Majina ya watia nia yanaweza kukatwa kwa kutuhumiwa Rushwa ndani ya CCM mkoani Simiyu

Majina ya watia nia yanaweza kukatwa kwa kutuhumiwa Rushwa ndani ya CCM mkoani Simiyu

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Watia nia wa nafasi za ubunge na udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Simiyu huenda wakakosa kurejeshewa majina yao kwenye mchakato wa kuteuliwa, kufuatia tuhuma za matumizi ya fedha kwa ajili ya kushawishi wajumbe na kufanya mikutano isiyo rasmi na madalali wa kisiasa.

Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa baadhi ya wagombea walihusishwa na vitendo vya kugawa fedha kwa wajumbe, kuendesha vikao vya kificho, na kushirikiana na makundi ya wafitini ili kujipatia uungwaji mkono kisiasa.

"Vyombo vya ulinzi na usalama vya ndani na nje ya chama vilikuwa kazini wakati wote wa mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu. Tayari ripoti zao zimewasilishwa Makao Makuu ya chama," kilisema chanzo chetu cha ndani kwa sharti la kutotajwa jina.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, hatua kali huenda zikachukuliwa dhidi ya wagombea waliobainika kukiuka maadili ya uchaguzi wa ndani ya chama, ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa majina yao kabla ya hatua ya uteuzi rasmi.

"Msishangae kuona sura mpya kabisa zikichukua nafasi ya wale waliokuwa wakipigiwa debe. Chama kimejipanga kusafisha mchakato na kuhakikisha haki, usawa na nidhamu vinatawala," chanzo kingine kilieleza.

Hatua hiyo inaonekana kuwa ni sehemu ya juhudi za CCM kujisafisha dhidi ya vitendo vya rushwa na ushawishi haramu, ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa na wanachama na wananchi kwa muda mrefu, hasa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Hadi kufikia sasa, maelfu ya wanachama wa CCM nchini kote wamechukua fomu kuomba uteuzi wa kugombea nafasi za ubunge na udiwani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
 
Angela Kairuki anatoa rushwa kama hana akili vizuri hapo KIBAMBA
Kila mjumbe anakula 70000/=
anafanya hivyo wazi wazi kabisaa mchana kweupe
 
Back
Top Bottom