Majirani wanao jishtukia na kuvikana tabia zisizo na ukweli

Majirani wanao jishtukia na kuvikana tabia zisizo na ukweli

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Tupo mwanzo wa wiki na mwezi nao ndio unayoyoma.. kwa wenye mishahara mwisho wa mwezi vibunda vimekaribia Mwaisa, unyama mwingi, hapa kazi tu, tuendelee kuupiga mwingi In every day, enjoy to the Maximum. Fight to complete 💪🏿 what you plan to do, as early as possible.

Niseme mawili matatu.. Kuna mtaa (rural area) ninakaa ambao nina kama Nusu mwaka tu, kwa kazi yangu na hobb yangu kama kucheza mpira (ndondo tu mtaani) kunanipa nafasi ya kujuana/kukutana na watu wengi lakini watu hao wote marafiki kwangu ni wachache sana.

Kuna vitu nakutana navyo kwa majirani na marafiki vinanishangaza sana...Mimi nilivyo kwanza, sio mtu wa kuogopa kuchukiwa au kusemwa vibaya na watu, yani mtu akinisema huwa naona ndio kama Ananipaisha na kuniongezea sifa tu.

Nina jirani yangu Hapa mmoja anaishi na mdogo wake, wote huwa tunacheza mpira uwanja mmoja.. ni wastarabu vizuri tu ila sijui ni ustarabu kuzidi au na kutopenda ukaribu sana na watu, mie sijui.. kama majirani huwa kuna Vitu mtashare tu, mfano ukiwa kwake ukikaribishwa kula hata kama huna njaa jirani akikushurutisha kula, inakubidi lakini mimi ninacho washangaa mimi nikiwakaribisha kwangu wanakua wazito au kupokea ninacho wapa, wanakua kama hawamini amini hivi

Dogo wa jirani yangu ni jobless lakini cha ajabu unaweza kuta hajaenda kunywa chai ukimwambie twende tukapige hata supu hapo nyuma, yani anakua mgumu, atatufuta sababu ya kukataa

Sasa kwenye swala la Mahusiano na mapenz hapo ndo pasua kichwa yani hadi nashangaa.. mimi nikisimama tu na mwanamke naonekana kama namtaka, kuna wadau ground(uwanjani) wanachuki hatusemeshani kisa niliwahi kusemeshana na mademu zao, na wakati mimi sijawai kula demu wa mtu hata mmoja.
Kiasi kwamba wasichana wengine nakwepa na kuwakaushia hata salamu nikiogopa chuki kwa mabwana zao.
nikijua msichana fulani, anatoka na fulani basi inanibid nikae mbali na huyo binti

Mimi ni mgumu kupenda lakini nikipenda huwa napenda mazimaa, so sina tabia ya kubadili badili wanawake (umalaya) lakini cha ajabu kila rafiki yangu wa kiume huku hunishuku mimi ni mzee wa mademu, hadi naanza kujitetea nacha kusikitisha nipo single yani hata bebi wa kunitumia sms umeamkaje sweet hayupo yani.

Nikawa naumueleza dogo hapa jirani, Mfano jana tunacheki Match ya simba, nikawa namwambia.. mimi sina girlfriend just why toka tuanze kuangalia mpira hadi unaisha na masaa tuliokuwa tumekaa hapa hujaniona nashika simu yangu kuongea na mtu wala kutuma sms, kama wewe, huwezi kuniona nipo busy nachat DM, ukiona nachat basi ni social network au message mbili au tatu za kikazi full stop.
Naeleza hayo lakini haniamini.

Naomba wanaume tuache huu ukatuni huwezi kumchukia mwanaume mwenzio kisa tu umesikia alisimama na hawala yako, hayo mambo yanazungumzika 😃😃😂

Sharauti wasukuma wote nasema hivi acheni ushamba.
 
Tupo mwanzo wa wiki na mwezi nao ndio unayoyoma.. kwa wenye mishahara mwisho wa mwezi vibunda vimekaribia Mwaisa, unyama mwingi, hapa kazi tu, tuendelee kuupiga mwingi
In every day, enjoy to the Maximum. Fight to complete [emoji1548] what you plan to do, as early as possible.
Hapo kwa wasukuma nasapoti

Yaani mtu ni demu wako lakini una mtreat kama mke na wivu wakishamba

Tabia zao ni hizi hapa

Anatongoza demu akikataliwa anakuja sema ni demu wake so wana hawamsogelei

Ukisimama na demu wake pekee yenu kama wapo wawili wanajua wanaweza kukudhibiti wanakuja kukushika matai

Ubaya huku nilipo mademu zao wanapenda ngono sana na wageni tunapendwa
 
Majirani siku zote wanataka mfanane kiuchumi,kimahusiano na hata maendeleo Ukionesha dalili za kumove on unatafuta utata bro. Hapo ni kuuchuna tu jiandae kila baya kutupiwa wewe mpaka uhame!
 
Mkuu huwezi kabisa kufocus kwenye mambo yako ,inaonekana wewe jamaa unapenda shobo Sana ,unashobokea watu ambao hawana mpango na wewe ,kama huyo unamwambia mkanywe supu hataku ,kiufupi haluelewi na anakuona msumbufu ,eti unawagawia watu vitu wanachukua kwa kusuasua ,yaani wanakuona wewe ni jinga ,unapenda kushobokea watu ...

Acha kujifanya wewe ni mzee wa shobo ,unashobokea Hadi na wake za watu ,mademu za watu,unajifanya wewe ni mtu wa kusocialize utakuja kufanywa kitu mbaya ,
 
Wewe wamekufanya mala ngapi.
 
Mimi ni mgumu kupenda lakini nikipenda huwa napenda mazimaa, so sina tabia ya kubadili badili wanawake (umalaya) lakini cha ajabu kila rafiki yangu wa kiume huku hunishuku mimi ni mzee wa mademu, hadi naanza kujitetea nacha kusikitisha nipo single yani hata bebi wa kunitumia sms umeamkaje sweet hayupo yani.
Nafikiri tangazo lako lilikuwa ndio hili hayo mengine ni utangulizi na Hitimisho tu
 
Back
Top Bottom