Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ndiyo kuna senene, panzi, halafu wale wanaoliwa wako kama mchwa wanaitwaje, hasa kule kwenye "bomba hii, nyumba hii" wana mafuta hao!!
anaitwa TONDOFWA
Dragonfly wanaitwa 'Kereng'ende' kwa kiswahili
Jioni njema.
Ni siku za karibuni tu nimebahatika kufahamu kuwa matopetope yanajulikana kama custard apple, jina lake la kisayansi silijui.
Napenda kuulizia majina ya: mastafeli na Mafenesi. Jina la kiingereza au kilatini. Ahsanteni.
Katika pitapita yangu kwenye mtandao (nadhani kwa michuzi - sina hakika) nilikutana na kitu ambacho sijawahi kufiri kinaliwa.
Kuna 'maua' ya migomba (ambayo hutoa ndizi), kwamba yanauzwa (Ulaya?) na kutumika kama chakula .
Hivi yanaitwaje (Kiswahili) na yanatumikaje kwa msosi (sababu kwetu sisi yale ni chakula cha ng'ombe/mbuzi)?
![]()
By the way WanaJF, hivi mizaituni kama inavyopatikana kule Mashariki ya Kati inaitwa nini katika Kiingereza, na scientific name yake ni nini?! Natanguliza shukrani.
MAFENESI,ni JACKFRUIT.jamani je zambarau kwa kingereza zinaitwaje?
Olive tree
Olive tree
Wakuu, na "sharon fruit" linaitwa nini kwa Kiswahili au jina lake la Kilatini?!
Huwa nasilia watoto wengi wakimwita "kombamwiko" huyo praying mantis. Sina hakika kama ni kiswahili fasihi au msimu tu.
Arusha yanapikwa kabisa.Katika pitapita yangu kwenye mtandao (nadhani kwa michuzi - sina hakika) nilikutana na kitu ambacho sijawahi kufiri kinaliwa.
Kuna 'maua' ya migomba (ambayo hutoa ndizi), kwamba yanauzwa (Ulaya?) na kutumika kama chakula .
Hivi yanaitwaje (Kiswahili) na yanatumikaje kwa msosi (sababu kwetu sisi yale ni chakula cha ng'ombe/mbuzi)?
![]()