Elections 2010 Majukumu Makuu ya CHADEMA

Mzee Mtei siku zote kumbuka kuwa kumsema mwenzio ni raha saaana na kusemwa wewe ni chungu mno.

Wewe Mwl hakukupa fursa ya kukusikiliza na badala yake ukatimuliwa (though wewe unadai ulishaamua kuacha kazi pia). Au nikuulize, je wakati unatimuliwa kulikuwa na demokrasia? Ulisikilizwa kama ulivyostahili? Je wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kesi zao zipo mahakamani wanaposemwa kwenye majukwaa ya kisiasa unafikiri wanajisikiaje? (nchi yetu ni ya utawala wa kisheria kumbuka) Ungekuwa ni wewe unatuhumiwa tu (na moyoni unajijua hauko fisadi) unaposemwa hadharani utajisikiaje?

Tufikirie leo viongozi au wagombea wa vyama wanaanza kutuhumiana kwa tuhuma binafsi tutakuwa tanatathmini nini? Tuhuma ama hoja za kuleta maendeleo? Kama CCM walivyo na mapungufu hata Chadema pia mnayo, think about tribalism scandals, ufisadi wa Mbowe (two years ago), (au unataka kusema mliliona hilo ndiyo maana mkaamua Mbowe asigombee Uraisi?), uadilifu ktk maisha ya kindoa n.k. Kumbuka kwa kila mahali kuna aina ya watu tofauti tofauti, kuna wazuri na wabaya, wema na wasio wema, wezi na waibiwa, na kadhalika na kadhalika.

Unaweza ukawa mwanzilishi wa Chama ukifikiria kuwaletea watu wako mabadiliko ya kiuchumi kumbe wenzako ulio nao pamoja wanafikiria Chama hicho hicho kitawafanya wachumie matumboni mwao. Kama ilivyo CCM hata nanyi Chadema ni vivyo hivyo. Hata mabadaliko mnayoyasema yataonekana kwa siku 100 ni ndoto tu, its just a gear of bringing political change rather not solving core problems facing our country!

Usitudanganye sana Mzee Mtei! kuwa halisi, Sio wote tunakubaliana na wewe!
 
ASANTE BABU.
LABDA WATAKUSIKIA WEWE, MVUMO AND MWENDO KASI WA UPEPO WA SLAA ni mkali mno, na unaumiza vichwa vya wanaCCM, ndio maana Kinana kanena kukanusha yaliyosemwa ktk Uzinduzi wa kampeni ya CHADEMA. Kukmbuka alipoulizwa mbona hata CUF wamerusha akasema atajibu siku nyingine lkn kwa chadema majibu yapo. kisa HOFU YA ANGUKO. the time has come and it is here to make change in leadership, si mmesikia watu wameanza kuwazomea kwenye kampeni zao,
LA KUFURAHISHA NI KUWA WATANZANIA NI WAVUMILIVU. ILA SASA HAWADANGANYIKI TENA.
PIGENI MBIU HADI VIJIJINI, HABARI HIZI ZIWAFIKIE WANANCHI WOTE KUWA UFALME WA TANZANIA UREJESHWE KUWA MIKONONI MWA WATANZANIWATANZANIA. NI LAZIMA KAULI ZA NCHI HII INA WENYEWE ZIKOME, BALI KILA MTU AIMBE TANZANIA NI YETU SOTE.

NATAMANI NIONE MTANZANIA AKIPEWE HESHIMA KULIKO MGENI.

UZAWA JAMANI UZAWA JAMANI.

NIJIVUNIE KUWA MTANZANIA

VOTE FOR CHANGE
 
Mzee Mtei siku zote kumbuka kuwa kumsema mwenzio ni raha saaana na kusemwa wewe ni chungu mno.

Wewe Mwl hakukupa fursa ya kukusikiliza na badala yake ukatimuliwa (though wewe unadai ulishaamua kuacha kazi pia). Au nikuulize, je wakati unatimuliwa kulikuwa na demokrasia? Ulisikilizwa kama ulivyostahili? Je wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kesi zao zipo mahakamani wanaposemwa kwenye majukwaa ya kisiasa unafikiri wanajisikiaje? (nchi yetu ni ya utawala wa kisheria kumbuka) Ungekuwa ni wewe unatuhumiwa tu (na moyoni unajijua hauko fisadi) unaposemwa hadharani utajisikiaje?

