Makabila ya Tanzania: Tamaduni zao na Historia yao

Umenena vema
 
Hivi hivi mnafeli mitihani unaulizwa kitu kingine unajibu kingine.

Kuna Koo Fulani zinatokea maeneo ya kiagata na Silorisimba hao ndio nafahamu Wanaoa binamu zao.

Kwetu hapana maana ningeenda kuoa moja ya binamu zangu maana watoto mashallah..
Nipe mimi mkuu binamu yako MUMOCHAAA
 
Kuna wenye chura mkuu nije kuoa, maana dah
 
Mkuu ina maana Wairaqw nio Wambulu na wadatooga?
Oh mkuu Wadatoga wengi wanakifahamu kiiraqwi na sehemu walipo wadatoga na wairaqwi wapo hata historian wanasema wote wametokea Ethiopia wakirandana
 
Hii thread namuona kiwia na mumewe kilewo,mhhhh acha sisi wandereko tutakuja na thread nyingine haya kina matimbwa,njechere,malinda,ulongo,jongo,mkumba,lumbwe,ngomango,kitutya,kwangaya,ngoro,ngorwe,ngwere,dambaya,mtupa,kulita,kihambwe,chembera,koliti,lwambo,msengwa,pamba, haya mje huku
 
Psychiatry with religion
 
Utazani nilisikia watu wote duniani walitoka tz kama sikosei
 
Datooga ndio Wamang'ati na ndio wabarbaig. Hawa ni ndugu ya wanandi wa Kenya.
 
This is not directly relevant to this thread, but it is helpful:

Raia mzawa halisi wa Tanzania ni yule ambaye alikutwa hapa na Wajerumani. Kwahiyo ukisikia Karl Peters aliingia mkataba na chifu Fulani au chifu Fulani alikataa kuingia mkataba na Karl Peters basi ujue kuwa makabila ya hao machifu ni wazawa halisi wa Tanganyika. Between 1885-1890 Tanganyika ilikuwa chini ya German East Africa company ya Karl Peters.

Kuwa more precise mzawa halisi ni yule ambaye yupo ndani ya mipaka ya Tanganyika by 1891, ambapo Tanganyika ilikuwa formally koloni la serikali ya Ujerumani.

Vile vile mtu aliekua Tanganyika by 1961 alipewa uraia wa Tanganyika automatically. Sera hii ili lenga ku avoid kuwa bagua wageni ambao walikuja au waliletwa na wakoloni Tanganyika. Kwa mfano, mtu ambae aliletwa na wajerumani Tanganyika kumwambia arudi kwao mwaka 1961 ingekua sio vizuri, na unaweza kukuta alisha kusahau huko mababu zake walikotoka.

Kila kabila lina ingia kwenye nchi ya Tanganyika na ardhi yake. Vile vile linaondoka kwenye nchi ya Tanganyika na ardhi yake. Kwa mfano Wagogo wanaingia Tanganyika na ardhi yao ya Ugogo ya Dodoma, na wanaondoka na ardhi yao. Huwezi kuwaondoa Wagogo Dodoma halafu ukabaki na ardhi yao kwa kisingizio cha utaifa. Kama hutaki Wagogo Tanganyika basi usiitake na ardhi yao pia. Hivyo hivyo kwa makabila mengine wamakonde, wachagga etc. Au uwaondoe wachagga Moshi na ubaki na mlima Kilimanjaro Tanzania. Wachagga wanaingia Tanganyika na Tanzania na ardhi yao na mlima wao na wakitoka wanaondoka na ardhi yao na mlima wao. Wasukuma, wakurya nao hivyo hivyo. Sio vizuri kutenganisha watu na ardhi yao ya jadi, hata kama utawapeleka sehemu nyingine ndani ya nchi.

