Majina ya watu ya Asili kama vile ya kikabila na ya kiswahili uenda yakatoweka

Mimi naangalia maana ya jina na siyo mambo sijui ya asili na upuuzi mwingine.

Siwezi waita watoto wangu (Shida, Masumbuko, Tabu) ety kwa sababu ya asili au lugha ya Kiswahili inanitaka kufanya hivyo,, ni ukichaa huo 😎🤏
Mbona yapo majina ya kiswahili au ya kilugha yenye maana nzuri... Furaha, neema, rehema, Akili, Fikiri, na majina yote mazuri ya kiswahili, au ya kilugha

Wewe majina ya kiswahili umeona tu Shida, Masumbuko, Tabu... Au ndio ufinyu wa kufikiri, mtoto unaenda kumuita Happiness, je ungemuita Furaha ungekosa nini
 
Sidhani kama hiyo zama za kale ulikuwepo.
 
Kwenye kabila langu hakuna neno Tumaini. Je tupende vyetu kama kabila au tupende vyetu kama nchi au tupende vyetu kama bara au labda tuoende vyetu kama dunia?
Kuna watu ukisema vyetu watanaanisha vya Kizungu au vya Kiarabu kulingana na imani zao, je wapi mtu anaona ndiyo nyumbani. Dini au kabila?
All in all jina ni jina tu, mimi huwa nawapa watoto wangu majina kwa sababu zangu binafsi.
 
Usipangie watu mkuu, ita wa kwako inatosha
Kuna sehemu nimesema napangia watu, au wewe nimekupangai?

Jua kuelewa utofauti wa mtu kutoa mtazamo wa maoni na mtu kumpangia mtu mwingine
 
Ulimbukeni ni tatizo kubwa kwa jamii ya waafrika. Nina watoto 4 majina yao ni
1. Baraka
2. Upendo
3. Maseko ( Mavuno)
4. Kisaka ( Dunia)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…