Elections 2010 Majukumu Makuu ya CHADEMA


Tunajua mmejipanga wengi wa aina yako kama sisimizi. Hapa ni spray tu ya kuwafutilia mbali. Shwain.
 
Watu kama mzee Mtei ni wa kuheshimiwa sana.

Mkuu mzee Mtei unafahamu mengi na tunakuombea Mungu azidi kukupa uhai ili utuoneshe njia ya kuwa na taifa la watu wenye kujua nini wanafanya kuleta maendeleo Tanzania.

Tanzania ya leo si Tanzania ya miaka ya 47, ina watu wenye upeo wa hali ya juu na sasa wanajua kuchambua kati ya pumba na mchele.
 
Unajua haya mapandikizi ya August 2010 wanataka kujenga hoja Chadema haijatapakaa nchi nzima, ili tuwasadiki wakati ule watakapokuwa wameiba kura za vijijini, eti tutaridhika! Hapana ! No no no! Operesheni Sangara imefungua njia na tunajua kabisa kura za vijijini kwingi tu tunazo, ole wenu mkiziiba!
 
Tunajua mmejipanga wengi wa aina yako kama sisimizi. Hapa ni spray tu ya kuwafutilia mbali. Shwain.

Unataka niwaze, nifikiri na nitende kama wewe? Hatujaumbwa hivyo, na ndiyo maana ya kuwa na demokrasia. Leta hoja, acha matusi.

Even if I am young member in the jamii forums I may be knowing it more than you.
 
mimi najitolea kuwa wakala siku ya uchaguzi katika kituo au vituo katika jimbo la kawe dar es salaam, inshaallah
 

Dhana ya 'mapindikizi' ni dhana ya mtu asiyekuwa na hoja...yaani mtu akitoa altenative views basi tayari ni pandikizi....mimi ningekuwa mpenzi wa kweli wa CHADEMA ningefuatilia kwa makini criticism zinazotolewa na kuzifanyia kazi..hata kama hazifurahishi masikio yangu.....sasa wewe subiria matokeo ya OPERESHENI SANGARA.....utashangazwa OCTOBER 31. Hakuna wa kuwaibia chochote....mnaji defeat wenyewe kwa kushindia ndoto ya ushindi pasipo kuwa na mikakati ya kisayansi....... angalieni wapinzani makini wanavyofanya kuchukua nchi.....cheki reference ya Barak Obama alivyofanya.....cheki reference ya NPP ya Ghana na Prof John Atta Mills walivyofanya. Ukweli inabaki pale pale CHADEMA is no where near what NPP was. Nendeni mkajifunze vizuri kwa wenzenu ndio mtaelewa ninachosema...

HAIBIWI KURA MTU YOYOTE......suala ni CHADEMA haijajenga ushawishi wa kutosha na kuaminika kwenye GRASSROOT.... laiti kura zingekuwa zinapigiwa kwenye JAMII FORUM..I can guarantee kwamba mgepata asilimia 110% including na za wizi.... lakini as long as kura zinapigiwa kule vijijini....BADO BADO hamjajipanga vya kutosha.....ANZENI SASA KUJIPANGA KWA AJILI YA 2015...
 

Huo ndiyo ukweli ila unaumiza!!!
 

Hivi wewe unajua historia ya vyama vingi Tanzania? KUDADADEKIIII!!!
Sema vilianza lini na CCM ilianza lini kupora mali zilizojengwa na watanzania wote
 

Kwa uelewa wangu pandikizi...ni stranger asiye belong kwenye kundi Fulani....It is only natural kwa watu wa kundi husika ku resent against stranger huyo kwasababu mtu wa aina hiyo siku zote hakuwa sehemu ya kundi lao, ameibuka ghafla na kujiingiza katika kundi na kuanza kutoa mawazo yake ambayo ni tofauti na mtazamo wa kundi zima....hivi ndivyo baadhi yetu tunavyoonekana ndani ya JAMII FORUM

