Anaitwa Abdulrahman Amiri Shimbo.
Alikuwa katika kikosi cha JWTZ kilichotumwa Seychelles kufundisha Jeshi la visiwa hivyo.
Major Abdulrahman Shimbo alikwenda Seychelles mwaka 1978 kuwa katika kikosi cha JWTZ kilichoongozwa na Lt.Col.Hassan Ngwilizi.
Hassan Ngwilizi alikuwa mwalimu wa Abdulrahman Shimbo chuo cha maofisa wa jeshi MonduliJ
Mwaka 1980 Lt.Col. Ngwilizi alirudi Tanzania, hivyo Major Shimbo akawa mkuu wa kikosi kilichokuwa Seychelles.
Mwaka 1981 Seychelles ikavamiwa na askari wa kukodiwa waliolenga kupindua Serikali ya nchi hiyo.
Jaribio hilo lilizimwa na kikosi cha JWTZ na kupelekea mamluki hao kuteka ndege na kutoroka kwenda Afrika ya Kusini.
Abdulrahman Shimbo alipanda ngazi za utumishi JWTZ mpaka kufikia kuwa Mnadhimu Mkuu, na alistaafu akiwa na cheo cha Luteni Jenerali.
Sikiliza mahojiano aliyofanya na Azam TV kipindi cha Zumari kujua historia yake, na kilichotokea Seychelles mwaka 1981.