Tukiazima mfano wa kibiblia, hii inafanana kwa mfano na Israel wakati wa agano la kale, atokee mfalme wa Israel, awanyang’anye kabila la Yudah ardhi yao kwa kisingizio cha utaifa wa Israel. Au atokee kiongozi wa kabila la Yudah awanyanganye wanaukoo Fulani wa kabila la Yudah ardhi yao kwa kisingizio cha maslahi mapana ya kabila la Yudah. Haya hayatakuwa mazuri kibiblia.

Watu wanaweza kutenganishwa na ardhi yao kwa kupitia itikadi ya mrengo wa kushoto, wa kati au wa kulia. Kwa Mfano unaweza kusema unawaamisha wazanzibari wote kutoka Zanzibar ilikupisha shamba kubwa la karafuu la kijamaa la serikali au ili kumpisha mwekezaji mkubwa wa hoteli kutoka ndani au nje au ili kuhifadhi mazingira ya bahari au ili kujenga umoja wa kitaifa. Baadhi ya sababu hizi zinaweza kuonekana ni za kizalendo, au nzuri kiuchumi, au nzuri kimazingira, lakini kiukweli ni kwamba zitawaumiza wazanzibari na kuwanyang’anya ardhi yao ya jadi.

Kuna situations ambapo ardhi ya makabila inatumika na wengine. Kama makabila kutenga maeneo yao kuwa miji na majiji ilikurahisisha muingiliano wa kiutawala na kiuchumi. Makabila yenye shortage ya ardhi kuhamia kwa wenye surplus ya ardhi etc (hata hapa pia kabila wazawa linatakiwa kuwa na ardhi nyingi na muhimu kuliko kabila wahamiaji).

Kwenye ardhi pia dhana ya next of kin ni muhimu (ndugu wa karibu). Mfano wakifa bushmen (San) wote wa Republic of South Africa, next of kin wao ni wabantu wa South Africa, so hao ndio watairithi ardhi yao. Akitokea mtu mwingine kutoka bara lingine akajifanya ndio mrithi wa hiyo ardhi, ita fanya watu wagune. Au wakifa wa Scotland wote Scotland, next of kin wao ni wacelts au wa irish au waingereza ambao watairithi ardhi yao. Vivyo hivyo akitokea mtu mwingine kutoka bara lingine akajifanya ndio mrithi wa hiyo ardhi, ita fanya watu wagune. So kabila Fulani likifa kabila ndugu la karibu yake ndio wanakua warithi wa hio ardhi.


Maranyingi mabeberu na watu wanao jenga empires ndio hua hawa pendi dhana hiyo ya ardhi hapo juu.

Kwa mfano, anakuja mfalme wa Assyria anawahamisha taifa zima kutoka sehemu moja na kulipeleka sehemu nyingine. Ili kuwafanya hao watu wasiwe na mizizi na wamtegemee yeye.

Kuconclude raia mzawa halisi wa Tanzania ni yule ambaye alikutwa hapa na Wajerumani. Na makabila halisi ya wazawa ni yale ambayo yalikutwa hapa na Mjerumani. Vile vile mtu aliekua Tanganyika by 1961 alipewa uraia wa Tanganyika automatically.
 