The same analogy could be drawn kule kwenye mchakato wa uchaguzi majimboni...... CCM imejikita majimboni, ina mfumo ulio active kuanzia wajumbe wa mashina, viongozi wa matawi, viongozi wa kata, viongozi wa wilaya na viongozi wa mkoa.....system yote hii ipo karibu na wananchi..siku zote..ni sehemu ya mfumo wa maisha kule vijijini...... hivyo inapofikia kipindi kama hiki cha uchaguzi....wapiga kura wengi (hasa vijijini) wanaji identify na mfumo waliouzoea, mfumo wanaoishi nao..... mifumo ya ya chadema iliyokuwa inactive miaka yote na kuibuka kipindi cha uchaguzi...kwa formula ile ile ya ndani ya jamii forum niliyoitaja juu......wanakumbana na resentment ya wananchi....hawajui jamaa hawa wanatokea wapi, walikuwa wapi, mbona lugha yao ni ya tofauti na lugha tuliyozoea kuisikia.....and eventually wanawakataaa....hawawapigii kura.

Soooo there you go...CHADEMA needs to build systems kwenye grassroots....kwa sasa hawana system....ndio maana leo inawalazimu heavy weights wale wale akina MARANDO, MPENDAZOE kuhusika na uzinduzi wa kampeni katika kila jimbo...juzi walikuwa Ubungo, Jana walikuwa Kawe, Kesho wataenda Ukonga..hiyo yote ni kwasababu kule majimboni CHADEMA haina watu.....na hili litakuja kuwagharimu sana....haiwezekani Lwakatare amudu vizuri majukumu ya kampeni zake za Ubunge katika jimbo la Bukoba Mjini,wakati huo huo a play a role ya msaidizi wa Mhe. Slaa kwenye kampeni nchi nzima.....kwa hali hiyo, LWAKATARE akishindwa Ubunge Oktoba, utalalamika kweli kwamba ameibiwa KURA? Kwa taarifa nilizonazo...kule Bukoba Mjini, ukiachilia CCM, CUF bado ina grassroot base ambayo ni lazima LWakatare apambane nazo ili kushinda.

Tofauti na hali ilivyo kwa CHADEMA, tukiangalia upande wa CCM....majimbo mengi yameshazindua kampeni zake.....hawakusubiri...Kinana, Msekwa waende kule majimboni kwenye uzinduzi...ni kwasababu systems zipo mpaka kwenye grassroot.....anapopita Mhe. Kikwete kwenye maeneo yale, anachofanya ni kuwawekea uzito zaidi wagombea hao.

Tatizo la CHADEMA kutokuwa na grassroot base linawafanya wazidiwe hata na CUF.....CUF pamoja na kutokuwa na majimbo ya ubunge huku Bara, wanazo grassroot base zao zilizo active..ndio maana in terms of IDADI ya kura...Prof Lipumba hujikuta akipata kura nyingi kuliko mgombea wa CHADEMA..
Until something is done........msitegemeee maajabu yoyote ya ushindi... Na wale wanaodhani OPERESHENI SANGARA italeta impact, ninasikitika kuwaambia....sio rahisi... LAITI MFUMO ULIO ACTIVE TOKA CHINI ungekuwepo...OPERESHENI SANGARA ingekuwa na maana kwani ingekuwa ina invigorate kazi inayofanywa na makada wetu walipo ACTIVE kwenye grassroot on full-time basis....
 

Sinshangai mkuu kwa statistics zako hapa chini, wale wale... tena uko so organized; UMETUMWA!!!!!


salaama
Member
Join Date Wed Aug 2010
Posts 12
Thanks : 0
Thanked 1 Time in 1 Post
Rep Power:becky:
 
..binafsi sipigi kura kwa kuangalia kama chama kina mtandao nchi nzima ama la.

..napigia kura candidate, and this time nadhani Slaa atatufaa.

..rekodi ya utendaji ya Kikwete inadhihirisha wazi kwamba ameshindwa uongozi.

..kama CCM iko karibu na wananchi, basi ni katika kuyakwaza, na kuyahujumu, maendeleo ya wananchi hao.

