Majumuisho kesi Mbowe, Kinyang'anyiro ni katika DR

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kesho Inshallah, mawakili wasomi watawasilisha majumuisho yao mbele ya Jaji Tiganga.

Msingi wa kinyang'anyiro bila shaka utakuwa katika uhalali wa Detention Registers (DR). Moja kutokea Central Police Dar na nyingine kutokea kituo cha Polisi Tazara.

DR ya Central iliwasilishwa na D/C Msemwa aliyedai kuwa akilitumikia jeshi la polisi kutokea Central katika kipindi hicho. Ya Tazara, ikiwasilishwa na mkuu wa sasa kituoni hapo.

Hata hivyo shahidi wa utetezi Lembrus Mchome anadai D/C Msema hakuwahi kuwa central polisi kipindi hicho bali alikuwa Oysterbay polisi. Kwamba yeye akiwa mahabusu D/C Msemwa, askari H4323 alimhudumia mara kwa mara Oysterbay Polisi.

Ya Lembrus Mchome yanaweza kuwa na nafuu kwani ni madogo!

Funga kazi ni ya komando Mhina. Mhina anadai kuwa Tazara na baadaye kupelekwa mahakamani kutokea hapo.

Alikuwapo Tazara Polisi mahabusu 23/9/2020 - 25/9/2020 lakini hayumo popote kwenye DR ya Tazara:





Wasaa wa Jaji kuithibitishia dunia kuwa mahakama ni huru na yenye hukumu za haki kwa mara nyingine unajongea.
 
Wasaa wa Jaji kuithibitishia dunia kuwa mahakama ni huru na yenye hukumu za haki kwa mara nyingine unajongea.[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
..kesho mawakili wa pande zote wanawasilisha majumuisho ya hoja zao.

..December 14 ndiyo siku ambayo Jaji atatoa maamuzi ya kesi ndogo ndani ya kesi kubwa.
Duuh!
 
Detention register waliitupa wakatengeneza mpya wakajikuta baadhi ya majina hayapo😅😅😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…