Ukabila utawatesa sana, at the end of the day mtagundua kwamba mengi mnayojaribu kuyatafiti,either Yana ukweli kidogo , hayana uhakika Sana au ni ya uongo kabisa. Tatizo hapa ni kwamba makabila mengi ya kiafrika (ukiacha yale yenye asili ya kush na Arabic) njia zao za kurekodi historia zilikua primitive .
wali record historia yao orally zaidi. Mimi nikiwa mzawa wa wachagga, kwa Muda mrefu nimekua nikitafiti asili (origin) yetu, mnamo mwaka 2008 nikiwa naishi south Korea nitembelea chuo kikuu cha seoul. Nikaingia maktaba ya Afrika ya chuo. Nikakuta wamarekani kule wameacha baadhi ya vitabu. Moja Kati ya kitabu kilichonivutia ni hiki kilichofanya niwaeleze habari hii.Kitabu chenyewe kinaitwa "The history of The chagga people of Kilimanjato before 16 century by Prof Arthur Murdoch". Kitabu chenyewe kina Emphasize Origin, customs,and culture of the Tribe. Hilo la asili ya wachagga lipo very complicated kuliko mnavyoweza kufikiri. Ila pamoja na yote unabakia ukweli kwamba The chaggas are the Combination of many tribes. main clusters zikiwa Ongamo (Origin of the tribe from ethiopia highlands) Kambas, Maasais, and Taita . kitabu hiki chenye takriban 3000 pages kinaelezea history of chaggas back to 11 century AD. kolichoniacha Hoi zaidi ni kwamba wazungu wanatufahamu vizuri kuliko sisi wenyewe tunavyojijua. Wakati silabasi zetu mashuleni zinazungumzia our history after year 1840, wao wazungu wanatuzungumzia before year 1200... .. kumbe wachagga wa Mwanzo. hawakutokea Congo wala Dodoma, wala hawakua bantus. Ila baada ya 17century koo za mwanzo za kibantu zilianza kuchanganyika na Hawa early chaggas. Kwamba warangi wahamitiki (wanaojulikana kama wasi) walikua neighbors wa hawa wachagga na asili Yao ni kilimanjaro.,tena waliishi maeneo ya kuanzia Himo kuzungukia ,Ryatta , Lotima hadi holili.(hata haya majina Yana sound ki hamitili zaidi ) ..hii inatupa jibu jingine kwamba hata majina ya maeneo na vitongoji vingi vya kilimanjaro yalikua ya ki hamitiki.maeneo ya Marangu kwetu Kuna majina kama Toor,Aris, na mengiineyo mengi ,majina ambayo haya sound bantu kabisa. Kumbe hata nyuso za hawa ndugu zangu wachagga wa leo zina define origin yao.Hembu Watizame wengi nyuso zao ni narrow jee pua zao???. Wao Mungu wanamwita RUWA. wambulu (Hammites) wao Mungu wanamwita RUWOR( it sounds the same) majirani zetu wapare Mungu wanamwita MULUNGU (tofauti)Either kwenye kitabu hiki tunaelezwa jinsi kabla ya 14century walivyokua tayariwameanza ku apply irrigation way of farming, tofauti kabisa na bantus wengine. Kwamba hata kabla ya their southern bantu neighbors yaani pares, sambaas ziguas and Bondeis,hawajaform chiefdormships wao tayari walikua na wamangi. Kuna jambo moja lilinishangaza zaidi kwamba hata Hao Ancient chaggas walipokuja kule nao walikuta wenyeji waliojulikana kama wa umbo au Wateremba. Ambao walikua pygmies Hawa waliishi huku walipo wachagga leo, (kwenye mwanzo wa miinuko) walikua na nywele za singa, alafu kule juu misituni waliishi wengine wakiitwa wakonyingo ambao walikua ni jamii ya Kongo Pygmies . Hivyo new comers walipokuja Wali walifukuzia mbali wenyeji walowakuta. Hivyo basi Kutokana na historia hii fupi tunapata conclusion kwamba Hawa bantus wanao claim kwamba ndio the owners of the Land nao pia sio watangulizi hapa. Hii historia niliyotafiti inahusiana na kabila langu ila naamini" even the history of other tribes ,all around this country sounds the same." Hivyobasi mwenye haki ya ku claim kwamba hii nchi ni yake ya asili ni MBILIKIMO tuu na si mwingine. NB: nipo kwenye hatua za mwisho kutoa kitabu kitakacho kuwa na simulizi nyingi ambazo zitakusaidia kuelewa mengi kama utahitaji kuelewa.
 
Yapo makabila mengi Tanzania yanafika adi 130 kwa makadrio
mengine ni kama
.1.WALUO
2.WAMERU
3.WAKURYA
4.NYASA
5.WAKAMBA
6.NYASA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…