..ni uzushi kudai huyu bwana alikamatwa na Interpol.
..kabla ya huo ukamataji ni lazima awepo anayemtafuta.
..sasa unajiuliza ni jeshi gani la Polisi lilikuwa linamtafuta?
..pia huyu bwana ni askari wa Jwtz, hivyo wenye mamlaka ya kumkamata ni military police / mp wa Jwtz.
..hata tukidai alikamatwa nje ya nchi, maofisa wa ngazi za juu kama huyu bwana kusafiri kwa kutumia pasi za kidiplomasia / diplomatic passport. Sheria za kimataifa zinazuia ukamataji wa wasafiri wenye diplomatic passport
..tunapotoa madai tujitahidi kutoa taarifa zenye mantiki, na zenye ukweli ndani yake.
..VIJANA wa Kitanzania mnachosha sana kuwaelimisha. Yaani mnadanganyika kwa mambo mepesi mnooo.
..Kama mtu unaweza kufika hapa JF unatakiwa uwe unajua mambo mepesi kabisa niliyokueleza halo juu.
NB:
..inawezekana huyu bwana alimung'unya mapesa ya umma, lakini sio kwa namna ilivyowasilishwa hapa JF. Na kama alihusika basi itakuwa alishirikiana na watu wa juu yake, na chini yake.
Cc
MALCOM LUMUMBA,
Nguruvi3