NAWATAFUNA
JF-Expert Member
- Nov 14, 2019
- 13,284
- 24,047
Mzee Mohammed Said namuheshimu kwa jitihada zake za ubobezi kwenye historia ya Uhuru wa Tanganyika.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mdukuzi,Miaka hiyo mji mwisho magomeni wengi dini moja,weka na picha ya wapigania uhuru mkoa wa mbeya na iringa,uhuru haukupiganiwa kariakoo na gerezani pekee.huyo mzee haruna taratibu ni babu yangu aliyehamia dodoma,ntakuletea rafikize wa imani nyingine aliokuwa nao kwenye harakati,japo nae alikuwa mmanyema kama mimi ila sifagilii approach yako ya mukhtadha wa unachokiandika
Nawa...Mzee Mohammed Said namuheshimu kwa jitihada zake za ubobezi kwenye historia ya Uhuru wa Tanganyika.
Bond...Binafsi huwa nasoma sana makala za huyu Kaka yangu Ila kwa hili imebidi nitie neno, sioni sababu kwa nini majina yote ya kiislam na ndio anaona hao pekee wanafaa wapewe mitaa although sio tatizo sana but one may ask himself,. Why?????
Nilipofungua uzi nilitarajia kuona majina Kama ngamia, sukumawiki, Kibindoni, Mnana nk Ila akaona atuwekee majina ya waislam.
Naelewa kwamba hao ndio anaona walikuwa wapigania uhuru ambao kwa mtazamo wake wanesahaulika, lakini ni ngumu sana kuweka kila mtu aliyepigania uhuru maana kila mtu wazazi wake walipigania Uhuru maana waliutaka hakuna mwafrika ambaye hakutaka hata kama alikuwa kibaraka wa wakoloni.
Naangalia namna anavyojibu nimeona kama hajielewi sababu yeye anatoa history ya kila mmoja ya aliowataja, sisi hatuhitaji kuwaweka kwenye mitaa au basi angekuwa fair sababu kama ni wapigania uhuru aisee ni wengi mno asidhani babu yake pekee na hao wazee anaowajua yeye ndio walikuwa Frontline.
No wonder you have been taken to be a threat to national peace and unity tuliyonayo.
Your life is ending hebu ukiondoka duniani uache kazi nzuri ya historia Ila sio ya kuweka mtafaruku ambao kila siku unaambiwa na hujikagui au unafanya kwa makusudi.
Una heshima kwenye jamii Ila you are becoming incumbent and inconsiderate of the fact that tunaishi kwenye jamii ambayo wengine hawapendi haya majibizano yasiyo na faida yeyote hata wakiwekwa hawatafufuka.
Haya maandishi yako kuna siku yatatumika vibaya kuigawa hii jamii sijui huko uliko utajisikiaje na Mwenyezi Mungu atakupa adhabu gani.
Well, punguza unazi basi.Bond...
Ninachosema mimi ni kuwa tuwaenzi wapigania uhuru wa Tanganyika kwa kutunuku majina ya mitaa kwao kwa kuthamini mchango wao.
Ikiwa wewe mathalan unaona jina kama ''Ali Msham'' halifai unapendelea jina la mtaa liwe ''Kibindoni'' hilo ni wazo pia na wakazi wa eneo hilo wataamua jina lipi limebeba maana na kuhifadhi historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Si kuwa Mohamed Said kasema ndiyo itakuwa.
Mimi siyo niliyoweka majina ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mimi siye niliyemjaalia Abdulwahid Sykes kadi ya TANU No. 3 na mdogo wake Ally kadi No. 2, wala siye niliyekuwa naitisha mikutano ya siri usiku nyumbani kwake kuanzia mwaka wa 1950 kupanga mipango ya kuunda TANU.
Wala si mie niliyejaalia baba yao awe muasisi wa African Association 1929 chama kilichokuja kuzaa TANU wala si mimi niliyemshawishi yeye na Mzee in Sudi kuunda Al jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tangnayika) 1933;
Wala siye mimi niliyeunda Baraza la Wazee wa TANU ndani yake likiwa na wajumbe zaidi ya 120 wote Waislam na kumfanya Sheikh Suleiman Takadir kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo.
Hii ndiyo historia kama ilivyokuwa.
Wala si mimi niliyewazuia wengine na wao wasishiriki katika harakati hizi za kupigania uhuru kama waivyoshiriki wazee wangu.
Kama kunilaumu nilaumu kwa nini nimetafiti historia hii na kuandika kitabu?
Kuwa kuna wapigania uhuru wengi hawajulikani hili linawezekana sana na tuna wajibu wa kujua historia zao.
Sijajua nahatarisha amani vipi kwa kuandika historia ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Kitabu nilichoandika cha maisha ya Abdul Sykes ambacho yote mnayosoma hapa ndiyo chanzo chake kinakwenda chapisho la tano na kinauzwa madukani toka 1998.
Wala sijaskia watu wamepigana baada ya kusoma kitabu changu.
Ingekuwa hiki kitabu kinaleta chembelecho "mtafaruku," na kuhatarisha amani na umoja wa kitaifa kingepigwa marufuku miaka mingi.
Unajisemea mambo usiyoyajua.
Nahusika katika juhudi ya kuhifadhi historia ya Mwalimu Nyerere, TANU na uhuru wa Tanganyika takriban sasa mwaka wa 10.
Maktaba yangu ni kati ya maktaba bora tatu zenye taarifa nyingi kuhusu Baba wa Taifa na historia ya TANU na uhuru wa Tangnayika.
Maktaba hizi ni Maktaba ya Salim Ahmed Salim, Brig. General Hashim Mbita na ya Mohamed Said.
Umesema kweli maisha yangu yako ukingoni na wala sikusubiri wewe kunifamisha hili.
Mtume SAW ametuambia umma wake umri wao ni miaka 60 au 70.
Juma lijalo natimiza miaka 70.
Nini nitaacha?
Nitakachoacha ni hazina ya taarifa na historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo ilipotea kabisa.
Mimi nikaitafiti na kuiandika ije kusomwa na kizazi hiki na kijacho.
Historia hii haijagawa Tanzania nikiwa hai na haitagawika baada ya umauti wangu.
Huna sababu ya kujitisha mwenyewe na kuwatia wengine kwenye taharuki ya kufikirika.
View attachment 2124583
Picha ya hivi karibuni sana TBC walikuja nyumbani kufanya kipindi cha historia.
Bond...Well, punguza unazi basi.
I'll see into it., siku njema .Bond...
Mimi si mtu wa hivyo.
Fanya utafiti kidogo tufahamiane ujue wapi pa kuniweka.
Bond...I'll see into it., siku njema .
mim nafuatilia sana mada mzee nafurah sana kuwa nimeelimika na kufunguka macho baada ya kusoma historia hii za wazee.Bond...