Majuto ni mjukuu: Jokate anajuta kuifahamu CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426

Huyu dada baada ya kuingia kwenye siasa za majungu za UVCCM, wananchi kwa umoja wao waliamua kuachana na bidhaa zake za " KIDOTI " zikiwemo rasta na mawigi , kwa wakati ule haikumgusa sana kwa vile bado alitambulika kama kiongozi ndani ya UVCCM ( Taasisi ya vijana inayosifika kwa rushwa kwenye eneo la maziwa makuu ).

Sasa baada ya kutimuliwa mithili ya nyau aliyekunywa maziwa ya mtoto njiti, hali yake ni tete mno! Walio karibu naye wanasimulia jinsi alivyokumbwa na msongo wa mawazo.

Ukisoma vizuri maandiko matakatifu utaelewa kwamba hata siku moja Mungu hataniwi, huyu akifahamu kwamba CCM ndiye adui wa wateja wa bidhaa zake akaamua kuungana nayo kitu kilichosababisha kifo chake kisiasa na kiuchumi.

Pole dada.


Soma zaidi hapa; Mwenyekiti UVCCM, Kheri James ametengua Uteuzi wa Kaimu Katibu Idara ya Uhamasishaji, Jokate Mwegelo
 
Ata nape alikomaaaa watu wakashinda lakn badae mbele ya media kanyooshewa bastola [emoji1][emoji1][emoji1]ccm ya wawili mkulu na mwanawe wa dar
 
Ata nape alikomaaaa watu wakashinda lakn badae mbele ya media kanyooshewa bastola [emoji1][emoji1][emoji1]ccm ya wawili mkulu na mwanawe wa dar
Siasa ni mchezo mchafu, hata Dr silaa tuliona ktk chama fulani, hivyo kuwa mwanasiasa kubali lolote kwa wakati wowote.
 
Siasa siyo baba, mama au ndugu, siasa ni kazi kama kazi zingine tu, waweza kuacha ccm au act au hata chadema wakati wowote ule..
Ila baba, mama, ndugu na familia hawaachiki..
Kila la heri Jokate..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…