Majina ya Waigizaji/Wacheza filamu.

Majina ya Waigizaji/Wacheza filamu.

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2012
Posts
3,598
Reaction score
1,544
Salaam,

Wakati mwingine Jina ni zaidi ya tuchukuliavyo, yaani jina ni zaidi ya pesa, madaraka wakati fulani.

Nchini kwetu(Tanzania), mara nyingi imekuwa kawaida kwa waigizaji maarufu, wacheza filamu kufahamika kwa majina ya uigizaji wao na sio majina halisi mfano "Ray" ambaye jina lake halisi ni Vincent Kigosi, na wengine wengi, tofauti hasa na nchi zingine(hata nchi zilizo bora zaidi katika sanaa hii).

Wakati fulani ni ngumu kumtambua mtu katika hali fulani, hata kama ulikuwa unamfahamu kwa sababu tu jina lake halisi " SI JINA LAKE", Shida ni nini hasa, Ni waigizaji kupenda majina hayo au watazamaji na washabiki kutohitaji kuwafahamu waigizaji kwa majina halisi?
 
Huwa namfurahia Irene uwoya, na wengineo waliojitahidi kukuza majina yao halisi
 
Huwa namfurahia Irene uwoya, na wengineo waliojitahidi kukuza majina yao halisi

Ni kweli mkuu, kwa baadhi ya wasanii hutumia majina yao halisi, hii husaidia hata kukuza vipaji vyao kwa nchi jirani...lakini ni ngumu sana kwa baadhi kutokana na kutojulikana kwa majina yao halisi!
 
Wema sepetu
hemed suleiman
jacklin wolper
yusuph mlela
steven kanumba*
riyama ally
 
ata wasanii wengi uwa wanatumia a.k.a ni kawaida,hivo wanaotumia jina halisi na wasiotumia yote ni sawa,cha muhimu kazi anayofanya inakubalika na anatoa mambo mazuri kwa mashabiki
 
Haya ni majina yanayotumiwa sana na Mashabiki hivyo wanajikuta wanayakubali kutokana na kuwa na umaharufu zaidi sio Bongo tu hata nchi zingine wasanii maarufu kama Mr Bean, Bushman au Salafina mjins hayo ni maarufu zaidi ya majina halisi.
 
Sure. Usisahau haya pia.
  1. Rambo - Sylvester Stallone
  2. Ibu - John Okafor (mchekeshaji maarufu wa Nigeria)
  3. Aki - Osita Iheme
  4. Ukwa - Chinedu Ikedieze (wale Wanigeria waigizaji wafupi sana)
  5. Cheni - Mahsen Awadh
  6. Mhogomchungu - Abdalla Mkumbila .....nk
 
Hehehe! Mzee Majuto, mzee small, mzee kipara, pwagu na pwaguzi, haya majina hata kama ndio mastaa wa bongo that's why yanaishia hukuhuku kipunguni mtaro.

Wanataka kujifananisha na Rowan Atkinson a.k.a Mr. BEAN.
 
Sure. Usisahau haya pia.
  1. Rambo - Sylvester Stallone
  2. Ibu - John Okafor (mchekeshaji maarufu wa Nigeria)
  3. Aki - Osita Iheme
  4. Ukwa - Chinedu Ikedieze (wale Wanigeria waigizaji wafupi sana)
  5. Cheni - Mahsen Awadh
  6. Mhogomchungu - Abdalla Mkumbila .....nk

Ni kweli mkuu, lakini mara kadhaa katika maonyesho, sherehe badala ya mtu kuitwa kwa jina lake anaitwa kwa jina la usanii..mf. Tumia jina la Rambo USA kama kuna watu watakuelewa lakini ukiongelea Sylvester S, utaeleweka na unafahamika kusaidiwa vizuri.
 
Back
Top Bottom