Makabi Lilepo, Mshambuliaji bora kwa Afrika kwa sasa

Smart AJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
5,564
Reaction score
5,884
Jamaa linajua sana, linapiga free kick za kikubwa sana. Juzi limewatungua Waarabu, jana cotton sports wamelizwa kwa magoli makali yote.

Nadhani huyu jamaa hatasalia tena Al Hilal baada ya mashindano kuisha.

Screenshot_20230225-033708_Chrome.jpg
 
Naona bado ana miaka 25 tu, mapacha wa Kariakoo wachangamke!

Hawa ndo washambuliaji sasa, ni clinical kwenye lango la mpinzani
 
Naona bado ana miaka 25 tu, mapacha wa Kariakoo wachangamke!

Huyu si ndiye tulisikia kasajiliwa kwa bilioni moja? Timu za Kariakoo bado hazijafikia huko
 
Jamaa linajua sana, linapiga free kick za kikubwa sana. Juzi limewatungua Waarabu, jana cotton sports wamelizwa kwa magoli makali yote.

Nadhani huyu jamaa hatasalia tena Al Hilal baada ya mashindano kuisha.

View attachment 2529124
Hawezi kuwa Mshambuliaji bora kwa Afrika labda kama unaangalia timu moja tu.

Wapo washambuliaji wengi tu level yake au zaidi, sema kwa mashindano haya yuko form tu lakini siyo kuwa Mshambuliaji bora Afrika.
1. Mailula ana goli tatu mpaka sasa
2. Lilepo ana goli tatu
3. Patient Wassou ana goli mbili
Jaures Ngombe ana goli mbili
4. Khabba ana goli tatu.

Halafu Lilepo awe bora kuliko hao wote ?
 
Naona bado ana miaka 25 tu, mapacha wa Kariakoo wachangamke!

Shida yao katika kufoji umri... sura zimekomaa sanaaaa lakini umri utaambiwa ni 25...!

Hawa watu salute
 
Timu zetu tz Zina kazi, Jana kulikuwa na mbugi ya wydad na Petro de Luanda, Petro de Luanda unaona kabisa Hawa wana quality ya wachezaji ambao wanaweza kuifunga timu yoyote afrika na muda wowote ule.
 
Unasema Petro de Luanda wana quality ya wachezaji ya kuifunga timu yoyote Africa lakini tambua hao wana point 4 tu hadi sasa katika mechi tatu. Ligi si rahisi hivyo
 
Wana points nne Kwa sababu wamekutana na wenzao wanaokaribiana, kundi lao ni gumu sana laiti kama zingekuwa timu nyingine Sasa hivi tungeongelea point sifuri kwao, kimsingi quality wanayo, wana mechi mbili nyumbani chochote kinaweza tokea, ukiangalia kabisa unawaona Hawa wako level Moja na timu kubwa nyingine za afrika hivyo si rahisi kusema kuwa atafungwa kirahisi hata ugenini, ni timu inayoweza kukupa tumaini la bao muda wowote.
 
Unasema Petro de Luanda wana quality ya wachezaji ya kuifunga timu yoyote Africa lakini tambua hao wana point 4 tu hadi sasa katika mechi tatu. Ligi si rahisi hivyo
mkuu Ni kweli ana point 4 sema ana kundi gumu mpaka hapo kajtahd lakin game za nyumban anafanya vzuriii Zaid
 
Unasema Petro de Luanda wana quality ya wachezaji ya kuifunga timu yoyote Africa lakini tambua hao wana point 4 tu hadi sasa katika mechi tatu. Ligi si rahisi hivyo
Kundi la Petro Luanda siyo gumu lina timu mbili dhaifu, As Vita na JSK halafu Wydad msmu huu yupo hovyo.

Elewa komenti ya mdau hapo ligi ni ngumu hao petro Luanda hawana timu ya kutisha kihivyo.
 
Back
Top Bottom