ngakotecture
JF-Expert Member
- Dec 30, 2014
- 2,569
- 2,847
mzee wa meremeta uyo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio lenyewe na ukiacha hiyo kashfa ya Hele.za wajed pia kulikuwa na kashfa ya kuwa na hela nyingi sana kwenye bank za south africa.Kuna jina ninalifananisha na hili, liliwahi kuingia kwenye kashfa ya kula hela za wajeda mabilioni ya shilingi!
mzee wa meremeta uyo
Rene alimlaumu sana Nyerere kuingilia masuala ya Seychelles. Nimesahau hii historia kwa mapana. Ila all in all, sijui kwanini mambo mengi wanadanganya nchi hii. Hovyo sana!
Ahsante JokaKuu
Mtangazaji alimkatiza bila kumpa nafasi ya kueleza zaidi kuhusu Seychelles baada ya jaribio kuzimwa. Askari walitoka wapi na walikuwa na lengo la kumweka nani madarakani?
Wakati huo Albert Renne kama sikosei alikuwa wapi?
Pili, mtangazaji hakumpa nafasi ya kueleza amefanya kazi na akina nani.
Nadhani mwaandaji hakuwa na background ya kutosha.
Kwa CV ya shimbo hapo tungewasikia akina Sarakikya, Twalipo, Kiaro n.k.
Mtangazaji angeandaa sehemu ya pili na ni vema ikiwa Watangazaji watatafuta maoni kabla ya kuhoji watu wazito kama hao.
Mathalani angemuuliza Balozi Shimbo, wakati akiwa CoS kwanini alisema 'jeshi litachukua hatua wakati wa uchaguzi wa kiraia Tanzania"? Kulikuwa na viashiria gani wakati huo n.k
Ok itakua nimechanganya jina...Rene anamlaumu vipi Nyerere wakati ndiye aliyemsaidia akadumu madarakani?
..Unless umemchanganya na mpinzani wake ambaye ilikodi hao mercenaries waliobambwa na Jwtz?
Ok itakua nimechanganya jina.
Ni mambo niliyasoma kitambo sana siasa za visiwani huko
Anaitwa Abdulrahman Amiri Shimbo.
Alikuwa katika kikosi cha JWTZ kilichotumwa Seychelles kufundisha Jeshi la visiwa hivyo.
Major Abdulrahman Shimbo alikwenda Seychelles mwaka 1978 kuwa katika kikosi cha JWTZ kilichoongozwa na Lt.Col.Hassan Ngwilizi.
Hassan Ngwilizi alikuwa mwalimu wa Abdulrahman Shimbo chuo cha maofisa wa jeshi MonduliJ
Mwaka 1980 Lt.Col. Ngwilizi alirudi Tanzania, hivyo Major Shimbo akawa mkuu wa kikosi kilichokuwa Seychelles.
Mwaka 1981 Seychelles ikavamiwa na askari wa kukodiwa waliolenga kupindua Serikali ya nchi hiyo.
Jaribio hilo lilizimwa na kikosi cha JWTZ na kupelekea mamluki hao kuteka ndege na kutoroka kwenda Afrika ya Kusini.
Abdulrahman Shimbo alipanda ngazi za utumishi JWTZ mpaka kufikia kuwa Mnadhimu Mkuu, na alistaafu akiwa na cheo cha Luteni Jenerali.
Sikiliza mahojiano aliyofanya na Azam TV kipindi cha Zumari kujua historia yake, na kilichotokea Seychelles mwaka 1981.
CoS Shimbo alionekana kuwa tayari sana kueleza ''declassified' information kwa bahati mbaya muongozaji hakuwa na background ya mambo mengi. Kwa mfano aliposema Msumbuji hapo CoS T. Kiwelu angetajwa kwasababu alishiriki sana na Shimbo angeeleza.Nguruvi3,
..katika mahojiano hayo Shimbo anadai alipoitwa makao makuu alidhani anapelekwa Msumbiji, au Zimbabwe.
Tatizo ni lile lile la muongozaji kutokuwa na ufahamu wa nyuma! huenda alikuwa amdogo lakini kazi yake inamruhusu kujifunza na ni muhimu kufanya homework kabla ya kukutana na watu kama Shimbo...Watz wengi hawajui mchango wa Jwtz ktk vita vya ukombozi wa Zimbabwe, ni bahati mbaya kwamba muongoza kipindi aliacha hilo likapita.
