Majina mengine jf!!!

Kindimbajuu hili ni jina la kijiji huko wilaya ya mbinga mbele kidogo ya kijiji kinaitwa Rwanda ukiwa unaelekea direction ya Lituhi. Hivyo inawezekana huyu jamaa anayejiita jina hili anatokea huko.

Aksante mkuu kwa kutuhabarisha, je lakwako linamaana gani?
 

10. Kyachakiche;
11. Bwabwa
 
13.Omwana
 
Acha masihara lini uliona mbwa amevaa chupi?Au unamaanisha ni chupi /bikini iliyotokana na ngozi ya mbwa?

huyu amezaliwa bongo anajifunza kichaga

itei tei ni ndenga/ama sehemu ya chini ya uzazi unaohifadhi mbegu za kiume

kitee ni mbwa

haya jibu mwenyewe

a)CHUPI YA MBWA
B)NDENGA ZA MBWA
C)SEHEMU ZA CHINI ZA MBWA
D)B & C NI SAWA
 
10. Kyachakiche;
11. Bwabwa

Mkuu ukipitia mada hii kutoka mwanzo huko katikati maana ya jina lililokolezwa hapo juu imeshatolewa. Ila kwa kukusaidia tu ni, ISIYO JALI!
 
Gangilonga ni jiwe moja kubwa sana ambalo liko Iringa mjini eneo moja ambalo pia huitwa gangilonga. Enzi za mababu walikuwa wanasema jiwe hilo lilikuwa linaongea hivyo watu walikuwa wanaenda kuabu na kusema shida zao. Binafsi na wenzangu enzi hizo tukiwa pathfinder tulikwea jiwe hilo, juu ni tambarare, lina eneo kubwa kama sikosei watu zaidi ya 200 wanaweza kukaa na pia kuna majina mengi ya watu mbalimbali waliwahi kulikwea jiwe hilo. Vile vile kuna chemichemi nzuri ya maji. nakumbuka tulikwenda na vyakula vyetu vibichi tukavipikia huko juu ya jiwe na kutumia yale maji masafi ya chemichemi kwa kupikia na kunywa.

Kama mpaka sasa uharibifu wa mazingira haujajitokeza eneo hilo lilikuwa ni zuri sana kwa picnic na utalii. Gangi = Jiwe; Longa = sema/ongea. Gangilonga Jiwe lisemalo.
 
Aksante kwa kutuelimisha mkuu, nimekugogea pia senksi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…