Tufikirie leo viongozi au wagombea wa vyama wanaanza kutuhumiana kwa tuhuma binafsi tutakuwa tanatathmini nini? Tuhuma ama hoja za kuleta maendeleo? Kama CCM walivyo na mapungufu hata Chadema pia mnayo, think about tribalism scandals, ufisadi wa Mbowe (two years ago), (au unataka kusema mliliona hilo ndiyo maana mkaamua Mbowe asigombee Uraisi?), uadilifu ktk maisha ya kindoa n.k. Kumbuka kwa kila mahali kuna aina ya watu tofauti tofauti, kuna wazuri na wabaya, wema na wasio wema, wezi na waibiwa, na kadhalika na kadhalika.

Unaweza ukawa mwanzilishi wa Chama ukifikiria kuwaletea watu wako mabadiliko ya kiuchumi kumbe wenzako ulio nao pamoja wanafikiria Chama hicho hicho kitawafanya wachumie matumboni mwao. Kama ilivyo CCM hata nanyi Chadema ni vivyo hivyo. Hata mabadaliko mnayoyasema yataonekana kwa siku 100 ni ndoto tu, its just a gear of bringing political change rather not solving core problems facing our country!

Usitudanganye sana Mzee Mtei! kuwa halisi, Sio wote tunakubaliana na wewe!

Sheria ziko wazi. Ukiwa na kesi ya jinai unasimamishwa kazi mpaka kesi iishe. Ukishinda unarejeshwa kazini ukishindwa ntolee. WanaCCM wao wana kesi za jinai lakini wanapeta bungeni na kwingineko halafu mnapita huko na kule kujidai kwamba kesi za EPA ziko mahakamani.

Acheni uongo na mumwogope Mungu!
 
Ahsante Awo keshaelewa wapi alikosea. Ahsante mzee Mtei kwa mchango wako.
 
SHY sasa naona utaka kukaribisha mamaluki jikoni. Be vetry careful.
 
Nataka kuongezea kuwa jukumu jingine kuu la Chadema sasa ni kujiandaa kuchunga kura tutakazopigiwa na Watanzania wanaoridhika kwamba sisi ni chama m'badala wa CCM na kwamba Dk. Slaa atafaa zaidi kuliko Kikwete.
CHADEMA isiridhike na hamasa ya wananchi kwa sasa! Japokuwa kazi ya kulinda kura ni muhimu sana, Kikubwa kwa mtazamo wangu ni kuweka nguvu zaidi kuelimisha Jamii ya kitanzania juu ya Ilani ya Chama, na Umuhimu wa mageuzi. Watanzania wanatakiwa kuelewa kuwa hawatapata kipya bila kubadilika na kubadili mfumo wa utawala. Kwa mimi nionavyo CCM walifanya kazi ya kuleta uhuru wa KISIASA, lakini hawana mbinu yoyote ya Kuwaletea Watanzania uhuru wa KIUCHUMI.

Hili likielimishwa vizuri wananchi wakielewa umuhimu wa kuchagua chama mbadala CHADEMA haitakuwa na sababu ya kuwa na wasiwasi wa kuibiwa kura. Kura zinaweza kuibiwa pale panapokuwa na tofauti ndogo na wananchi kutojua wajibu wao. Lakini wakielewa Sera nzuri za Chadema na uhumu wa mabadiliko wao ndio watakuwa wakwanza kuzisimamia kura.

Pili Jambo muhimu katika miezi hii miwili iliyobaki ni chama kujilinda na mbinu zozote chafu zinazoweza kukipotezea chama sifa. Hapa napo panahitaji nguvu sana. CCM wanaonyesha maji yapo shingoni ndio mana inashangaza Mgombea wao anayeomba kipindi kingine kutumia nguvu kama vile ni mara yake ya kwanza.

Kwa miaka mitano katumia rasilimali za taifa kuzunguka nchi nzima, na kutumia vyombo vya habari lakini bado hajakubalika. Na kwa sababu hiyo nguvu wanayotumia CCM wakiona haina mafanikio wataingia kwenye mchezo mchafu kwa hali ya juu! Nadhani week end dalili zimeanza kuonekana kwa wao kutumia vyombo vya habari. Hivyo Mwito wangi ni kwa Chadema kuwa makini sana na kuibua hujuma yoyote kwa wananchi kujua na hata jamii ya kimataifa.

