Majirani & riadha

Majirani & riadha

Kibunago

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2008
Posts
300
Reaction score
122
Muda mfupi nimeshuhudia mabinti wa ki-Kenya wakiwanyanyua Wakenya katika viti katika mashindano yanayoendelea ya mabingwa wa Afrika.
Nadhani tungewekeza katika michezo ya hivi tungewahi kupeperusha bendera yetu katika viwanja duniani
 
Miaka ya sabiini tulikuwa nao sambamba katika riadha, sisi tunarudi nyuma wao wanaenda mbele. Niliangalia zile mbio za mita 5,000 wanawake, si mchezo wadada wa Kenya wanatisha!. Kama ulivyosema tunahitaji kuwekeza na kuwa na subira pia, tukiwa na haraka kama kwenye mpira wa miguu tutakata tamaa mapema. Kwanza tuwekeze mashuleni ili kupata vipaji, halafu tuwekeze ili kuviinua hivi vipaji ili wawe washindani wa kweli. Nilimuona dada mmoja wa Tz alijitahidi sana, aliyekuwa wa 7 kumaliza ila ule muziki wa Wakenya si mchezo mwenyewe alikubali yaishe.
 
Back
Top Bottom