Makabila ya Tanzania: Tamaduni zao na Historia yao

Kwa ufupi makabila ya Arusha yote yanashida sana na pia hayapendani/ hawasemani vizuri hata kidogo
 
Nadhani kutokana na tamaduni zao mila hata desturi kwa kiwango kikubwa kushabihana na wachaga nao pia waweza kuwa wachaga
 
Huu uzi aliyeuanzisha alitaka kujua na kufahamishana kuhusu makabila yetu asili zake,tamaduni zake ,mwingiliano/uhusiano kati ya kabila na kabila.
Lakini ukachafuliwa hata haueleweki mwelekeo wake.
Ni kurasa nne tu za mwanzo na mbili za mwisho angalau na mtu unaweza pata kitu cha maana. JF inasikitisha sana.
 
mnanitia aibu jamani... Wanyakyusa hawana asili ya Afrika Kusini...
MM ni school of thought tuu maana wapo ambao husema wanatokea Sudan uko wakiassociate na Nubian Queen no wonder majina ya watoto hutokea kikeni
 
MM ni school of thought tuu maana wapo ambao husema wanatokea Sudan uko wakiassociate na Nubian Queen no wonder majina ya watoto hutokea kikeni

1. Kwa nini Wameru wanasemwa ni wakorofi?

Maeneo mengi ya Tanzania, wameru husemwa kama watu wakorofi, wajeuri, wasioaminika na mengine mengi yanayofanana na hayo. Ukweli ni kwamba wameru ni watu wapole sana na wenye ukarimu wa hali ya juu. Jambo ambalo halina ubishi ni kwamba mmeru hakubali hata kidogo kuonewa. Kwa mmeru nyeusi ni nyeusi na si vinginevyo. Historia yao pia inawaingiza kwa bahati mbaya katika haya. Kwa muda mrefu kabla na wakati wa ukoloni wameru wamekuwa kwenye vita. Wamasai na wachaga ni kati ya makabila yaliyopambna na wameru sana kabla ya ukoloni. Wakati wa ukoloni walipambana sana na wakoloni na ilifikia mahali ambapo askari wa kichaga walikodiwa na wajerumani kuja kupambana meru. Viongozi wengi pia walinyongwa hadharani.

Hili na mengine liliwafanya wawe ni watu wa kujihami na kutoendekeza watu wasio wajua. Ndo maana hata dini za kikristo zilichelewa maru kwani wamissionari wengi sana waliua na hivyo kuogopa kufika meru kwa haraka.

Wameru wana umoja na misimamo isiyobadilika kwa mambo wanayoamini, hii imedhihirika kisaisa, kiutamaduni na hata kiuchumi. Mila zao hazijabadilika sana kwa muda mrefu; ni eneo ammabalo kwa sasa kuna adhabu ya viboko 70 kwa wale wote wanaokikuka misingi iliyokubaliwa katika jamii yao.

Wameru ni watu wachapa kazi sana na kwa hakika kuanzia waume kwa wake wote kazi ndo jadi yao. Wanalima na kufuga kisasa pia. Kwa ujumla kama ukiwa dar utakuwa unakula nyanya na vitunguu vinavyolimwa meru; arusha na maeneo jirani yote yanalishwa na wameru kwa maziwa, nyama, mbogamboga na matunda.

Kielimu, wameru hawakuwa na shule nyingi ila hata hivyo kuna wasomi wa kutosha meru. Ukipata nafasi soma kitabu cha “blood in our land” cha profesa mbise.



Naweza kuhitimisha kwa kusema, ikiwa wewe ni mtu mababaishaji huwezi kukaa na mmeru ama meru, ila ukiwa mtu mkweli, mchapa kazi na imara utafurahia sana kukaa na mmeru na kuwa sehemu ya wameru.
 
Wapo pale NCCA au NCAA...

Mengine sisemi
 
Ila kwa ukatili hawa jamaa nawavulia kofia maana ukienda ARUSHA issue zao zimekaa kibandidu.
Ati wabaweza nunua mapanga mji mzima kisa kuna mahala wanaenda fyeka migomba kisa mgogolo wa mipaka.
 
Wambulu wananywele kama za waethiopia/wasomali, kwa wanaume wanapenda pombe sana hasa za kienyeji(mangure).Kwa watoto wa kike sio wachoyo kwa vitu walivyopewa bure na mungu nadhani umenipata mtu mzima.




Mkuu mbona takwimu zinaonesha manyara na kigoma ukimwi ni asilimia moja tu unlike mbeya,iringa,kagera,sasa huo uchoyo usikwepo impact yake nini?
 
Umeelezea vizuri sana
 
Ni muhimu sana kufuatilia historia ya makabila yetu.
 
Naomba nijulishwe kabila ili chimbuko lake ni wapi?na tabia za kabila ili.Je hivi kweli ni wacha Mungu maana kila MTU ni mlokole.Nikipa hayo ntarudi kuwaeleza kwanini?
 
Mkuu ahsante kwa kutuwakilisha vyema "Sisi wameru tunasemaga (Ekanu Dei) "Ahsante sana
 
Wadau hasa wajita, naomba maelezo ikibidi hata picha kuhusu mavazi ya kitamaduni ya wanaume wa kijita. Natanguliza shukrani
 
Wanajukwaa amani kwenu.

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza ningependa kufahamu maisha halisi ya kabila la Wakurya, mila na desturi zao. Bila shaka Wakurya wapo humu na ningependa kujifunza namna walivyo kama nilivyotangulia kusema hapo awali.

Karibu tuelimishane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…