Majirani mna cha kujifunza kutoka kwa Wakenya, Uhuru, Ruto na Raila washirikiana kwenye kukagua bandari mpya

Hatua Nzuri Sana
Inatia Moyo Sana Kuona Viongozi Wapo Pamoja
 

Tokea vyama vingi viruhusiwe huo ukosoaji wa kijinga ndiyo ukaanza. Angalia hata mada za kabla ya JPM kuingia madarakani kama hazikuwa za manung'uniko.
Halafu hata kwenye social media zenu kuna walalamishi kama ilivyo humu, hamna jipya. Vyama vingi ni saratani inayotafuna umoja wa Waafrika.
 
Jamaa anajikuta mwana ushauri kwa watu wakati kwake hapafai [emoji23][emoji23][emoji23]
 

Social media zetu kwa sasa zina wakosoaji panapostahiki, maana wamepewa uhuru wa kidemokrasia, watu wanakosoa na wengine kushauri, ila ukisoma kila wanachokisema kina mantiki ya kiaina. Ukilinganisha na hapo awali ambapo viongozi wetu walikua wanalumbana, watu walikua na hasira na waliponda kila kitu iwe kizuri au kibaya, hawakutaka kujua wala nini.
Ukwaminya watu tegemea hilo, lakini la kukosoa kwa nia njema ni jambo nzuri sana, ni vizuri watu wapige makelele ya mwizi ufisadi ukitajwa, ni vizuri watu wakosoe pale serikali inaibuka na mikakati ya ovyoo, na lipo kwetu hata leo hii, kuna wakati rais Uhuru anazingua kishenzi, lakini ile ametupatia sote uhuru wa kusema, tunalipigia makelele linatutoka moyoni.
 

Miradi mnayoisifia humu kama SGR ukisoma social media zenu wapondaji wapo wengi tu. Kuna wakosoaji wa kudumu ambao hata ufanyaje hawawezi kuridhika.
 
ila BABAA alichomfanyia miguna miguna ni UNAFIKI wa waziwazi yaani swahiba wako katolewa nchini mwake kinguvu we una gonga cheers tu
 
ila BABAA alichomfanyia miguna miguna ni UNAFIKI wa waziwazi yaani swahiba wako katolewa nchini mwake kinguvu we una gonga cheers tu

Miguna kiburi chake kilimponza maana yeye alibomoa madaraja yote ikiwemo baina yake na Raila.
Soma kitabu chochote cha kisiasa, utaelewa kwanini haufai kubomoa madaraja ila kujenga uelewano na kila aliyekuzunguka.
Huyo Miguna alijua ana kasoro ya kisheria baada ya kuukana uraia wake na kupokea wa Kanada kipindi kile katiba yetu haikua inaruhusu uraia pacha.
Aliporudi badala ya kuiweka sawa, akazembea kisa alikingiwa kifua na waziri wa wakati ule, sasa akaendelea kufanya madudu dhidi ya serikali, kawaida system yoyote ile huwa na taarifa zako zote na husubiri tu mud muafaka wa kuzitumia. Ndio kama mnachofanya kwa akina Makamba na Membe.
 
Unachangia kwa kuonyesha busara na hekima kubwa sana kuliko hao wanaokujibu majibu ya kipuuzi yenye kuendeleza chuki za kutisha miongoni mwa Watanzania hadi kufikia Serikali kuuwa watu wake wasiokuwa na hatia yoyote bali kutumia uhuru na haki yao ya kikatiba kuikosoa Serikali au kuandika magazetini ukweli wa yale yanayojiri nchini.

Ahsante sana Mkuu πŸ™πŸ½πŸ‘πŸ½

 
umewataja wa na siasa wa Tz hapo mwishoni ktk maoni yako...sifahamu kama waelewa siasa za tz ww ? kenya najua unafahamu kuna siasa za ukabila pia....VP na genge lake wana roaming around the country to seek for what ?
 
umewataja wa na siasa wa Tz hapo mwishoni ktk maoni yako...sifahamu kama waelewa siasa za tz ww ? kenya najua unafahamu kuna siasa za ukabila pia....VP na genge lake wana roaming around the country to seek for what ?

Siasa za kwenu nazifahamu fika, kwanza mna uchama uliokubuhu, unakuta taifa lote kila mtu hata wasomi wote mumegawanyika kwenye misingi ya vyama, msomi mzima hatumii ubongo wala akili anapojadili hoja, anasklizia kwanza wapi msimamo wa chama.
Uchama unafuatwa na ushirikina, udini, ukanda na chembe chembe za ukabila haswa kwa Wasukuma kwenye siasa za awamu ya tano asilimia yao kubwa wanaimba mapambio ya misifa. Na jinsi wengi huwa mumeapa hamuwezi kumpa Mchagga atawale nchi.

Ruto kuzunguka nchi sio issue maana ni Mkenya na naibu wa rais, hivyo anayo haki ya kuzunguka taifa lote hadi kwenye mashinani kuhakikisha kazi zinafanyika, mbona huulizi hilo swali wakati rais wenu nimekua nasoma anazunguka kote akihutubia halaiki ya watu na hata kutaja mambo ya chama huko huko ilhali wapinzani mumewakandamiza hawaruhusiwi kukusanyika hata watano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…