Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Chai hii kapeleke kijiweni kwenu. Hakuna kitu kama hiki
 
Taarifa Ina mapungufu kwanza mi nikitoa taarifa polisi yule niliyemripoti hapaswi kunijua ni polisi wenyewe wanakuja kufanya uchunguzi wakijiridhisha hakuna tatizo basi wanakuja kukwambia hakuna shida
 
Upo sahihi, hapo wa kulaumiwa ni Polisi kwa kuwataja watoa taarifa.

Kingine, huenda Polisi wamechoshwa na tabia za watoa taarifa, labda watoa taarifa wamekuwa na tabia za kunyanyasa watu mtaani kwa style hiyo ya kuwa report Polisi mara kwa mara, hivyo wakaamua kuwa expose.
 
Huu uzi ni chai na tunauchangia kwa sababu hatujanywa chai. Uongo kabisa we mleta uzi umeamua kutunywesha chai bila vitafunwa😂😂😂
 

Hiyo siô tàarifa ya tukio, NI tàarifa ya Hisia za Mtu.
Yàani Mtu atumie Hisia zake alafu akapeleke tàarifa Polisi ya Hisia zake juu ya Mtu Mwingine, kwèli?

Tàarifa za kiintelejensia hazihusu Hisia za Watu, Bali zinahusu tàarifa za kuona, kusikia, Jambo ambalo linaviashiria vya uhalifu.

Wewe Mtu upo naye mtaani, unaona anaishi Vizuri lakini Hana madhara Kwa jamii. Ila unaanza kutafuta chanzo cha Maisha yake mazuri NI kipi. Huoni hilo NI tatizo.
 
Kuishi uswahili ni kazi kama kazi nyingine.yan kabisa jamaa wameungana na kwenda kureport kisa hawa muelewi mshkaji.?

Hao jamaa wanatakiwa kuhangaishwa hivyo hivyo mahakamani mpaka akili ziwakae sawa.
 
Akomae nao tu wamlipe hyo m 500 ,,Ili aendelee kukaa ndani vzr azidi kuwakera majiranii..
 
Mleta mada ni mmoja wa majirani waliotoa taarifa polisi ndio maana ana wasiwasi😂
 
Wapigwe tu faini ya kutosha hao majirani ili wakome kufuatilia maisha ya watu. Mtu anaishi maisha yake, hajawah kukuibia wewe mchecheto wa kujua kazi yake wa nini!
 
Taarifa Ina mapungufu kwanza mi nikitoa taarifa polisi yule niliyemripoti hapaswi kunijua ni polisi wenyewe wanakuja kufanya uchunguzi wakijiridhisha hakuna tatizo basi wanakuja kukwambia hakuna shida
Polisi waliwataja watu wanaomhisi na watu hao waliitwa na polisi yeye akiwa ndani
 
umesoma vizuri ujumbe wangu?

acha kuropoka
 
Uko sahihi mkuu yaani huyu mwamba ana maisha murwa kuliko hao majirani, hizi ni fikra za ovyo sana.
 
Hata pengine nimeona kuna jirani mmoja majirani wanamvizia wamchome maana hawamuelewi.

Yeye ni kukaa ndani tu na kusafiri.
Kwa sababu hawajui mchongo wake wale wamama anaowasaidia kwa nia njema kwa kuwapa vikazi vidogovidogo kufua na usafi, wanamuhisi jamaa ni msambaza madawa, wanatunga kuwa anaposafiri kuwa anafuata mzigo, wa madawa marafiki zake wanapokuja wanasema ndio huwa wanakuja kununua.

Kwa utafiti wangu sasa dunia iko mbali sana. Kazi za kijadi zinabaki kwenye uelewa wa wananchi ambao hawana updates. Kuna watu wanafanya kazi hadi dubai na kila baada ya mwezi wanarudi kupumzika. Kama hujui unaweza kudhani ni jambazi au muarifu.

Nilichogundua mtu ukiwa na kazi na namna hiyo kubet, youtuber, freelancer, content creator, kazi za shift oversea inabidi ukae eneo lenye watu waelewa wasiofuatiliana maisha, ukikaa uswahilini labda ukajielezee kwa kitongoji kama hutaki shida. Watakutungia vitu tu.
 
Kama inawezekana tupe elimu za hao majirani na kabila gani pia inatatanisha
 
Mbu kanyea Kambi subiri matokeo🤣🤣🤣
 
hii hata kama ni chai kama wanavyoongea wadau, ila tuache kufuatiliana kwenye maisha

Kuna sehemu nimehamia na nimejenga ila hao majirani kwenye kupiga nao story utasikia hivi unafanya kazi wapi?
Hili swali la kipumbavu huwa silijibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…