George Magere Massatu,bonge la center half wa miaka hiyo
Mkuu Dominick Chilambo R.I.P nadhani alikuwa ameshafariki enzi za kina Lubigisa Madata Lubigisa
Sidhani ila wanaokumbuka zaidi wanaweza kutujuza manake nakumbuka huyu alikuwa kipa wa pamba ya mwanza enzi hizo....Yawezekana unamchanganya na Lubigisa Lubigisa....
Huyu Abdalah Bori,anafanya kazi kwenye kampuni moja kwa sasa ambapo niko nae karibu sana aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa mcheza mpira nikamkatalia kabisa, nimeona anatajwa hapa, kumbe ni kweli. Maana yawezekana enzi hizo nilikuwa mtoto.
mongella ..............................
Nakumbuka sana best nilikuwa never miss....nilikuwa ball boy (naokota mipira na kurudisha uwanjani pale ushirika) nikiwa shule ya msingi. Ushirika walikuwa na kocha mmoja Dan Koroso alifundisha soka maridadi sana enzi za kina Bahatisha ndulute, Ofen Martin, Stephen Nyenge, Waziri Ally, Kaunda Mwakiptope, Venance Motto...dah kumbukumbu zinaanza kupotea. Nakumbuka katika msimu mzima wa ligi ni Yanga tu iliweza kuifunga ushirika goli moja, goli lililofungwa na Abeid Mziba kwa kichwa. Timu zote ama ziliambulia sare au ziliondoka na kichapo.
Mimi wachezaji majina yao hayanikoshi kama inavyonikosha timu ya LIBOLO.....simba wanaijua shughuli ya libolo
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Halafu ilikuwa mpaka nje ya nchi. Kwa mfano soma haya majina ya wachezaji wa nchi na ligi nyingine duniani kwa lugha ya Kiingereza. Kuna wakati mpaka watangazaji waliokuwa wanaona kuyataja wanauchuna tuu
Kwa msaada wa: The Top 11 Filthiest Football Player Names Ever - FTBpro na Funny Football Player Names | Soccerlens
- David Seaman
- Nick Butt
- Argelico F.u.c.k.s
- Stephan Kuntuz
- Andre Muff
- Ralf Minge
- Paul Dickov
- David Goodwillie
- Danny Shittu
- Johan de Cock
- Fabian Assman
- Daniel Drinkwater
- Creedance Clearwater Couto
- Boy Waterman
- Steve Kums
- Shiteus Bramble
- Francisco Arce
- Ars Bandeet
- Segar Bastard
- Milan Fukal
- Bongo Christ
- Wolfgang Wolf
- Peter Pandel
- Rafael Scheidt
- Rod Fanni
- Johnny Moustache
- Quim
- Brian Pinas
- Bernt Haas
- Uwe Fuchs
- Norman Conquest
- Danger Fourpence
- Harry Daft
- Ruud Boffin
- Mark De Man
mweeh!!!Best umenikumbusha tena michezo ya majeshi pale CCP kuanzia soka, basket, netball, kutupa tufe na vikoro koro kibao mikoa yoote it was a full shangwe kwa mwezi mzima kuona manjagu wakipambana aisee....nilikuwa nikitoka shule hadi giza linaingia niko pale...halafu ukirudi home kichapo....
Halafu kumbe ulikaa RAU? Nilikuwa nafika sana pande hizo kuna kinyozi mmoja maarufu sana aliitwa Abunuwasi alikuwa akinyolea chini ya mti hapo RAU....yaani nilikuwa natembea karibu KM 4 kumfuata aisee...
Mida hiyo pia kulikuwa na timu za soka za mashirika ya umma zilikuwa nzuri usipime...mf. Coffe FC, TPC nk halafu kulikuwa pia na Machava FC nimeisikia juzi ndhani imefufuliwa tena.
But all in all Mkuu gfsonwin naona hii trend ya kufa kwa hivi vilabu ni mikoa yote tukianzia na Mwanza Pamba kwishney, Kagera kulikuwa na RTC Kagera ikiwa na mpishi wa mabao aliyeitwa Kasiga Machapati, Pia Tanga Cost ya kina Mgunda na Razack Yusuph ilikuwa tishio bila kuwasahau African Sports ya kina Victor Mkanwa, Mororgoro kukawa na Reli iliyokuwa ikishuka na kupanda daraja kila mwaka ikiwa na wakali kina Dkt Madundo mtambo, then wakaja kina Mbuyu Yondan (Nadhani ni baba yake Kelvin kuna mdau amegusia kw post mojawapo), Mbeya kukawa na Tukuyu Stars ya kina Justine Mtekere na Godwin Aswile (actually Yanga walikuwa wameifanya chuo chao cha mafunzo kwa kuvuna wachezaji wazuri), Songea usipime kukawa na Majimaji ya kina Madaraka Selemani "Mzee wa kiminyio" ambaye alikuwa akiitesa Yanga kama anavyotaka hadi alipokuja Simba. Walikuwepo pia kina Mrope Stephen Nemes nk..Dar kina Plisner enzi za Iddi Pazi na Andrew Godwin, Nyota Nyekundu enzi za kina Omary Mghalike (Mzee wa Offside), Costa Ndunguru...(alikuwa akicheza rafu mbaya!), Idrissa Ngulungu, bila kuisahau RTC Kigoma enzi za kina Sanif Lazaro...dah orodha ni ndefu na muajiri naye ananidai ....
Nimegoogle kwa ajil yenu, ondoeni shakaMkuu, kuna Mtaliano mmoja alikuwa ni bingwa wa kuteleza juu ya theluji (skiing) miaka ya 1990. Jina lake la kwanza ni Alberto T.o.m.b.a.
Mkuu, kuna Mtaliano mmoja alikuwa ni bingwa wa kuteleza juu ya theluji (skiing) miaka ya 1990. Jina lake la kwanza ni Alberto. La pili ni neno la Kiswahili ambalo huwezi kuandika humu. Hebu google maneno haya alberto skiing au alberto skier na utaelewa nina maana gani. Vyombo vyetu vya habari vya Bongo vingekuwa na wakati mgumu sana kama bwana huyu angekuwa, kwa mfano, ni mchezaji wa kiwango cha juu Manchester United, Barcelona au klabu nyingine maarufu Ulaya.