Baada ya hayo kukamilika, na Chadema ikiwa na hazima kubwa ya wapiga kura, basi nadhani zoezi la kulinda kura litakuwa rahisi. Hivyo NI KUWA MAKINI MANA SAFARI NDIO KWANZA IMEANZA, japo ni busara kuangalia mwisho wa safari, lakini ni vyema kuepuka kuanguka hapa njiani!

Mwisho naona vyombo vya habari, kwa jinsi inavyoelekea, mana ndio kwanza kampeni zimeanza, vitaleta matatizo makubwa sana mwaka huu. hawa waandishi na wahariri wakumbushwe kuwa chochote kitakachotokea wao watakuwa wa kulaumiwa. Wajue matatizo yatawakuta wao wenyewe, watoto wao, familia zao, marafiki na majirani zao. Wasipokuwa makini na kazi yao watawatesa sana watoto na ndugu zao, kani machafuko hayatamchagua mtu. Na hao viongozi wanowachochoa wasifikirie watakimbia, siku hizi kuna Mahakama ya Kimataifa...wamuulize raisi wa SUDAN soon ataingia kwenye mikono ya mahakama.

MUNGU WABARIKI WATU WA TANZANIA
 
Avanti
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
  • email.png
    Send Email
user-online.png
Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join Date Tue Aug 2010
Posts 3
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power0
Mzee huna haja ya kuhangaika na huyu. Woooote waliojiunga Augu 2010 tunajua shida yao
 
Nilipofunga kompyuta yangu asubuhi leo ili nishughulikie mambo binafsi yanayoniletea kipato, nilikuwa nimechangia kwa ufupi topic kwamba "Watanzania si Mabwege" any more. Mhe. Kinana alikuwa amenukuliwa au alijieleza kuhusu misimamo ya chama chake cha CCM, kwamba WaTz. si mabwege, na eti Chadema wanadhani hivyo, kwa kuteua mgombea mwenza asiye na degree.

Kama Muasisi wa Chadema, nilisisitiza ni jukumu la Chadema hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi, kufichua uoza wa CCM na kuonyesha weaknesses za viongozi wao, tukiwataja majina pale tulipo na ushahidi. Hiyo ndio demokrasia. Tunahitaji ujasiri na uzalendo ili wananchi wapate viongozi adilifu.

Nilipofungua kompyuta baadaye nilimkuta Mhe. Kinana akizunguzia Chadema 'Kupotoka' kwa kutaja watu ambao kesi zao za ufisadi ziko mahakamani. Kinana namheshimu sana kwa vile amepata kuongoza wizara nyeti serikalini kama mimi. Lakini serikali wakati wetu, ikimshutumu mtu yeyote, ingeshauri CCM ya wakati huo isimteue Mgombea! Sisi Chadema tunasema "Mafisadi pamoja na Watuhumiwa wa ufisadi Ziiiiii". Watanzania msikubali kupotoshwa na wakina Kinana Oktoba 2010. Hawakubaliki!

Nataka kuongezea kuwa jukumu jingine kuu la Chadema sasa ni kujiandaa kuchunga kura tutakazopigiwa na Watanzania wanaoridhika kwamba sisi ni chama m'badala wa CCM na kwamba Dk. Slaa atafaa zaidi kuliko Kikwete.

Ni lazima kila kituo cha kupigia kura kiwe na wakala wetu shupavu, mkali na jasiri. Ahakikishe ni mpiga kura stahiki tu anapiga kura, na mara moja tu. Ujanja wa CCM kuleta watu wao kurudia kupiga kura, au kununua vitambulisho ili wapenzi wetu washindwe kupiga kura vifichuliwe mapema. Hakuna kulala, mpaka kieleweke.

Namalizia kuwatahadharisha wananchi wenzangu kwamba yaliyotokea pale Jangwani juzi, ambapo wafanyakazi wa TBC walirushiwa mawe na wapenzi wa Chadema wakati TBC walipositisha matangazo 'live' ya mkutano wao, yanaashiria uvumilivu wa WaTz. unafikia kikomo.