Halaf kuna wajinga wanakuja hapa wanasema sijui Rwanda ni kiboko sijui nyenyenye 🚮
baada ya kuwakamata wanajeshi wa kukodi wengi kutoka france na south Africa jw wakaweka silaha chini wakawaambia wapigane shimbo anakuja kufika alkuta wazungu wanamanundu ya kutosha 😂😂😂😂😂..hata mimi nadhani mtangazaji hakuitendea haki interview hii.
..naona kama ametunyima watazamaji nafasi ya kumsikia Abdulrahman Shimbo akifunguka kuhusu mission ya Jwtz nchini Seychelles.
..naweza kukubaliana na wewe kwamba mtangazaji hakuwa amejiandaa na hakujuwa anakwenda kumhoji mtu wa aina gani.
..tukirudi kwenye hiyo operation, kunapotokea crisis ktk uwanja wa ndege, na kukawa na raia ktk eneo hilo, ni lazima yafanyike mambo mawili.
1. Uwanja wa ndege lazima uwe sealed kwamba hakuna anayeingia na kutoka.
2. Ni lazima ndege zizuiwe kuruka na kutua. Haitakiwi kuwe na vyombo vinavyoruka karibu na eneo hilo.
..Sasa Shimbo wakati huo akiwa Major na incharge wa kikosi kilichokuwa Seychelles anaeleza kuwa aliwasiliana na ndege iliyokuwa inatarajia kutua Seychelles na kujaribu kuizuia.
..Ukisoma sources nyingine zinadai mercenaries waliteka control tower na kuanza kuzungumza na ndege na kuiruhusu itue.
..Kwa hiyo bila shaka rubani alitua kwa maelekezo ya mercenaries waliojaribu kupindua serikali.
..Na hao mercenaries walitoroka kwa kutumia ndege hiyo kwasababu ndege waliyotua nayo ilikuwa imeharibiwa.
..Jambo lingine la kulizingatia ni usalama wa RAIA waliokuwa ktk ndege iliyotekwa na kutorosha hao mercenaries toka Seychelles.
..Kuhusu umuhimu wa mission ya Jwtz Seychelles, kwa maoni yangu ni busara zaidi kupigana vita nchi ya mipaka yako, kuliko kuruhusu vita ije nchini kwako.
wote tulkua wajamaa at by that time coldwar ilkua imetamalaki lkn pia south ilkua chini ya makaburu..Tz ili-support upande mmoja dhidi mwingine huko Seychelles.
..kwa hiyo ni kweli kabisa kwamba tuliingilia mambo yao.
..na upande ambao tuliunyima support lazima utulaumu. Na ndio hao waliokwenda kutafuta msaada kwa makaburu wa Afrika Kusini na Walowezi wa Rhodesia.
..lakini uwepo wetu Seychelles naamini ulilenga ktk suala zima la USALAMA wa Tanzania.
Anaitwa Abdulrahman Amiri Shimbo.
Alikuwa katika kikosi cha JWTZ kilichotumwa Seychelles kufundisha Jeshi la visiwa hivyo.
Major Abdulrahman Shimbo alikwenda Seychelles mwaka 1978 kuwa katika kikosi cha JWTZ kilichoongozwa na Lt.Col.Hassan Ngwilizi.
Hassan Ngwilizi alikuwa mwalimu wa Abdulrahman Shimbo chuo cha maofisa wa jeshi MonduliJ
Mwaka 1980 Lt.Col. Ngwilizi alirudi Tanzania, hivyo Major Shimbo akawa mkuu wa kikosi kilichokuwa Seychelles.
Mwaka 1981 Seychelles ikavamiwa na askari wa kukodiwa waliolenga kupindua Serikali ya nchi hiyo.
Jaribio hilo lilizimwa na kikosi cha JWTZ na kupelekea mamluki hao kuteka ndege na kutoroka kwenda Afrika ya Kusini.
Abdulrahman Shimbo alipanda ngazi za utumishi JWTZ mpaka kufikia kuwa Mnadhimu Mkuu, na alistaafu akiwa na cheo cha Luteni Jenerali.
Sikiliza mahojiano aliyofanya na Azam TV kipindi cha Zumari kujua historia yake, na kilichotokea Seychelles mwaka 1981.