Makabila ya Tanzania: Tamaduni zao na Historia yao

Makabila ya Tanzania: Tamaduni zao na Historia yao

Doubtless to say, Malawi inayo mahusiano ya karibu sana na Wanyakyusa kama ilivyo kwa Wangoni na Wawemba kule Zambia, lakini kumbuka hata sasa wanyakyusa wa Kyela na wale wa Tukuyu wanayo tofauti kubwa tu, ikiashiria pia tofauti ya asili zao.

Wapo wanyakyusa wenye asili ya Ukinga, Usangu, Malawi kule Karonga (Kumbuka mkoa wa Karonga wanaongea Kinyakyusa na ndicho kinachoitwa Nyakyusa Ngonde). Lakini wengi sana wanaongelea asili kuwa Mahenge.

Inasemekana waliamua kuondoka pale kwa sababu ya vita ya kikabila. Lakini pia majanga ya asili ya mazingira yanawezekana. Ninachojiuliza, ikiwa wanajiita Waluguru kwa asili yao, Mahenge kuna Waluguru?

Naambiwa walianza kuchanja mbuga kupitia kwa Wahehe na Wasangu (ndio maana ni watani zao) kisha wakajichimbia kundi moja pale Suma (pana msitu mkubwa sana wa makaburi - isyeto) ambapo miili ya watu wazima na viongozi wao wengi imelala hata leo - japo hapajapewa tunu kihistoria. Wengine kwa mtawanyiko uliosababishwa na Melele wa Wasangu aliyetumiwa na waarabu kupata watumwa, walijikuta wanakimbilia uelekea wa Zambia na wakajificha milimani ndio Undali na baadaye wakateremkia Rungwe na kukutana na wenzao. Hata pale Suma walitawanyika sababu Melele aliendelea kuwasarandia, mke mkuwa wa kiongozi wao Kyusa akaendelea kusini hadi Masoko, wengine kama Ngosi na wanae wakaenda mashariki. Inadaiwa mpiganaji mmoja Kitunda Mjaba alijichimbia mlimani Livingston. Akaoa wake sita ambao uzao wake ndio kina Mwangosi, Mwakatobe, Mwakajila, Mwandumbya, Mwakipesile (?). Hao waliitwa kwa majina ya mama zao ambao pia kuepusha magonvi kati yao wenyewe kwa wenyewe mzee aliwatawanya akabakia na mke mkubwa Ngosi pale kilimani na wanae, ndio maana ya Mbanyangosi...........

Waliokwenda Masoko na Kyusa waliandamana na Nsasu ambaye alienda Mpata mlimani Kyejo karibuna machimbo ya sasa ya gesi, nao wakaongezeka kwenda Ipinda na Kyela kukutana na wengine waliotokea Malawi na wengine wakaenda Makwale na Matema wakakutana na Wakinga na kuchanganyika. Inasemwa ndi maana hata Kinyakyusa cha Matema, Mwakaleli, Masoko, Kiwira ni tofauti sana, wenyewe wanajuana wanapoongea.

Kuna haja ya kujua zaidi, historia ya watu hawa kwa faida ya vizazi vijavy. Mjerumani MONICA ndiye pekee aliyechimbachimba sana historia na utamaduni wa wanyakyusa, lakini hakutoa nakala nyingi, nadhani ilikuwa ni mfumo wa ripoti na sio kitabu cha kuuza. Hakuna bookshop iliyo na kitabu hicho maana hawakutoa chapa nyingine baada ya yeye kufariki. Alikuwa katika harakati za kutafuta namna ya kueneza Injili kati ya watu hawa.

Leka
You have made my day gwe nyambala ugwe. That's my ipso facto history, really it is hard to find a true history of the same, but, though little, I give 99 plus per cent. Gundunile kanunu fijo. Stay blessed na kweli jf inatia moyo.
 
interesting...
Khantwe njoo huku uniambie asili yako ni ipi mama!
 
Last edited by a moderator:
Wakuu nimekaa na wameru kimeru kinafanana mno na kimachame kwa asilimia 98% nauliza je wameru ni wachaga?majibu please
 
Wameru wametokea uchagan mwanzo walikua wachaga wote kuna baadh ya koo tunashare na wachaga
 
Truly asili ya wameru ni wachaga na pia kuna story ndefu inayoelexea ukwel huo ipo Google
 
Kila baada ya dakika chache kuna post zinatuhusu humu. Imekuwa kero aisee... Moderators mpo?
 
Wakuu nimekaa na wameru kimeru kinafanana mno na kimachame kwa asilimia 98% nauliza je wameru ni wachaga?majibu please

Subiri kwanza warudi krismas ndo watakujibu, hawa wangine walobaki ni wazaramo tu watakudanganya
 
Wameru ni wachaga pia. Kuna makundi kazaa ya wachaga ambayo ni warombo, wamarangu, wakibosho, wamachame, wauru na wameru.
 
yeah wameru ni wachaga waliopo arusha, kimeru kinafanana na kirombo, kimarangu, kimachame n.k
 
Ndio bosi kama kina urio wapo wachaga na wameru
 
Nina swali pia.Hivi hao wameru watz na wameru wa huku Kenya wanoshi sehemu za mlima Kenya wana uhusiano?Wameru wanielimishe tafadhali.
 
Wamefanana mambo mengi jografia,luga,kilimo,utamaduni,desturi pia wameru ni wachapakazi sana
 
Back
Top Bottom