Gangilonga ni jiwe moja kubwa sana ambalo liko Iringa mjini eneo moja ambalo pia huitwa gangilonga. Enzi za mababu walikuwa wanasema jiwe hilo lilikuwa linaongea hivyo watu walikuwa wanaenda kuabu na kusema shida zao. Binafsi na wenzangu enzi hizo tukiwa pathfinder tulikwea jiwe hilo, juu ni tambarare, lina eneo kubwa kama sikosei watu zaidi ya 200 wanaweza kukaa na pia kuna majina mengi ya watu mbalimbali waliwahi kulikwea jiwe hilo. Vile vile kuna chemichemi nzuri ya maji. nakumbuka tulikwenda na vyakula vyetu vibichi tukavipikia huko juu ya jiwe na kutumia yale maji masafi ya chemichemi kwa kupikia na kunywa.
Kama mpaka sasa uharibifu wa mazingira haujajitokeza eneo hilo lilikuwa ni zuri sana kwa picnic na utalii. Gangi = Jiwe; Longa = sema/ongea. Gangilonga Jiwe lisemalo.