Endapo dalili za kutumia vyombo vya umma, kama TBC, ili kuhujumu au kukandamiza upinzani halali zitaendelezwa na serikali, CCM na viongozi wake watabeba lawama kwa lolote litakalotokea. Mimi binafsi nashauri wapenzi wa Chadema wawe watulivu na wapenda amani. Lakini wenye uwezo wa kuepusha vurugu ni wale walio madarakani sasa.

Ahsanteni

CHADEMA is getting their priorities wrong....

Mzee Mtei, anadai JUKUMU KUBWA WALILONALO NI KUFICHUA UOZO WA CCM NA KUCHUNGA KURA......in my view that is a very misguided priority....ni kwa jinsi hii..lazima CHADEMA ishindwe uchaguzi mkuu ujao..kwani chama chochote chenye nia ya kupata ushindi...priority yake ya KWANZA ni KUTAFUTA KURA... Kwanza uzipate kura hizo, then ndio uzilinde..

Kura zinapatikanaje? Kura hazitafutwi kwa njia ya kuelezea mapungufu ya wapinzani wako pekee, na kupandisha jazba....kura zinatafutwa kwa kuwafikia wapiga kura na kuwaelezea mpaka waelewe utawafanyia nini, msimamo wako kuhusu mambo yanayowagusa ni upi......

Wapiga kura wapo wapi?.....80% ya wapiga kura wa Tanzania wapo vijijini...sioni kama CHADEMA wana any mechanism ya kufikia wapiga kura walio wengi...zaidi ya kwenda na helikopta siku moja kupiga debe kisha wanaondoka...... CCM kwa upande mwingine wana mechanism inayowafikia wapiga kura...wana mtandao wa wajumbe wa nyumba kumi kumi, wana mfumo wa uongozi ulio hai FULL-TIME kuanzia kwenye matawi , kata, wilaya, mkoa... Mfumo huo upo active wakati wote kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.....

CHADEMA hawa mfumo imara kama wa CCM, mifumo yao inakuwa active wakati wa vipindi vya uchaguzi na baada ya uchaguzi zinarudi kuwa inactive....ndio maana wameshindwa kuwa na wagombea wenye kukidhi vigezo vinavyotakiwa na tume ya uchaguzi katika MAJIMBO kwa ajili ya nafsi za UBUNGE na UDIWANI..... na ni kwasababu hiyo, wapiga kura hasa walio vijijini hawana attachment na CHAMA husika kwasababu....hawawajui....hawako active kwenye maeneo yao, wakati wa heri na taabu.

Kwa hili...tu lazima tukubali ukweli kwamba, haitokuwa rahisi kwa CHADEMA kupata ushindi ambao wapenzi wake wanatamani upatikane.....ushindi haupatikani by mere wishes...unafanyiwa kazi....wengi wenu mlio USA mnakumbuka...organization ya Barak Obama..iliyoanzia kweye grassroots ndio iliyompa mtaji mkubwa wa kushindana ndani ya CHAMA CHAKE na baadaye kwenye uchaguzi mkuu.....MHESHIMIWA WILBROAD SLAA hana base hiyo.....hata hii FRIENDS OF SLAA imechelewa sana.....ilitakiwa mobilization ya FOS ianze miaka 5 iliyopita...na sio leo hii dakika za lalasalama na kuanza kuchangisha pesa kwenye mkutano wa hadhara....it is too late.....Msidhani uelewa na ushabiki mlionao ndani ya mitandao ya aina hiii.....ndio hali ilivyo kwa wananchi kule Nanyumbu, Msalasala, Iyungo, Kojani, Katavi, Ileje etc etc

Ni kweli wapiga kura siku hizi hawadanganyiki....kama KAULI MBIU YA CHADEMA inavyosema....ni uelewa huo huo wa wapiga kura wasiodanganyika..watatambua kwamba ahadi nyingi zinazotolewa na mgombea wa CHADEMA za kufanya mambo within 100 days ni uongo mtupu....KWELI HAWATADANGANYIKA....

Ushauri wa Bure kwa Chadema:
Wekeni nguvu zenu ku retain majimbo ya Ubunge mliyokuwa nayo last time...na kuweka nguvu kwenye yale majimbo ambayo prospects za kupata ni kubwa...(hasa yale maeneo ambayo wagombea wa CCM wapo weak au yale maeneo ambayo wagombea wenu wapo strong)......KWa kufanya hivyo, mtapata reasonable number of seats itakayowawezesha kuwa Chama Kikuu cha Upinzani Bungeni.....na kwa jinsi hiyo, mtakuwa na suati zaidi ya kutoa constructive criticism kwa serikali.....

