waajiriwa wa Serikali waliokuwa wanajiendeleza kielimu wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao ili kuendelea na kazi.

4.Fedha za kujikimu za siku saba (7) na nauli kwa walimu wapya zimetumwa katika Halmashauri waliko pangwa walimu. Hivyo, kila mmoja aripoti katika Halmashauri aliyopangwa.

5.Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 10/04/2014 hatapokelewa Atena na atakuwa amepoteza ajira yake.

Ajira Mpya za Walimu Angalia Hapa
 
The Magnificent, upo sawa kabisa, kuna jumla ya watu 11 (12,677-12,666) ambao hawaonekani kwenye list hiyo ya TAMISEMI, bila shaka watakuwa ni wale waliopelekwa kwenye ukufunzi kwani walimu wanaotakiwa kuajiriwa (kauli ya katibu mkuu-TAMISEMI) kwa ngazi ya degree ni 12,677 na hadi sasa tumeona jumla ya majina ya watu 12,666, watu kumi na moja (11) wanakosekana. Niungane na ww kuwa yawezekana kabisa kuwa hao walimu 11 wataajiriwa na wizara ya elimu kama wakufunzi wa vyuo vya ualimu. Kwa taarifa zaidi tuendelee kuwa na subira.

Back
Top Bottom