Miaka ya sabiini tulikuwa nao sambamba katika riadha, sisi tunarudi nyuma wao wanaenda mbele. Niliangalia zile mbio za mita 5,000 wanawake, si mchezo wadada wa Kenya wanatisha!. Kama ulivyosema tunahitaji kuwekeza na kuwa na subira pia, tukiwa na haraka kama kwenye mpira wa miguu tutakata tamaa mapema. Kwanza tuwekeze mashuleni ili kupata vipaji, halafu tuwekeze ili kuviinua hivi vipaji ili wawe washindani wa kweli. Nilimuona dada mmoja wa Tz alijitahidi sana, aliyekuwa wa 7 kumaliza ila ule muziki wa Wakenya si mchezo mwenyewe alikubali yaishe.