..I HOPE THIS TIME WANANCHI WATASIKILIZA KWA MAKINI HOJA ZA WAGOMBEA NA KU-JUDGE NANI ATAWAFAA.
 
ukitaka kujua ccm ina mapandikizi ona jinsi yasivyo na adabu hapa. mnashindwa kumheshimu mzee kama Mtei utamheshimu nani? hata kikwete anabidi awe macho nanyi. huenda ni yale ya Nyerere kuwa kikwete akiondoka mtakufa njaa
 


Mwalimu wenu ana matatizo
 

Joka kuu upo sahihi mtu anatakiwa kupiga kura kwa kuangalia sera za chama husika na sifa za mgombea wa chama hicho...lakini kwa mfumo wa siasa tuliopo, wapiga kura walio wengi..hasa wa vijijini bado wanapigia CHAMA...kwa mtaji huu....kura yako na watu wengine wenye mtazamo kama wako hazitoshi kumuingiza Mheshimiwa Dk Slaa IKULU. Hili somo la KUWEKEZA KWENYE GRASROOTS lazima lieleweke ili CHama chochote chenye kutafuta ushindi kifanikiwe barani Afrika.

Hapajawahi kutokea chama cha upinzani kilichopata ushindi simply kwa kufanya siasa za mijini na kwenye mitandao...ukiangalia cases chache za vyama vya upinzani vilivyoshinda uchaguzi na kuchukua dola,source yao kubwa ya ushindi ni GRASSROOT base...angalia kule Zambia Movement for Multiparty Democracy (MMD) cha Chiluba, kilitokea kwenye grassroots....kilipata support ya watu wa migodini na wakulima wa vijijini....ndipo wakaiangusha UNIP. Ukiangalia kule GHANA, the National Democratic Party (NDP) kiliweza kukiondoa chama tawala New Patriotic Party (NPP) kwasababu walikuwa na grassroot base (wao kwakuwa walishawahi kuwa madarakani chini ya General Rawlings) walishakuwa na mizizi kwenye grassroots. Actually ukifuatilia siasa za Ghana utaona kilichokuwa chama tawala (NPP) kilikuwa na wafuasi wengi mijini na kwenye diaspora kama ilivyo Chadema...lakini ndio hivyo...wakang'oka. (cheki allAfrica.com: Ghana: Ruling Party Set for Sweep in National Poll)

Hata ukiangalia kwa jirani zetu Kenya.....KANU ilitawala muda wote kwasababu ilikuwa na base kwenye grassroot...na kuondoka kwake maradarakani kulitokana na SPLIT ya KANU yenyewe.....na siasa za ukabila zilizotawala kwao huko.

To cut the long story short ushindi hauji kwa wishes na ndoto...LAZIMA CHADEMA irudi kwenye grassroots
 
Salaaama,
Mkuu umeandika vitu ambavyo mimi vimenishinda kabisa kufananisha wala kulinganisha.

Kwanza umetumia mifano ya Obama na Prof. John Evans Atta Mills kama mifano bora ya jinsi walivyoweza kufanikiwa. Hivi unachukulia maisha ya Obama na huyo Atta ukilinganisha na maisha ya Dr. Slaa au kitu gani?

Hawa watu, vyama vyao havikuanza jana kushika maradaka ya kuongoza. Yaani wamekuta tayari vyama vimekwisha jineemesha kisiasa na vimestawi iwejke ufananishe na Chadema mabcho hakijawahi kushika madaraka ya kuongoza nchi?..Hicho chama cha Domokratic cha Marekani huwezi kukifananisha na Chadema, na wala kusimama na hicho chama cha NPP ambacho pia umewapongeza.

Halafu navyojua mimi Atta sii kiongozi wa NPP isipokuwa anatoka chama cha NDC, chama alichokuwa akiongoza na Jerry Rawlings..hivyo ujenzi wa chama umeanza toka wakati ule na walisha ongoza nchi kwa muda mrefu kuliko unavyotaka wewe kutuhabarisha. Ingekuwa ushauri bora zaidi kwetu kama ungetumia mfano wa vyama hivi ni jinsi gani walianza hata kuweza kuchukua ushindi kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa tunashabihiana kimazingira na malengo.

