Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Uzungu upi sasa? Watanzania bana, yaani mtu akijua tu kuongea kiingereza, ndio tayari amekuwa mzungu? Watanzania si ndio mnaongoza kwa kuukumbatia huo 'uzungu'? Sio kwa yale majina yenu ya ajabu ajabu, utasikia eti JoanFaith John Kataria, mara sijui Jane John, Andrew Peter, n.k, na hao ni watanzania weusi tititi, ni zaidi ya aibu.
Sijui kwanini watanzania ambao hawajafika Kenya huwa wanadhani kwamba wakenya wanaongea kiingereza 24/7, kutoka che hadi machweo. Kiswahili ndio lugha ya mawasiliano nchini Kenya kwa asilimia kubwa. Ila wakenya tangia jadi huwa wanajivunia sana mila na tamaduni wao.
Wakenya wanathamini lugha zao za asili kwanza, kabla ya lugha yeyote nyingine. Kiswahili, kiingereza au hata kifaransa zote hizo kwetu ni lugha za kigeni. Tukisema hivyo huwa mnaishia kusema kwamba huo ni ukabila. Majirani mlipangwa ndani ya mfumo wa lugha moja hadi mkapangika kupindukia. Mwacha mila ni mtumwa, walisema wazee wa Ndemi na Mathathi
Mkishakuwa nchi moja yenye makabila tofauti na kila kabila likawa too proud na utamaduni wake basi lazima kutakuwa na migawanyiko ambayo huzua chuki na vurugu ambazo wanasiasa na hata mataifa ya kigeni huzitumia kwa faida yao,
Kuondoa hali hiyo inabidi kujenga tu nchi yenye utamaduni mmoja ikiwemo lugha moja
Kiswahili kinaongelewa na wananchi karibu wote na pia kina maneno mengi yenye asili ya makabila ya Kenya, Congo, Tanzania n.k so sio mbaya ikachukuliwa kama lugha ya asili kuliko ya kigeni.
Ingekuwa jambo zuri kama ukanda wa Afrika mashariki na kati tungekuwa na lugha moja iliyoundwa kutoka lugha za makabila ya nchi zetu, bahati mbaya kila mtu yupo too proud