Msipofanya hivyo,,,,mkaishia kutawanya nguvu zenu kila mahala.....I can assure you....mtaishia kupata majimbo idadi ile ile ya last time na pengine pungufu zaidi na CUF wataishia kuwa CHAMA KIKUU CHA UPINZANI BUNGENI
 
Karibu jamvini mkuu,

Kwa taarifa yako ni kwamba hata 2005 CCM haikupata asilimia 80! Kinachotakiwa ni kulinda kura za wapenda nchi na hapo CCM kwisheni kabisaaaaa!

Kwahiyo mzee Mtei kanena la mbolea, weka wazi wezi wote na mfumo wanao utumia takribani nusu karne sasa, ili wananchi wamjue mwizi wao na mfilisi nchi yao, kisha linda kura yako watakayo kupigia wancnhi waliochoshwa na wizi/unyonyaji huo!
 
Asante sana Baba mwasisi kwa mawazo yako busara.

Kwakeli mwaka huu Chadema ni kujipanga kweli. Jambo la msingi ni kuwaweka mawakala wa kweli. Kuna hatari ya mafisadi kuweka mapindikizi yao katika vituo vya kupigia kura, wakijifanya ni vijana wa Chadema.

Pia kujihadhari na vijana wasio na msimamo hata kama ni wa Chadema ambao muda wowote wanaweza kuwauzia mafisadi kura zote za wananchi, wakishapewa chochote.

Pia kuhakikisha wote ambao kwa kawaida hawawezi kupiga kura wenyewe husaidiwa kikweli. Niliona uchaguzi uliopita vijana waliandaliwa kuwasaidia wazee ambao hawawezi kupiga kura wenyewe. Kilichokuwa kinafanyika ni kuwa yule mwenye kadi alisindikizwa tu, ila anayepiga kura ni yule kijana aliyenunuliwa na mafisadi. Hiyo ni hatari sana.

Tukizingatia yote haya ukombozi wa mtanzania kutoka mikononi mwa mafisadi ni mwaka huu. Mungu ibariki Tanzania.

Asante tena Baba Mtei kwa hekima na busara zako. Mungu akulinde uweze kuona mtanzania akikombolewa kutoka mikononi mwa wadhalimu, na wala rushwa.
 
Asante sana baba Mtei kwa hekima na busara zako.
Kwa kweli Chadema mwaka huu ni kujizatiti mpaka kieleweke.

Kulinda kura ni pamoja na
-kuepuka vijana mapandikizi ya mafisadi
-kuepuka vijana wasiona msimamo ambao wanaweza kuuza kura muda wowote wakiona fedha
- kuwa makini kwa wapiga kura wanaohitaji msaada kama wazee. Uchaguzi uliopita niliona katika baadhi ya vituo wazee wa namna hiyo walisaidiwa na vijana walioandaliwa na ccm. Kilichokuwa kinaendelea ni kuwa vijana hawa waliwaelekeza hao wazee kuipigia CCM.

Hayo yakizingatiwa ukombozi wa mtanzania mwaka huu utapatikana.

Asante mzee Mtei, tunakuombea Mungu akulinde iliuonje matunda ya ukombozi.

Mungu ibariki Tanzania
 
Msipofanya hivyo,,,,mkaishia kutawanya nguvu zenu kila mahala.....I can assure you....mtaishia kupata majimbo idadi ile ile ya last time na pengine pungufu zaidi na CUF wataishia kuwa CHAMA KIKUU CHA UPINZANI BUNGENI
With a friend like you we do not need an enemy.
 
Mzee Mtei siku zote kumbuka kuwa kumsema mwenzio ni raha saaana na kusemwa wewe ni chungu mno.