Mwisho, hao NPP ambao unasisitiza tuwasome hivi wamefanikiwa kipi haswa cha kufikia wewe kuwazungumzia kama mfano bora...na sidhani kama mazingira yetu yapo sawa kwani kila chama kimeundwa ktk mazingira yake, watu wake nam malengo tofauti hivyo muundo wa itikadi hauwezi kufanana..
 

Kaka Mkandara, kwanza niombe radhi kwa mixup ya NDC na NPP...nashukuru kwa kusaihisha..
Pili naomba nitofautiane na wewe, suala la chama kuwa kikongwe sio automatic ticket ya kuweza kuji organize na kupata ushindi...laiti ukongwe ungekuwa ndio kigezo cha organization, basi KANU isingeanguka mara mbili toka itoke madarakani na UNIP isingeanguka zaidi ya mara nne toka kitoke madarakani...na hivi ni vyama vikongwe vyenye historia tangu enzi za kumtoa mkoloni..

Kwa mtazamo wangu kinacho matter...sio uzee, wala uchanga wa chama...kinacho matter ni kuwa na ORGANIZATION na mikakati inayokiwezesha chama kuwafikia walengwa (wapiga kura)....hicho ndicho MMD ya ZAMBIA walifanya...na hicho ndicho CHADEMA wanaweza kufanya 2015 na huko mbeleni....ila kwa sasa CHADEMA HAIJAWAFIKIA WAPIGA KURA VIJIJIN na HIVYO USHINDI 2010 NI NDOTO....

Anzeni kazi ya kujijenga sasa, na baada ya uchaguzi....MWISHO wa uchaguzi ndio usiwe mwisho wa ujenzi wa chama kwenye grassroots....
 
Bila samahani.. ndio tupo hapa kujadili na sii kubishana.. karibu sana mkuu wangu. Kwa hiyo maelezo yako yote ya kwanza hayana nguvu kama utaamini ukongwe sio kigezo isipokuwa ni kuwafikia wananchi (wapiga kura) vijijini?.

Pili, nafikiri Chadema wamefanya mengi kuwafikia wananchi vijijini kuliko hata hivyo vyama ulivyovisema. Sasa kama swala ni mikakati ya kuwafikia wananchi wa vijijini sidhani kama vyama vyote ulivyovitaja vimeweza kufanya zaidi ya Chadema pasipo ukongwe wao ktk siasa..Hao MMD unaozungumzia wao walikuwa na agenda moja tu. Nayo ni kuwaondoa UNIP madarakani jambo ambalo Chadema wamejipanga pia wakiwa na lengo hilo hilo.

Na sii kweli kwamba MMD waliweza kuwafikia wananchi wapiga kura vijijini isipokuwa wananchi wenyewe wa Zambia walitaka CHANGE ya uongozi baada ya Kaunda na UNIP kushindwa kuwaletea maendeleo kwa zaidi ya miaka 40 ya utawala wao. Wakaelewa malengo ya chama kipya na viongozi waliokimbia UNIP tofauti na sisi. Kwa hiyo utaona kwamba tofauti iliyopo baina ya Zambia, Kenya, Ghana au hata Marekani na sisi ipo kwa wananchi wenyewe.

Watanzania kwa uzoba wetu bado tunafikiria kwamba hakuna jema linaloweza patikana wakitoka CCM. Bado tuna mawazo mgando ya yaliyogandishwa toka tupate Uhuru na Changes zozote zile za kiutawala zitaondoa Unyenyekevu na amani (utumwa wa fikra) hivyo kuhofia kutokitegemea chama CCM kwa maendeleo ya nchi yetu..Kwa maana kwamba akili ya mtumwa siku zote humtazama na kulinda maslahi ya bwana (master) wake ili apate riziki yake..Na ndicho kinachoendelea hadi leo kiasi kwamba hata Chadema wafanye nini bado wapo watu wenye mtazamo unaotisha yaani pasipo CCM (masters) hakuna maisha..

