Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa siasa huwa hamna urafiki wa kweli au uadui wa kudumu, ndio ukweli mchungu, Uhuru na Ruto sio marafiki ila wapo pamoja kwa maslah yao ya kisiasa na kila mmoja anamtegemea mwenzie, ukiwa mwanasiasa lazima ujue jinsi kushirikiana na kila mmoja, ukipata fursa nenda ukatazame series za Games of thrones, utajifunza kitu.
Uhuru ameicheza vizuri sana kwa kuhakikisha Raila hakai mbali naye, maana kuongoza nchi huku nusu ya taifa ni full minung'uno hata ujenge madaraja, reli na barabara ngapi ni kazi bure. Leo hii hapa Kenya tupo kimoja, uzinduzi wowote ule unapokelewa kizalendo na kila mmoja, awe kwenye mlengo wa serikali au upinzani lakini kila mmoja anafurahia chochote kizuri na kukosoa panapostahiki, maana viongozi wetu wamewekanaa sawa kwa maslahi mapana ya taifa.
Hebu wewe jabribu kwenda kwenye JF kule kwa hoja mchanganyiko au jukwaa la siasa, anzisha uzi wowote wa jambo nzuri lolote analolifanya Magufuli, iwe uzinduzi wa Stigeler, terminal 3 au chochote hazitapita dakika kumi uzi unachezea kurasa kadhaa watu wanakosoa hawataki.
Ndivyo ilikua Kenya, lakini kwa Uhuru kuwekana sawa na upinzani na kuwapa uhuru wa kusema, wakaanza kupokea mazuri ya nchi kizaendo. Tanzania ya leo ina Watanzania wanaosheherekea timu ya taifa kufungwa mabao, wap umeona hilo dunia hii. Mtaongea kibabe na kuwatukana wapinzani, mtawazima na kuwafunga lakini ndio ukweli huo, mnaharibu na hamtaki kuskia, waacheni muwape nafasi wapige makelele, wakusanyike, wafanye mikutano yao, mwisho wa siku Watanzania watachagua nani wa kumskliza. Kama kuna lolote nzuri mnafanya, wenyewe wataliona bila kulazimishwa.
Lakini hili ya CCM mnazunguka nchi mkihutubia mikutano, yaani kampeni za 2020 mlishaanza tayari lakini mnawaminya hao wenzenu wa upinzani wasikusanyike hata watano.
Tokea vyama vingi viruhusiwe huo ukosoaji wa kijinga ndiyo ukaanza. Angalia hata mada za kabla ya JPM kuingia madarakani kama hazikuwa za manung'uniko.
Halafu hata kwenye social media zenu kuna walalamishi kama ilivyo humu, hamna jipya. Vyama vingi ni saratani inayotafuna umoja wa Waafrika.
Tokea vyama vingi viruhusiwe huo ukosoaji wa kijinga ndiyo ukaanza. Angalia hata mada za kabla ya JPM kuingia madarakani kama hazikuwa za manung'uniko.
Halafu hata kwenye social media zenu kuna walalamishi kama ilivyo humu, hamna jipya. Vyama vingi ni saratani inayotafuna umoja wa Waafrika.
Social media zetu kwa sasa zina wakosoaji panapostahiki, maana wamepewa uhuru wa kidemokrasia, watu wanakosoa na wengine kushauri, ila ukisoma kila wanachokisema kina mantiki ya kiaina. Ukilinganisha na hapo awali ambapo viongozi wetu walikua wanalumbana, watu walikua na hasira na waliponda kila kitu iwe kizuri au kibaya, hawakutaka kujua wala nini.
Ukwaminya watu tegemea hilo, lakini la kukosoa kwa nia njema ni jambo nzuri sana, ni vizuri watu wapige makelele ya mwizi ufisadi ukitajwa, ni vizuri watu wakosoe pale serikali inaibuka na mikakati ya ovyoo, na lipo kwetu hata leo hii, kuna wakati rais Uhuru anazingua kishenzi, lakini ile ametupatia sote uhuru wa kusema, tunalipigia makelele linatutoka moyoni.
ila BABAA alichomfanyia miguna miguna ni UNAFIKI wa waziwazi yaani swahiba wako katolewa nchini mwake kinguvu we una gonga cheers tu
Kuna nini cha ajabu kwenye michezo ya siasa, hii ni kawaida politics is about survival, Ruto hayupo hapo kisa Uhuru anampenda sana, ila yuko hapo kwa sababu amejua kucheza karata zake. Wote hao kila mmoja anacheza michezo yake kwenye level ya juu, ila furaha yangu ni pale panahitajika mambo ya kizalendo wanakutana na kuweka utaifa mbele.
Huko kwenu hata ndani ya CCM mnavurugana hakukaliki, mara mnaanikana maongezi ya simu ya viongozi wa nchi, mtu kama Membe unaanika mazungumzo yake.
umewataja wa na siasa wa Tz hapo mwishoni ktk maoni yako...sifahamu kama waelewa siasa za tz ww ? kenya najua unafahamu kuna siasa za ukabila pia....VP na genge lake wana roaming around the country to seek for what ?Miguna kiburi chake kilimponza maana yeye alibomoa madaraja yote ikiwemo baina yake na Raila.
Soma kitabu chochote cha kisiasa, utaelewa kwanini haufai kubomoa madaraja ila kujenga uelewano na kila aliyekuzunguka.
Huyo Miguna alijua ana kasoro ya kisheria baada ya kuukana uraia wake na kupokea wa Kanada kipindi kile katiba yetu haikua inaruhusu uraia pacha.
Aliporudi badala ya kuiweka sawa, akazembea kisa alikingiwa kifua na waziri wa wakati ule, sasa akaendelea kufanya madudu dhidi ya serikali, kawaida system yoyote ile huwa na taarifa zako zote na husubiri tu mud muafaka wa kuzitumia. Ndio kama mnachofanya kwa akina Makamba na Membe.
umewataja wa na siasa wa Tz hapo mwishoni ktk maoni yako...sifahamu kama waelewa siasa za tz ww ? kenya najua unafahamu kuna siasa za ukabila pia....VP na genge lake wana roaming around the country to seek for what ?