Elisha Sarikiel
JF-Expert Member
- Aug 29, 2020
- 905
- 1,540
MAJINA YA WAJUMBE WALIOCHAGULIWA KULIWAKILISHA BUNGE KWENYE TAASISI MBALIMBALI
(A). TUME YA UTUMISHI WA BUNGE
Wajumbe wanne wanaingia kwa mujibu wa nafasi zao ambao ni Spika (Mwenyekiti wa Tume), Naibu Spika (Makamu Mwenyekiti wa Tume), Waziri anayeshughulikia masuala ya Bunge na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya walio wachache Bungeni. Hivyo basi, nafasi ambazo zitatakiwa kujazwa ni za Wajumbe saba; Chama Tawala nafasi 5 na walio wachache nafasi 2 kwa kuzingatia jinsia. Ili kujaza nafasi hizo majina yafutayo yamependekezwa na kupitishwa na Bunge;
Mhe. Aeshi Khalifan Hillal
Mhe. Rashid Abdallah shangazi
Mhe. Janejelly James Ntate
Mhe. Zahor Mohammed Haji.
Mhe. Fakharia Shomar Khamis
Mhe. Halima James Mdee
Mhe. Khalifa Mohamed Issa
(B) BUNGE LA AFRIKA (PAP)
Ili kujaza nafasi zilizopo majina yafutayo yamependekezwa na kupitishwa na Bunge;
Mhe. Ng’wasi Damas Kamani
Mhe. Toufiq Salim Turky
Mhe. Jerry William Slaa
Mhe. Nape Moses Nnauye
Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest
(C) JUKWAA LA WABUNGE WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC PF)
Katika Jukwaa hili, Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake katika Bunge la Nchi husika anakuwa ni Mjumbe kwa nafasi yake ambaye ni Mhe. Shally Josepha Raymond. Ili kujaza nafasi nyingine nne zilizopo majina yafutayo yamependekezwa na kupitishwa na Bunge;
Mhe. Kassim Hassan Haji
Mhe. Selemani Jumanne Zedi
Mhe. Dkt. Alfred James Kimea
Mhe. Hawa Subira Mwaifunga
(D) UMOJA WA MABUNGE DUNIANI (IPU)
Ili kujaza nafasi zilizopo majina yafutayo yamependekezwa na kupitishwa na Bunge;
Mhe. Eng. Mwanaisha Ng’azi Ulenge
Mhe. Ramadhani Selemani Ramadhani
Mhe. Joseph Kizito Mhagama
Mhe. Elibariki Immanuel Kingu
Mhe. Esther Nicholas Matiko
(E) UMOJA WA MAZIWA MAKUU (Great Lakes)
Ili kujaza nafasi zilizopo majina yafutayo yamependekezwa na kupitishwa na Bunge;
Mhe. Dkt. Christine Gabriel Ishengoma
Mhe. Najma Murtaza Giga
Mhe. Eng. Ezra John Chiwelesa
Mhe. Deus Clement Sangu
Mhe. Shamsia Aziz Mtamba
