Majina, misemo na maneno kwenye khanga

Siku utavaliwa iliyoandikwa... Ndefu Tamu fupi inakera... sijui utajichungulia...
 
Mmmmh mkuu au ulimaanisha tujikumbushe misemo ya kwenye khanga...... Kuna uhalisia kweli??!
 
Ukisusa wenzio wala, MI NDIO NILIKULA SIKU HIYO
 
Kuna jamaa kamnunulia mama mkwe mtarajiwa khanga imeandikwa 'panua paja mkwaju waja'. Uhusiano umikatizwa siku hiyo.
 
hahahaha ila na wewe nimswahili sana kila khanga akiivaa unaisoma umenikumbusha nisome kagha zangu zimeandikwaje maana zinachakaa isijekuta navaa zina matusi
 
Ukweli ni kwamba sipendi na sijawahi kuelewa haya mambo...

Ngoja tuwaachie wenye ngoma zao waserebuke!
 
Dah nilienda visiwani kikazi. Nikaingia kwenye chumba cha hoteli. Kitandani nikakuta kangha nzuriii, mpya. Rangi ya nyeupe na nyekundu! maneno yake ualikuwa kama ifuatavyo:
' NI KWELI LAKINI HAYAKUHUSU'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…