Malaika wa Waha
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 319
- 885
Mi mwanangu namuita "Sangwa Ngungwa ngando"
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona yapo majina ya kiswahili au ya kilugha yenye maana nzuri... Furaha, neema, rehema, Akili, Fikiri, na majina yote mazuri ya kiswahili, au ya kilughaMimi naangalia maana ya jina na siyo mambo sijui ya asili na upuuzi mwingine.
Siwezi waita watoto wangu (Shida, Masumbuko, Tabu) ety kwa sababu ya asili au lugha ya Kiswahili inanitaka kufanya hivyo,, ni ukichaa huo 😎🤏
Mfano, NDIKUSIKULIKUJO😀Huku kwetu majina ya kiasili yalikuwa hayaandikiki, ilibidi walimu wawarudishe wanafunzi nyumbani waje na majina ya kanisani/msikitini.
Kwenye kabila langu hakuna neno Tumaini. Je tupende vyetu kama kabila au tupende vyetu kama nchi au tupende vyetu kama bara au labda tuoende vyetu kama dunia?Ukifanya utafiti utagundua siku hizi watu wengi hawawapi watoto wao majina ya Kiasili kama vile ya kikabila au ya kiswahili.
Siku hizi majina mengi yanabaki kuwa ya kizungu kwa wakristo au ya kiarabu kwa waislamu.
Zama za kale watu walipewa majina kulingana na vitu mbalimbali au matukio mbalimbali, ambayo kwa hivi sasa watu wengi kwao yamebaki kama majina ya ukoo tu, ila jina la kwanza linakuwa la kiarabu au kizungu.
Hii ni hali ya hatari kwa majina yetu ya asili au kiswahili. Familia muangalie sana kuepuka kuwapa watoto wenu majina ya kimagharibi au kiarabu, badala ya jina la kiswahili au kikabila.
Unakuta mtu anamwita mtoto wake "Hope" badala ya "Tumaini", au "Jamal" badala ya "Tumaini"... Sasa unakuta mtu anakimbilia kumuita jina la kiarabu au kizungu ambalo linamaana sawa na jina la ambalo lipo kwenye kabila analotoka au lipo kwenye kiswahili, mpaka unajiuliza kwa nini hasingemuita tu lile la kikabila au kiswahili.
Siwapangii majina ya kuwaita watoti wenu, ila tupende vyetu