Chadema wameweza kuanzisha operation Sangara hadi vijijini lakini nambie ni Watanzania wangapi wanataka hata kujua yaliyomo ktk operation hiyo. Na sii ajabu nazungumza na wewe hapa lakini hujawahi kupitia Operation Sangara na kufahamu mafundisho yake yaani siasa kwetu imekuwa kama dini. Wapo waislaam au Wakristu hawajawahi maishani mwao kushika kitabu cha dini nyingine hata kusoma tu kufahamu kina maagizo gani...

Hata baada ya Chadema kuwapeni wananchi Ilani yao ya uchaguzi bado wengi wana amini Chadema haijawafikia wananchi vijijini hali huwezi kunambia hata sehemu moja iwe kata au nyumba kumi Kitaifa wasiojua kuna chama Chadema na kina malengo ya kuwaondoa CCM madarakani. Ila sema tu kwamba katika sehemu zote hizo vijijini, wananchi wengi wamebatizwa ktk jina la CCM na hawaoni imani nyingine zaidi ya CCM kiasi kwamba sii jukumu la Chadema tena kuwalazimisha wananchi wapate kuifuata.

Chadema wamezungumzia umuhimu wa kuwaondoa CCM madarakani, lakini nambie ni Watanzania wangapi (wapiga kura) wako tayari kuona hilo linatokea! nadhani utasema sii wengi lakini nakuhakikishia kwamba mwaka huu, CCM wana wakati mgumu sana kisiasa kwa sababu wananchi wengi wamechoka na ndio maana hata wewe umezungumzia zaidi hofu yako kwa Chadema kuliko wakati mwingine wowote sawa na mzazi ambaye kaambiwa na mwanaye kwa mara ya kwanza kuwa amepata mchumba!...Mkuu wangu Chadema imefikia muda wa kuchukua majukumu mazito na hakuna muda wa kufikiria kujipanga hadi vijijini ambako sii swala la kuweka majengo isipokuwa IMANI ya kubadilisha uongozi wa nchi yetu kwa mara ya kwanza baada ya CCM kushindwa kuyafikisha maendeleo kwa wananchi vijijini..

Tazama mikutano yooote ya CCM, kwa waliohudhuria utagundua kwamba asilimia kubwa wamevaa magwanda ya kijani na njano..yaani wanachama. Umati mkubwa umelembwa na rangi za chama tofauti na Chadema ambao utawaona walalahoi wapiga kura wakihudhuria mikutano yao kupokea ilani ya chama wakati ile ya CCM wengi wanakuja kumwona rais wao kwa mara ya kwanza baada ya kuishi Ulaya (ooops) kwa muda mrefu.

Kikubwa sio swala la Chadema kushindana na CCM kuwafikia wananchi vijijini ila ni Chadema kuwapelekea maendeleo wananchi wa vijijini..
 
Uchaguzi kila mara ni deal kwa watu wanaogombea uongozi hakuna hata mmoja anayejali maslahi ya wananchi, ukipiga kura unawaongezea nguvu walaji wajisifu kuwa tumepata kura nyingi lakini hakuna lolote. Kuna tofauti kidogo au afadhali tu lakini sio kwamba wanatujali kwa sana. Kuanzia wabunge mpaka hao wanaokimbilia Ikulu hakuna demokrasia ya kweli. Kiongozi akishachaguliwa anahama mji wake anahamia jiji lenye maraha mpaka siku za uchaguzi zifike tena. Mbunge wa Arusha haishi safari za Dar es salaam na hii ni kwa majimbo mengi tu Tanzania.Mpaka hii leo hakuna mbunge yeyote aliyewahi kuthubutu kukaa kwenye mji wake na kujaribu kuwasiliana na kukusanya mawazo na kero za waliomchagua kwamba sasa hivi kipindi cha bunge kimewadia je tukazungumze nini? In Fact mtu anaamka asubuhi anafika kwenye kikao anasema yake tu yaliyomjia siku hiyo bora kasema tu na kibaya zaidi unawaona wengine kwenye kikao wanadiriki kusinzia. Nchi sijui inakwenda wapi na sijui tufanyeje wajirekebishe hawa. tunataka maendeleo ubinafsi umepitwa na wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…