Major General Mbuge Kuwa RC kutoka Mkuu wa JKT Kapanda Cheo au kashuka?

Habari wanabodi? naomba kupata uelewa kidogo, kwa nafasi kama ya Major General Mbuge kutoka kuwa Mkuu wa JKT na kwenda kuwa RC je hapo kapanda cheo ama kashuka? naomba uelewa wa kina juu ya hili tafadhali.

Hongera kwake kwa uteuzi!!
Kiherehere chake kimemponza.
 
ADC wa Kikwete Brigedia General M.N Mkeremy ndiye anaenda kuwa mkuu wa JKT Tanzania
 
Mkuu wako wa majeshi mabeyo huwa anampigia salute DC Jokate mwegelo
Pia anapigia saluti hata maiti ya mjane wa mkulima... saluti sio big ishu kiviile

Tujiwekeze kwenye mada tu
 
Au Diwani alipotoka DCI hadi Ras Kagera, halafu huu Mkoa ndio mara kwa mara unatumika kwa kazi hiyo sijui kwanini
Nature ya watumishi wa ofisi yake pale. Toka vita vya Kagera na baadaye wimbi la ukimbizi kutokana na civil war za rwanda-urundi; watumishi wa pale wamekuwa wakipelekwa kwa tahadhari kubwa. Kwa hiyo hata maboss wao inabidi wawe na mbawa kama zao.
 
Mkuu wako wa majeshi mabeyo huwa anampigia salute DC Jokate mwegelo
Unajua maana ya Salute? Nini DC? Na wewe unaweza kupigiwa salute ikiwa umekufa. Salute kwa yeyote aliye teuliwa na Rais. Inaonekana kuwa CDF anapiga salute, kwakweli ni kwamba anapokea salamu toka kwa DC. Kwa kuitikia kwa salute
 
Hujielewi wewe. Rais anakutana wapi na Wakuu wa Mikoa!? Kwenye kikao gani!?
 
Ibughe alikuwa kanali sasa Brigedia yule wa PCCB alikuwa Brigedia sasa ni Meja General tena last weeks

Mara nyingi kijeshi ukishapanda rank tegemea kubadilishiwa majukumu muda wowote
Kupanda kwake rank ni kutokana na upandaji wa madaraja kwa Watumishi wa Umma. Zoezi ambalo linaendelea kwenye kada mbalimbali.

Kwa ufupi tu, Ibuge, Mbungo na Mbuge, wamepata demotion kwenye madaraka ya kiraia.
 
Hujielewi wewe. Rais anakutana wapi na Wakuu wa Mikoa!? Kwenye kikao gani!?
Wewe ndiye hujui iwapo unadhani rais kukutana na mkuu wa mkoa ni kupitia vikaoni. kwani hata huelewei kuwa mkuu wa mkoa ni mwakilishiwa rais mkoani mwake.
 
Wewe ndiye hujui iwapo unadhani rais kukutana na mkuu wa mkoa ni kupitia vikaoni. kwani hata huelewei kuwa mkuu wa mkoa ni mwakilishiwa rais mkoani mwake.
Wewe unayejua si useme! Serikali inafanya kazi kupitia vikao. Sema sasa ni kikao gani Rais anakaa na hao wakuu wa mikoa.
 
Wewe unayejua si useme! Serikali inafanya kazi kupitia vikao. Sema sasa ni kikao gani Rais anakaa na hao wakuu wa mikoa.
Serikali haifanyi kazi kwa kupitia vikao bali inatekeleza sheria. Kama sheria inataka kuwe na vikao hilo ni jambo jingine, ila sheria ya sasa inasema kuwa Mkuu wa mkoa ni mwakilishi wa rais mkoani mwake! Full stop. Mawasiliano kati ya rais na wakuu wa mikoa yako open 24hrs.
 
Hujielewi wewe. Baki na ujinga wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…