Majukwaa ya kuuza bidhaa kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni yasaidia kuuza matunda ncini China

Majukwaa ya kuuza bidhaa kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni yasaidia kuuza matunda ncini China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Mkulima Wu Liuhong kutoka mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China, alipanda miplamu kwenye eneo la zaidi ya hekta 13.3 mwaka 2017, na mwaka huu amepata zaidi ya kilo laki moja za matunda. Lakini uuzaji wa matunda yake unasuasua kutokana na watu wote kupata mavuno mazuri mwaka huu.

Kwa bahati nzuri, timu ya uuzaji wa bidhaa kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni imemsaidia kuuza matunda yake. “Wauzaji maarufu mtandaoni” waliingia kwenye bustani ya Wu kuanzia tarehe 19 mwezi Julai, na kumsaidia kuuza matunda ya plamu zaidi ya kilo elfu saba kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni, Wu amepata yuan zaidi ya elfu 50 (sawa na dola 7,410 za kimarekani).

VCG111393538657.jpg

VCG111393538658.jpg
 
Back
Top Bottom