siku zote tunasema waziri mwandamizi (rasimu) waziri mkuu (katiba) atakuwa na wajibu wa kudhibiti na usimamizi wa shughuli za kila siku.
lipo tatizo la sisi kutokuwa na mfumo wa kitaifa unaoeleweka wa ni jinsi gani kiongozi huyu anaweza kutimiza majukumu yake.
ni jambo la busara sana kama tutaanzisha taasisi ya kupanga na kudhibiti uchumi hapa na hiki ndicho chombo cha kumsaidia waziri huyu kutimiza majukumu yake.
hapa tunatakiwa kuunda chombo kikubwa cha kitaifa ambacho kinapanga mipango ya uchumi na kudhibiti uchumi wetu.
waziri mkuu au waziri mwandamizi hawezi kutimiza majukumu yake kama hana chombo ambacho kinajihusisha katika sekita zote kikiangalia mwenendo wa nchi na kutoa dira ya utekelezaji wa shughuli za serikali, kufuatilia utekelezaji na kutoa maagizo.
ki msingi waziri hapa anakuwa msemaji wa chombo hiki lakini lazima kuwe na chombo kinachofanya kazi hiyo.
kuchelewa kwetu kuunda chombo hiki au kutokuunda chombo hiki kumemfanya waziri mkuu au kutamfanya waziri mwandamizi kushindwa kutimiza wajibu wake na atakuwepo tu.
kimsingi mipango ya nchi inatakiwa kuanzia katika chombo kimoja cha kitaifa ambacho kinaangalia tuna nini, kinaangalia ili tuweze kupata mafanikio ya haraka tupitie njia ipi ambayo ni fast katika kupata best result.
bila chombo hiki taifa litaendelea kubahatisha na katika kubahatisha hatuwezi kupata maendeleo.
hebu angalia mfano mdogo tu wa tatizo la foleni za dar es salaam.
hili ni tatizo ambalo linatakiwa kutatuliwa na mchumi na sio engineer.
mchumi hapa anaangalia tatizo la foleni limetokana na nini? je tuna magari mengi kuliko uwezo wetu? au tuna barabara kidogo kuliko magari tunayohitaji?
hapa yawezekana tumeshindwa kudhibiti sekita ya magari na watanzania wananunua magari mengi kuliko uchumi wa nchi unavyoweza kuhimili. kumbuka magari yanachota fedha zetu kupeleka kwa watengeneza magari na vipuri vyake, magari haya yanachota fedha zetu kupeleka kwa wachimba mafuta lakini magari haya tunayahitaji ili kutusaidia katika usafiri.
hapa tunahitaji kudhibiti magari haya kiuchumi ili tusinunue magari mengi kupita tunavyohitaji na kuathiri uchumi wetu lakini vilevile tusiwe na magari kidogo kuliko tunavyohitaji na kuathiri uchumi wetu.
hapa tunahitaji taasisi ya kukaa chini ikaangalia jiji la dar es salaam linahitaji magari ya aina gani na kwa kiwango gani ili kuondoa tatizo la usafiri.
chombo hiki kitaangalia barabara ya gongo la mboto kuja mjini mfano tukiwa na mabasi mengi ya kubeba ya kubeba abiria kuanzia 45 na kuendelea barabarani kuelekea maeneo tofauti ya jiji na magari kidogo ya binafsi ambayo yamebeba wastani wa abiria 2 je kiuchumi imekaaje kwa maana ya foleni au mda wa abiria kutoka gongo la mboto kwenda mjini, kwa maana mfumo huu una impact gani kifedha kwa maana kwa mwaka tutapoteza fedha kiasi gani kwenda kwa watengeneza magari na wazalisha mafuta.
alafu kinaangalia mfumo mwingine wa kuwa na magari madogo ya binafsi ya wastani abiria 2 mengi na mabasi ya kati na makubwa kidogo kinaangalia impact yake kiuchumi na kinaangalia scenario nyingi.
alafu kinaangalia utekelezaji wake kwa maana
kwa kuangalia kila chombo kinachohusika jinsi kinavyochangia katika sekita hiyo.
mchango wa serikali kuu na vyombo vyake kuanzia mipango, sheria za kodi, mamlaka za udhibiti na mengine, sekita binafsi.
alafu kinatoa dira ya mpango wa kukabiliana na tatizo hilo na hilo anapewa waziri mkuu na yeye sasa ndipo anaagiza wizara husika kila moja jambo la kufanya katika kutatua tatizo hilo na kuwapa time frame huku yeye akiwa amekwishapanga vipaumbele kifedha kutokana na picha ya sekita zote kitaifa inayoandaliwa na chombo hiki.
