Kama hujui, Marekani ilikuwa namba moja kwa uchimbaji wa mafuta duniani kutokakna na hydraulic fracturing. Hii teknolojia ni ghali sana, makampuni ya uchimbaji yamekuwa yakikopa benki ili kuendesha hii biashara. Ili makampuni hayo yaweze kujiendesha, inabidi bei ya mafuta iwe $50 (break even point). Sasa hivi bei ya pipa ni chini ya $20.
Urusi na Saudia wanaendelea kushindana bei ya mafuta kwa kuyajaza kwenye soko, soko ambalo halina wateja, watu wengi wako majumbani. Tuombe Mungu tuu, hali itakuwa mbaya siku zijazo, hii corona imeongezea kuni tuu.
Makampuni mengi yatahitaji bailout, kitu ambacho hakitawezekana sasa, usione watu wajinga kununua bunduki kwa wingi kipindi hiki, wanaelewa kinaweza nuka muda wowote.