Majumba ya kifahari ndani ya pori hapa Arusha ni mfano wa kuigwa

Majumba ya kifahari ndani ya pori hapa Arusha ni mfano wa kuigwa

menny terry

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
509
Reaction score
670
Wakuu,

Waswahili wanasema tembea uone! Katika pitapita zangu kama vlogger huku Arusha nimekutana na majumba ya kifahari, viwanja vya Golf, mito ya maji safi, wanyama mbalimbali na makazi yenye ubora wa hali ya juu vyote vikiwa ndani ya pori! Yaani wakati tunabanana hapo mwananyamala na Manzese huku Arusha kuna watu wanaishi kwenye pori kwa kujinafasi huku wakila fresh Air na kupishana na wanyama wa kila aina.



Makazi haya ni mfano mzuri wa kuigwa kwamba hatuhitaji kufyeka miji yetu ili kupata eneo la makazi.

Sema kikubwa kilicho nisikitisha ni kuwa aslimia 90% ya wakazi wa eneo hili ni wazungu tupu!

Jioni utawaona wakiteremka kutoka kwenye majumba yao kwenda kucheza Golf. Wamatumbi wenzangu ni wakuhesabu.
 
Hapo ni Kiligolf unaingilia Maji ya Chai. Mbona kawaida sana, halafu umepita kiangazi ungepita masika ungeona uzuri wa uumbaji wa Mungu.
 
Kwa bahati mbaya wamiliki si Watanzania vijana wa Arusha chukueni hii kama chachu ya kupambana zaidi badala ya kukimbilia kuolewa na wageni.

Kufanikiwa Maisha si mpaka ujidhalilishe kwa kuuza utu wako. Asante.
 
emoji16.png
emoji16.png
wamatumbi wasubirie picnic utawakuta wamesambaza bia
 
Njoeni Handeni kwasunga muwekeze kuna maeneo mazuri sana....Kwasunga iko karibu na Miono ...
 
Back
Top Bottom