Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema jumla ya wanafunzi 149,818 sawa na asilimia 69.96 wakiwemo wasichana 76,491 na wavulana 73,327 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule za sekondari za serikali 694.
Akitoa taarifa kwa umma Ijumaa Juni 6, 2025 Jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema kati ya hao, wanafunzi 1,728 wakiwemo wasichana 801 na wavulana 927 wamepangwa katika shule za sekondari 08 zinazopokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi.
Wanafunzi 6944 wakiwemo Wasichana 3353 na Wavulana 3591 wamepangwa katika Shule za Kutwa.
Wanafunzi 2875 wakiwemo Wasichana 1057 na Wavulana 1818 wachaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika Vyuo nne vya Elimu ya Ufundi, Vyuo hivyo ni pamoja na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo cha Maendeleo ya Jamii (WMDI)
Wanafunzi 2214 wakiwemo Wasichana 1099 na Wavulana 1015 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya ngazi ya Stashahada.
Wanafunzi 1609 Wasichana 443 na Wavulana 1166 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ualimu Kozi za Stashahada.
Wanafunzi 57,625 Wasichana 18,427na Wavulana 39,198 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Kada mbalimbali nchini.
Aidha, Mchengerwa ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa azma ya serikali ya kuwa na shule za sekondari za kidato cha tano katika kila tarafa inatekelezwa, ili wanafunzi wote wanaofaulu Mtihani wa Kidato cha Nne wapate nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.
WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI NA VYA KATI - 2025 (FIRST SELECTION)