SteveD,
Kuhusu koboko na king cobra nadhani ni nyoka wawili tofauti kwa sababu:
Koboko (japo sijawahi kumuona kwa macho)nafahamu anapatikana sana maeneo ya msitu ya miombo hususan kule Kigoma na Tabora.Habari zinaeleza kuwa ana ushungi kama wa jogoo!! Kama umesikia juu ya nyoka anayevizia watu kwa kujificha kwenye matawi ya miti na kuwadonoa wapitapo chini. Pale Bulombora JKT tulipata sana habari kama hizi. Na namna ya kumtega na kumuua ni kwa wanawake kubeba mitungi yenye uji wa moto na kupita eneo aliloko huyu koboko, ambapo atajitumbukiza kichwa kichwa kwenye uji wa moto!
Cobra kwa upande mwingine, habari zinaeleza kuwa anapatikana zaidi Asia, hususan India na ana umbile la mashavu(?) makubwa ambayo hujivimbisha anapoghadhabika.
Hebu tupate maoni ya wengine wajuao zaidi labda.
Ngao, Take 5!! Yaani umenikumbusha mbali sana... ni kama vile tumekua pamoja toka utotoni. Hizo tales kuhusu jinsi ya kuua koboko ni sawa sawa kabisa na zile nilizosimuliwa mimi. Yaani ni kubeba uji wa moto kwenye chungu na kata nzito, uji uliomzito sana... ili akijilengesha tu na kudonyoa kichwani anajikuta kazamisha kichwa chake chenye ('usunzu'- in sukuma au 'cock-crown' kwa waingereza nadhani) ushungi kwenye uji.
Ulivyo watofautisha king cobra na koboko, sasa nimeanza kuona na kukumbuka tofauti zao. Ahsante.
Ngao, je unajua jinsi ya kumuua kenge au buru kenge (mburu in sukuma)?!.. nitajijibu: kuchemsha mayai kisha kuyatia kwenye maji baridi haraka haraka na kuyatega kwenye njia yake... kiini chake kinakuwa bado cha moto pale atakapofakamia na kuyameza, maana huwa wanameza mazima mazima na kuyapasulia kwenye koo!! (lakini nakusihi ndugu, usiongelee mambo haya huko ma-ulaya kwenu, nasikia kuna watu kibao wa RSPCA!! natumaini unajua kasheshe zao.... lol)!
Ngao you are right kwa koboko si King Cobra ila ni Black mamba ambaye rangi yake si mweusi ila kijani hafifu ila ndani ya mdomo ndiyo mweusi.King cobra wapo wa Asia na wa Misri wote wana vimbisha mashavu.
Mwenekapufi, mbona na kumbuka kuwa koboko ana rangi ya kijivu au ni jamii nyingine hii?! Halafu characteristic yake nyingine ni mbio... nadhani kwa simulizi nilizopatiwa mimi, ana mbio kupita nyoka wote kule kanda ya ziwa.
By the way wanaJF, natoa mifano mingi kutoka kanda ya ziwa kwani huku ndiyo nimekaa na kuona viumbe wengi zaidi, haswa aina za nyoka.
Hivyo Tanzania wapo Cobra? Halafu yule ndege anaitwa Dudumizi analo jina la kiingereza?
Halafu kuna vile vindege vidogo hupenda kuruka kwa makundi (siyo mbayuwayu) yaani ni vidogo kweli sijui vinaitwaje, nimekuwa nikitafuta jina lake kwa muda mrefu sasa.