Wewe Mwl hakukupa fursa ya kukusikiliza na badala yake ukatimuliwa (though wewe unadai ulishaamua kuacha kazi pia). Au nikuulize, je wakati unatimuliwa kulikuwa na demokrasia? Ulisikilizwa kama ulivyostahili? Je wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kesi zao zipo mahakamani wanaposemwa kwenye majukwaa ya kisiasa unafikiri wanajisikiaje? (nchi yetu ni ya utawala wa kisheria kumbuka) Ungekuwa ni wewe unatuhumiwa tu (na moyoni unajijua hauko fisadi) unaposemwa hadharani utajisikiaje?

Tufikirie leo viongozi au wagombea wa vyama wanaanza kutuhumiana kwa tuhuma binafsi tutakuwa tanatathmini nini? Tuhuma ama hoja za kuleta maendeleo? Kama CCM walivyo na mapungufu hata Chadema pia mnayo, think about tribalism scandals, ufisadi wa Mbowe (two years ago), (au unataka kusema mliliona hilo ndiyo maana mkaamua Mbowe asigombee Uraisi?), uadilifu ktk maisha ya kindoa n.k. Kumbuka kwa kila mahali kuna aina ya watu tofauti tofauti, kuna wazuri na wabaya, wema na wasio wema, wezi na waibiwa, na kadhalika na kadhalika.

Unaweza ukawa mwanzilishi wa Chama ukifikiria kuwaletea watu wako mabadiliko ya kiuchumi kumbe wenzako ulio nao pamoja wanafikiria Chama hicho hicho kitawafanya wachumie matumboni mwao. Kama ilivyo CCM hata nanyi Chadema ni vivyo hivyo. Hata mabadaliko mnayoyasema yataonekana kwa siku 100 ni ndoto tu, its just a gear of bringing political change rather not solving core problems facing our country!

Usitudanganye sana Mzee Mtei! kuwa halisi, Sio wote tunakubaliana na wewe!
Kwa hiyo ufisadi wa viongozi wa CCM ni off limits. Maamuzi aliyofanya Kikwete kuelekea kuukwaa urais hata kama yameliumiza taifa yasifichuliwe. Kwa mtindo huu tutaendelea kutawaliwa na ufisadi hadi kiyama.
 
asante mzee mtei mungu akuongeze hekima na busara '2010 WATZ HATUDANGANYIKI'kuna haka kamsemo 'usituone wavumilivu ukadhani hatusikii maumivu' kweli kananza kudhirika. go slaa go.
 
Nashkuru sana mzee kwa maoni yako mazuri ambayo kama yakifanyiwa kazi yataleta tija. Pia nam-support NEXT LEVEL kwamba ni vizuri sana wana CHADEMA waliojiandikisha wasiache kupiga kura.

Ikiwezekana CHADEMA na stakeholders wake waanzishe mfumo wa ku identify, na kuhakikisha kila mwana CHADEMA aliyejiandikisha kupiga kura basi siku hiyo aende kupiga kura! Yaani kuanzia sasa kila mwana CHADEMA na stakeholders wake [hata silent stakeholders kutoka vyama vingine especially CCM (wenyewe wanajuana nani anampenda Dr Slaa] kila mmoja ahakikishe anamhimiza kuanzia sasa, anachukua ahadi toka kwa anayeahidi kuwa wataongozana siku ya kupiga kura, siku ya kura amkumbushie ile ahadi waliyoweka ya kuongozana nae, and then waende mguu kwa mguu kupiga kura.

Na pia CHADEMA wawe makini na jumla ya matokeo yote ya vituo kwani uwizi hautatokea vituoni tu, bali kiubabe matokeo yanaweza kutangazwa in favour of CCM na viongozi wa usimamizi wa uchaguzi hata kama baadhi ya maeneo CHADEMA wakiwa wameshinda!
 
Mzee mtei sisi wana watanzania tunakushukuru sana, strategies za chadema zisibadilike kwa sasa! mafisadi waanikwe wafunuliwe na wakiendelea kung'aka nifaida zaidi kwetu watanzania. ccm wataendelea ku-defence! chadema iendelee kushambulia na inshaallah mvua ya magoli itaendelea kuwa nyeshea pande zote... SLAA Go go SLAA wetu ...
 
Mzee Mtei heshima kwako,

Mimi ni mtumishi wa umma na kwa kuzingatia ushauri wako, ninahamasisha wafanyakazi wenzangu kukipigia kura Chadema.

Mzee umejitofautisha na wazee wa CCM maana uko uptodate
 
Back
Top Bottom