yawezekana matatizo ya sekita ya usafirishaji dar kwa sasa ni ugonjwa wa presha kiuchumi ambao unatokana na ununuzi holela wa magari ya binafsi na hivyo suluhisho ni serikali kudhibiti ununuzi wa magari ya binafsi kupitia kodi na tozo mbalimbali, kuhamasisha ununuzi wa magari ya jamii kwa kupunguza ushuru na gharama za uendeshaji.
lakini ukimueleza mhandisi au wizara ya ujenzi kutatua tatizo hilo yeye anaangalia foleni na kuona suluhisho ni kuongeza ukubwa wa barabara ili magari yapite mengi zaidi. hii yawezekana na kuwa ni sawa na kuumwa na ukaenda kwa maabara ukaambiwa tatizo una mafuta mengi mwili na ukienda kutafuta suluhisho lake kutoka kwa mwanamahesabu na sio dakitari anaweza kukushauri kuongeza uzito wa mwili ili ratio ya mafuta na mwili vikae katika uwiano mzuri kumbe ndio utakuwa unaongeza tatizo zaidi.
mfumo wa kodi unaweza kudhibiti tatizo la foleni pengine bila kuhitaji kupanua barabara. kupanua barabara ni jambo zuri lakini lazima tuelewe kuwa kuwa na wafanyakazi mfano laki tano katika jiji la dar ambao kila siku wanachoma mafuta ya 15,000 kwenda kazini na kurudi, wakitumia magari yanayohitaji mainteance ni hasara kwa taifa kuliko kama tuaweza kuwapunguza hawa na kubakiza laki moja tu na hawa laki nne wakapanda usafiri wa umma na kulipa jumla pengine 2000 tu.
tutaokoa fedha nyingi isiende kwa wazalisha mafuta, tutaondoa magari mengi barabarani hivyo barabara zetu zinaweza kutosha, tutaokoa fedha nyingi isiende kwa watengeneza magari.
kwa mfumo wetu wa sasa sioni jinsi waziri mkuu anavyoweza kudhibiti jambo hilo bali yeye atasubiri wizara ya ujenzi waseme tupanue barabara zetu, atasubiri wizara ya fedha ifanye mipango ya kupata fedha za kupanua barabara. hapa sioni waziri mkuu akidhibiti bali kusimamia yale wizara zimependekeza.
lakini ili yeye waziri mkuu aweze kudhibiti lazima tatizo hilo lianzie kwake na yeye kwa kuwa yuko katika wizara zote ndiye wa kuangalia tatizo hili tunalitatua kupitia njia au nyanja ipi na anatoa maagizo kama ni tra rekebisha mfumo wa kodi tunataka kupunguza magari ya binafsi, sumatra tunataka jiji la dar liwe na mabasi idadi kadhaa na kabla ya mtu kuagiza gari la abiria anangalia takwimu pengine ni njia gani zenye mapungufu na ni mabasi ya aina gani kama ni madogo, au makubwa au ya kati maana bila kuyadhibiti hayo pia yanaweza kununuliwa zaidi pale itakapoonekana ni biashara nzuri na hapo tunakuwa hatujafanya kitu katika fedha zinazokwenda kwa watengeneza magari.
takukuru na polisi wanaagizwa nini ili taasisi hizi ambazo zinaagizwa kudhibiti uchumi zisitumie hali ya mabadiliko yatayojitokeza ambayo kwa wananchi kabla ya kuizoe wataona kama ni crisis na inaweza kuchochea vitendo vya rushwa katika taasisi zinahusika katika mpango moja kwa moja na kuharibu mipango.
na baada ya mda anaangalia utekelezaji wa mipango.
kwa njia hii waziri mkuu kweli atakuwa anatimiza wajibu wake.
si vyema kuacha maelezo haya mafupi ya kwenye katiba kila mmoja atakayeshika madaraka atekeleze yeye anavyotaka. tutakuja kuwa na hali ya kiuchumi kama mipangilio ya miji yetu kwa maana huyu anaweza kulitia mkazo jambo hili na yule ana la kwake.
tunayo nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri kiuchumi lakini kupitia mipango, bila ya kuweka dira hasa kwa kuunda chombo tutayumbishwa sana kwa kila serikali inayoingia inataka kufanya inavyotaka yenyewe. huyu anakuta miradi fulani ilikuwa imeanza anaitelekeza na kuanzisha ya kwake, kila mmoja anawaza sekita fulani ndio niipe kipaumbele bila wachumi wa nchi kutathmini mpango na kumueleza mweshimiwa kuwa matokeo ya mpango wako ni hivi lakini kuna mpango mwingine matokeo yake ni haya.
ni vema tuunde chombo cha kudhibiti na kusimamia uchumi kikatiba na chombo hiki ndio chombo cha kumsaidia waziri mkuu kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa ibara ya 100 rasimu.