PostGE2025 Majizzo: Tuheshimu muziki, tusiwapangie wasanii Chama. Tumewaadhibu kwasababu ya shughuli za kichama

PostGE2025 Majizzo: Tuheshimu muziki, tusiwapangie wasanii Chama. Tumewaadhibu kwasababu ya shughuli za kichama

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Naelewa hasira, uchungu na hisia nyingine zilizoletwa na kile kilichotokea hasa baada Oktoba 29, lakini nadhani pamoja na yote hayo tuwaze tena ndugu zangu.

Namtolea mdogo wangu Nay mfano kwa sababu hata yeye anaathirika kwa hili japo tunajua mrengo wake wa kisiasa. Kina Rosa Ree na wengine, kuna riziki wanaikosa tukihukumu muziki kwa ujumla wake kwani tunakosa matamasha na show nyingine.

Tuupe nguvu muziki wetu bila kujali itikadi.
Mungu amrehemu Ruge Mutahaba, asingekaa kimya muziki ukishambuliwa hivi. Yeye aliwapeleka wasanii kwenye show za Ikulu na CCM, lakinia bado wakitoka walikuwa wanaendelea na muziki kwa sababu taifa linahitaji muziki nyakati zote.

Sisi tulio hai, tufanye wajibu huu kwa uaminifu na uzalendo. Tulinde muziki wetu uzidi kukua mbele ya muziki toka nje.
 
View attachment 3514161
WASANII NA SANAA . TUWAUNGE NDUGU ZETU HAWA. SOTE TUNATEGEMEA SANAA
 
Mungu amrehemu Ruge Mutahaba, asingekaa kimya muziki ukishambuliwa hivi. Yeye aliwapeleka wasanii kwenye show za Ikulu na CCM, lakinia bado wakitoka walikuwa wanaendelea na muziki kwa sababu taifa linahitaji muziki nyakati zote.

Sisi tulio hai, tufanye wajibu huu kwa uaminifu na uzalendo. Tulinde muziki wetu uzidi kukua mbele ya muziki toka nje.
View attachment 3514161
Simjio Majizo mwambie apeleke rubbish huko ccm
Wasanii are killers of democracy. Let them die, get rotten and have filthy smell
 
Angeamua kubaki kimya kuliko kuongeza hasira kwenye mioyo ya watanzania.
Mbona mauaji ya halaiki October 29 vyombo vyake vya habari havikuripoti kitu chochote.
Huyu mpumbavu anatetea ugali wake na sio kwamba anawajali wasanii
 
Wakafanye show zao huko wanakoitwaga!

Ova
 
Mimi nawalaumu ccm.wao ndo wamewagawa wasanii.yaani msanii akienda upinzani KOSA .NDO MAANA WASANII WANAOGOPA.
kuwe huru msanii aende chama chochote anachotaka
 
Mimi nawalaumu ccm.wao ndo wamewagawa wasanii.yaani msanii akienda upinzani KOSA .NDO MAANA WASANII WANAOGOPA.
kuwe huru msanii aende chama chochote anachotaka
Mkuu unajua CCM bado wapo kwenye Chama kimoja kama China au Russia ndiyo maana mtu yoyote awe Msanii mtumishi wa umma, Mfanyabiashara akijaribu kujiunga na vyama vya Upinzani anaoneka adui wa nchi anatumiwa na Wazungu, Siasa zetu zinatakiwa zitoke huku tulipo, Katiba hii ni ya Chama kimoja ilitengenezwa kwenye mifumo ya Dora ya Chama kimoja, Tofauti na Ghana, Kenya, Nigeria, hizi nchi Wananchi wapo huru na Wasanii na watu mashuhuri wapo huru kuchagua upande wa kufanya Siasa, kwa Tanzania ni tofauti ili Mambo yako yaende inakubidi uwe upande wa CCM, mfano Dainamo akiamua kuipigia lampeni Chadema na mwisho wa siku CCM wakashinda lazima Daimond atasumbuliwa kwenye Mambo yake binafsi ya kiuchumi na Maisha ya kila siku, ndiyo Maana Wasanii wanajipendekeza kwa watala ili mambo yao yaende ata wakifanya makosa polisi waogope kuwachukulia sheria, Polisi wakiona Msanii au mfanyabiashara kakaa Meza moja na Rais au kapiga picha na Raisi tu, Polisi wanaingia hofu kwa kujua itapigwa simu kutoka juu.
 
Back
Top Bottom