Majina ya Magari ya TOYOTA Na maana yake

Ngoja nitafakari hapo kwenye Toyota Alteza alafu nijitathmini nafaa kumiliki Alteza hau niiteme.
 
Sisi wenye mikokoteni ya diblo tunafanya nini hapa
 
Kuna hii Toyota ISIS sijui waliingia ubia na magaidi?
 
Hapa ndio naomba mnitoe tongo tongo wakuu Kuna landcruicer V8 Ina speed 180 kph alafu ni ya mwaka 2019 alafu Kuna 260kph pia ya mwaka huo huo je tofauti hapa ikoje ?
Inawezeka ni electronically limited kwa sababu za kiusalama watundu wakichakachua inaweza kwenda zaidi ya hapo,GXV8-240km/h(diesel),VXV8-260km/h(petrol) kuna toleo baada ya hizi zina 180km/h.
 
Tatizo watu wanaandika uzi hawasemi wamekopi wapi.

Kuna mtu alileta huu uzi humu na ameuweka kama wake na hapa huyu kauleta kama wake hajasema alipoutoa.
 
Mwanzoni mwa miaka ya tisini nilifanya kazi kwa muda mfupi kwenye karakana mojawapo ya Toyota pale Toyota city Nagoya. Elewa kuwa magari ya Toyota huwa hayaundwi sehemu moja, kila gari lina kiwanda chake tofauti, kwa mfamno miaka hiyo kiwanda cha Carina kilikuwa Tokyo, wakati kiwanda cha Corolla kilikuwa hapo hapo Toyota City (Aichi), Nagoya.

Chanzo cha kampuni hii ni kwenye mashine za kufuma nguo (looms) ambazo ndiyo ilikuwa biashara kubwa ya Sakichi Toyoda; babu wa Toyota. Jamaa huyu aliamua kumsomesha mtoto wake Kiichiro Toyoda elimu ya Mechanical Engineeringi huko MIT marekani kusudi akirudi aweze kuboresha mashine zao za kusuka nguo walizokuwa wanatengeneza wakati huo. Hata hivyo Kiichiro akiwa marekani, aliona Ford wakitengezea magari na akapenda sana kujiingiza kwenye biashara ya magari, kwa hiyo siku moja akiwa mwanafunzi wa MIT alitembelea kiwanda cha Ford huko Detroit na kupiga picha nyingi sana za production process. Kwa vile alikuwa na elimu nzuri ya engineering, ilikuwa ni rahisi kwanye kufanya reverse engoineering kutoka kwenye picha hizo. Alivyorudi japan, akajikita kwenye utegenezaji wa magari badala ya kutengeza mashine za kufuma nguo. Gari la kwanza alilotengeneza lilikuwa lionyeshwe kwa mfalme lakini kwenye safari yake ya kutoka Nagoya kwenda Tokyo likavunjia crankshaft mara nyingi sana; iliwachukua zaidi ya siku kumi kulifikisha Tokyo. Hata walipofika Tokyo, bado crankshaft nyingine ilivunjika wangali kwenye uwanja wa maonyesho. Mfalme akaagiza kuwa utawala wake uisadie Toyoda ili iweze kufikia lengo lake la kujenga magari Japan. Walibadilisha jina kutoka Toyoda kuwa Toyota kwa sababu walidhania Toyoda ilikuwa haisikiki vizuri kwa watu wasikuowa wajapani; hakukuwa na maana ya bahati au nini.

Majina ya magari yote ya toyota hubuniwa kwa ajili ya kuvutia soko tu, at least mpaka mwaka 1994; huwa hayatokani na lugha ya kijapani. Kwa mfano Land-Cruiser ilibuniwa ili kushindana na Land-Rover, Carina ilikuwa designed kushindana na Ford Cortina.
 
Tatizo watu wanaandika uzi hawasemi wamekopi wapi.

Kuna mtu alileta huu uzi humu na ameuweka kama wake na hapa huyu kauleta kama wake hajasema alipoutoa.
Nimeutoa kwenye channel yangu YouTube
 
Nimesoma kwa uzuri ila nilicho elewa ni kuwa kwenye maana fulani ya neno huwa na nadharia nyingi sana.
Hapo kila mtu huja na yake
 
Nimesoma kwa uzuri ila nilicho elewa ni kuwa kwenye maana fulani ya neno huwa na nadharia nyingi sana.
Hapo kila mtu huja na yake
Sikuja na maana ya kwangu bali nimekuambia niliyotoa Toyota City mwaka 1994. Kama yako ni ya baada ya mwaka 1994, basi uko sahihi ila kama ni tafsiri ya historia nzima ya majina ya Toyota, basi fanya review tena. Hata kubadilisha jina kutoka Toyoda kuwa Toyota ilikuwa ni kwa sababu ya soko tu
 
Kwahiyo wewe ndiye umeibiwa? Utafute humu utaukuta umeletwa na mtu kabla yako
Nilijaribu kuserch sikupata ila huenda ukawa na title tofauti.
Lakini ni vyema maana ni moja ya njia ya kushare Idea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…