Mkjj, hapa umenikumbusha ndege mmoja kule mwanza tulikuwa tuna mwita 'dodorima/dodolima'... this one I have seen it na nawajua kabisaa, wana rangi nyingi kama kasuku, ambao jina lao generic nadhani ni macaws (off course wapo species mbali mbali wa hawa). Hawa dodorima they are simply beautiful... lakini ni mbumbumbu kweli kweli... (no offence, lakini ni sawa na zile jokes za blondes, if you know what i mean!), hawa dodorima, hawana akili, kazi yao kusinzia tuuu... siongopi, yaani unaweza ukamkamata kwa mikono bila hata kuhangaika kumfukuza... kuna wimbo mmoja wa utotoni naukumbuka ulikuwa unaenda hivi:
#...dodorima sinzia
#...dodorima sinzia
#...mama yake....(sijui nini kilikuwa kinafata hapa, it's long time, can't remember)
Nikirudi kwa huyo dudumizi, nadhani amepewa jina hilo kutokana na kutoa sauti yake hiyo... yaani : duuduu... duudu-duuduu x2 !! Nikitaka kuwa describe kwa maisha ya kanda ya ziwa, ni kuwa, hawa wanapenda sana kuishi kwenye miti ya miembe... huwaoni, bali unasikia sauti yao tu hiyo wakiimba....hivyo jina ndiyo maana wanaitwa dudumizi. (naweza kuwa na describe ndege tofauti kabisa hapa, mtanisamehe). Na kwa nyongeza ni kuwa, hawa wanao kaa kwenye miembe, wanafanana sana na njiwa pori.
Mkjj, hao ndege wanao ruka kwenye makundi.. ni wale wenye speed kali sana kama vipanga, yaani wana madoido mengi utafikiri jet fighters... au hawa ndiyo mbayuwayu.. I'm confused, sijui yupi ni yupi..
Nadhani Cobra kwa Kiswahili anaitwa KIFUTU
Nadhani Tanzania wapo Cobra. Nakumbuka nimeshawahi kumuona mtoto wa Cobra miaka mingi iliyopita. Labda macho yangu yawe yalindanganya akuwamdgo sana.
Kuna ndege wadogo warukao kwa makundi. Wana kelele sana, na vidari vyao ni vya njano. Wanaitwa USIGI. Sijui km ni hao uwazungumziao.
T-1!
Za siku ndugu?!... hapa sina hakika kwa kweli, inawezekana you are right, lakini nadhani kifutu ni tofauti... kifutu kwa jinsi ninavyojua mimi ana rangi nyingi nyingi (kama za chatu hivi), na ni mfupi sana ila mnene. Sumu yake kwa wenye bahati mbaya ya kung'atwa naye nikuwa ina ozesha miguu au kiungo. Kwa hisia zangu mimi nafikiri kifutu ni rattle snake kama wale wa kule America. Kifutu hana hasira kama cobra.
Cobra ni mweusi na kule kanda ya ziwa tuna mwita Swila. Nadhani ulishawahi sikia hili. Na kama nilivyosema mwanzoni kabisa nadhani hili jina linaweza kunyambulishwa na kuwa neno la kiswahili. Jina swila linatokana na kutema mate, kama unavyojua, cobra are notorious kwa kutema mate, hence jina swila.
-----
Mkjj, Eeeh, kuna stori moja nikupe, unajua hawa kasuku wanaoimba nyimbo na kutamka maneno wanakamatika sana (off course wamepungua siku hizi) maeneo ya kanda za ziwa.... nakumbuka nikiwa mtoto, kuna jamaa kutoka Dar, ilikuwa ukifika tu msimu wa kuivisha na kuvuna mtama (nadhani inaitwa sogharm kwa kiingereza) na uwele (huu nao sijui ni jamii ya ulezi - i don't know!), walikuwa wanazingira vijiji kibao kwenye mashamba ya mazao haya. Walikuwa wanatumia ulimbo (watu wa dar na mijini kwingineko wanaweza wasijue haya -just ask me nyie watoto wa mijini... will describe the variety of this stuff.. lol), huo ulimbo ulikuwa unapakwa kwenye miti kibao kandokando ya mashamba hayo, maana ndege hutua kwenye miti hiyo kabla ya ku-swarm ndani ya shamba na kuanza kuteketeza nafaka... in a way, jamaa walikuwa wanasaidia wana kijiji, so to say, but nilibahatika kwenda dar na wakati fulani kwenda huko ulaya, ndiyo nilipoona hali halisi, yaani, kwanini jamaa walikuwa wanakamata ndege hao... they are dead expensive pets!! kumbe jamaa walikuwa wanakamata matenga na matenga ili kupeleka kuuza huko ulaya... duuh, i wish i knew this, nami ningelikuwa ka millionea fulani hivi labda hivi sasa... lol!
SteveD.