Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Huyu dada baada ya kuingia kwenye siasa za majungu za UVCCM, wananchi kwa umoja wao waliamua kuachana na bidhaa zake za " KIDOTI " zikiwemo rasta na mawigi , kwa wakati ule haikumgusa sana kwa vile bado alitambulika kama kiongozi ndani ya UVCCM ( Taasisi ya vijana inayosifika kwa rushwa kwenye eneo la maziwa makuu ).
Sasa baada ya kutimuliwa mithili ya nyau aliyekunywa maziwa ya mtoto njiti, hali yake ni tete mno! Walio karibu naye wanasimulia jinsi alivyokumbwa na msongo wa mawazo.
Ukisoma vizuri maandiko matakatifu utaelewa kwamba hata siku moja Mungu hataniwi, huyu akifahamu kwamba CCM ndiye adui wa wateja wa bidhaa zake akaamua kuungana nayo kitu kilichosababisha kifo chake kisiasa na kiuchumi.
Pole dada.
Soma zaidi hapa; Mwenyekiti UVCCM, Kheri James ametengua Uteuzi wa Kaimu Katibu Idara ya Uhamasishaji, Jokate Mwegelo