STAMICO kusherehekea miaka 50, imezalisha makaa ya mawe rafiki kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Makaa yana ufanisi mkubwa na huwaka kwa muda mrefu kuliko mkaa wa kawaida.
Pia husaidia katika utunzaji wa mazingira maana yatazuia ukataji wa miti hovyo.
BEI yake ni rafiki pia kwani yatapatikana kwa
Reja reja 1000/ kwa Kilo 1
Jumla 800/ kwa Kilo 1
Yanatumika kwenye majiko haya haya ya mkaa? kama wanaweza kukidhi mahitaji makubwa ya soko hasa maeneo ya mijini huenda ukawa mwarobaini wa kupunguza uteketezaji miti kwa ajili ya kuzalisha mkaa.
Ni jambo zuri. Ingawa elimu inahitajika sana kwa wale Watanzania wasuo na taarifa! wale wa maeneo ya pembezoni, na wanaotegemea zaidi nishati ya kuni na mkaa wa kawaida.