Salaam,
Wakati mwingine Jina ni zaidi ya tuchukuliavyo, yaani jina ni zaidi ya pesa, madaraka wakati fulani.
Nchini kwetu(Tanzania), mara nyingi imekuwa kawaida kwa waigizaji maarufu, wacheza filamu kufahamika kwa majina ya uigizaji wao na sio majina halisi mfano "Ray" ambaye jina lake halisi ni Vincent Kigosi, na wengine wengi, tofauti hasa na nchi zingine(hata nchi zilizo bora zaidi katika sanaa hii).
Wakati fulani ni ngumu kumtambua mtu katika hali fulani, hata kama ulikuwa unamfahamu kwa sababu tu jina lake halisi " SI JINA LAKE", Shida ni nini hasa, Ni waigizaji kupenda majina hayo au watazamaji na washabiki kutohitaji kuwafahamu waigizaji kwa majina halisi?