Makachu divers wahamia Dar baada ya kutimuliwa Zanziber

Makachu divers wahamia Dar baada ya kutimuliwa Zanziber

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
16,054
Reaction score
11,568
Hawa jamaa Makachu divers wamejizolea sifa nyingi zanziber lakini ghafla serikali ya zanziber imesitisha huu mchezo. Ila nasikia wamehamia coco beach.

Kabla ya kuruhusu huu mchezo ni bora kuangalia yaliyosababisha ukafungiwa zanziber yasijejitokeza na huku. Pili huu mchezo ni kama hatarishi kwani mtu asiyekuwa na ujuzi wa kuogelea anaweza zama na kupoteza maisha

Tatu, upo uwezekano waovu wanaojulikana kama beach boys wakautumia vibaya na kuleta taharuki kwenye jamii.

Nne, ni vyema kila jambo linalofanyika nchini lifanyike kwa uratibu ili kulinda usalama na maudhui ya watu, huu mchezo huchezwa huku wakijirekodi na kurusha mitandaoni, ni vyema maudhui haya yakaratibiwa.
 
Back
Top Bottom