Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Ukifanya utafiti utagundua siku hizi watu wengi hawawapi watoto wao majina ya Kiasili kama vile ya kikabila au ya kiswahili.
Siku hizi majina mengi yanabaki kuwa ya kizungu kwa wakristo au ya kiarabu kwa waislamu.
Zama za kale watu walipewa majina kulingana na vitu mbalimbali au matukio mbalimbali, ambayo kwa hivi sasa watu wengi kwao yamebaki kama majina ya ukoo tu, ila jina la kwanza linakuwa la kiarabu au kizungu.
Hii ni hali ya hatari kwa majina yetu ya asili au kiswahili. Familia muangalie sana kuepuka kuwapa watoto wenu majina ya kimagharibi au kiarabu, badala ya jina la kiswahili au kikabila.
Unakuta mtu anamwita mtoto wake "Hope" badala ya "Tumaini", au "Jamal" badala ya "Tumaini"... Sasa unakuta mtu anakimbilia kumuita jina la kiarabu au kizungu ambalo linamaana sawa na jina la ambalo lipo kwenye kabila analotoka au lipo kwenye kiswahili, mpaka unajiuliza kwa nini hasingemuita tu lile la kikabila au kiswahili.
Siwapangii majina ya kuwaita watoti wenu, ila tupende vyetu