John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Majina Mbalimbali ya Mungu
Kwa nini majina tofauti
Mungu ni mmoja tu, lakini katika umoja wake amekuwa akijifunua katika majina mengi, kulingana na uweza wake alio nao, au majira fulani yaliyopita, au matukio ya namna tofauti tofauti yaliyotokea.
Mifano ya majina tofauti kwa mtu yule yule
Ni kama vile, rais fulani aitwe John, lakini huyo huyo anaweza akaitwa baba sehemu fulani, akaitwa mjomba sehemu nyingine, mhandisi kwa watu fulani, amiri jeshi mkuu eneo fulani, babu sehemu nyingine, n.k.
Utaona kuwa vyeo vyote hivyo vimekuja aidha kulingana na wakati, au matukio, au nafasi aliyopo au ujuzi alio nao, n.k. Mtu huitwa kwa majina hayo yote, kwa nyakati tofauti. Ndivyo ilivyo pia kwa Mungu wetu. Alijifunua katika majina mbalimbali. Hebu tutazame majina hayo, japo kwa ufupi.
Mungu ni jina linalotumika kwa anayesadikiwa katika dini kuwa na uhai wa hali ya juu.
Katika somo hili, Mungu anayezungumziwa ni Mungu wa Mbinguni, Muumba mbingu na nchi, MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:13-15).
Majina tofauti ya Mungu (majina yote ni kwa lugha ya Kiebrania)
1. MIMI NIKO AMBAYE NIKO: Mungu afunua jina lake takatifu (Kutoka 3: 13-15)
2. ADONAI: Mungu Mwenye enzi yote, kimbilio imara (Mwanzo 15:2‐8, Kut 6:2‐3)
3. EL-ELYONI: Mungu aliye juu zaidi (Mwanzo14:18, Dan 4:34)
4. ELOHIMU: Mungu mwenye uweza, muumbaji wa milele, mwenye nguvu (Mwanzo 1:1, 17:7, Yeremia 31:33)
5. YEHOVA EL–SHADAI: Mungu Ututoshelezaye (Mwanzo 17:1)
6. YEHOVA EL-OHEENU: Bwana Mungu Wetu (Zaburi 99:5, 8-9)
7. YEHOVA EL-GIBBORI: Mungu Mwenye Nguvu (Isaya 9:6)
8. YEHOVA-MEKADISHKEMU: Bwana atutakasaye (Kutoka 31:13)
9. YEHOVA-NISI: Mungu ni Bendera yetu (Berani ya vita) (Kutoka 17:13-16)
10. YEHOVA OLAMU: Mungu wa milele (Zaburi 90:2)
11. YEHOVA-RAFA: Mungu Atuponyaye (Kutoka 15:26)
12. YEHOVA-ROHI: Bwana ndiye mchungaji wangu (Zab 23:1)
13. YEHOVAH SABAOTHI: Bwana wa Majeshi (1Samweli 1:3)
14. YEHOVA SHALOM: Bwana ni Amani Yangu (Waamuzi 6:23-24)
15. YEHOVA SHAMA: Bwana Yupo Hapa (Ezekiel 48:35)
16. YEHOVA TSIDKEMU: Bwana ni Haki Yetu (Yeremia 23:6)
17. YEHOVA-YIRE: Mungu atupaye (Mwanzo 22:14).
18. YE-SHUA (YESU): Mungu utuokoaye (Mathayo 1:21)
Jina Hili la YESU ndilo jina tulilonalo hadi sasa. Kwa kupitia jina Hili ndiyo tunapata wokovu. Kwa jina Hili, ndiyo tunamshinda adui. Kwa jina Hili, ndiyo tunapata baraka, na kwa jina Hili, ndiyo tunaishi.
Hivyo, Mungu ni mmoja tu, lakini ana majina mbalimbali, kulingana na uweza wake, majira fulani yaliyopita, au matukio yaliyotokea katika namna tofauti.
Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake (Dan 2:20).